Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa nyumba kumi na viongozi wa mashina na matawi ya CCM katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam, mchana, ubungo Plaza ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa TANU na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa Wilson Mukama baada ya kuingia ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam leo mchana na kuongea na wajumbe wa nyumba kumi-kumi katika kuadhimisha kuzaliwa kwa TANU
Viongozi wa nyumba kumi na viongozi wa mashina na matawi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo
Wakimshangilia Kikwete
Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihamasisha mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akizungumza akwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, Msekwa na Mukama wakimfurahia mmoja wa waasisi wa TANU kati ya watatu walio hai, Mzee Costantine Milinga (90) alipokuwa akieleza alivyoshiriki kuanzisha chama hicho. Alikuwa miongoni mwa waasisi 17 walioanzisha TANU mwaka 1954, na hivi sasa walio hai ni watatu tu
Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru naye akapata fursa kueleza alivyojiunga na TANU. Picha na Bashir Nkoromo
hata kama umesema nisichafue hali ya hewa.... hivi kweli imeshindikana kuwawekea viti jamani...? hivi CCM haijui kwamba hao ndio wako karibu kabisa na wananchi/wapiga kura wao?
ReplyDeleteJamani hao wa Ubungo plaza walipeleka wapi viti?????? Wajumbe wa shina wanakaa chini katika karne hii ya 21? Hii naona ni dharau kwa wajumbe wa shina!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMdau
Kweli hawa wajumbe wa nyumba kumi kumi hawathaminiwi.
ReplyDeleteKukaa chini siyo dharau ndiyo maana hata baadhi ya ibada za watu wengine nao hukaa chuni na kwa kweli ndiyo wengi kwenye ngazi hiyo ya uongozi wa CCM.
ReplyDeleteJamani hawa wajumbe ndio muhimu kwa kuimarisha chama lakini wanawekwa chini hivi kwa nini jukwaa kuu wasikae nao chini iwe kama style mpya, wamewadhalilisha wajumbe kwenye hotel kubwa kama hii afadhali ingekuwa uwanja wa biafra kinondoni tungeelewa.
ReplyDelete