Baadhi ya mawaziri wakimpongea waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jummanne Maghembe mara baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara yake jana jioni katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge baada ya kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge baada ya kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na baadhi ya wabunge wa upinzani Moses Machari (kulia), Philipa Mturano (katikati) na Ezekia Wenje (kushoto) baada ya Filikunjombe kumwambia Wenje kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto ) na Maryam Msabaha (katikati) baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na Mbunge wa viti Maalum (CHADEMA) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti Maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) na Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini (NCCR – MAGEUZI) Moses Machari baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Pwani Subira Mgalu (kulia) akimsikiliza mbunge wa Buchosa (CCM) Dkt. Charles Tizeba nje ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.Picha na Anna Nkinda - Maelezo,Dodoma.
CHADEMA SASA MIE HAPA NDIO KWA MARA YA KWANZA NIMEWAVUNJIA HESHIMA BORA KUENDELEA NA MAISHA KUJALI MTAANI KWAKO MTUU NA JAMII KWAM SAADA WA MOYO KULIKO KUSUBIRI HIVI VYAMA BORA UTIZAME FAMILIA NA JAMII KULIKO HIVI VYAM, CHADEMA SASA NDIO NAO WANAJIONESHA WANA UCHU MMBAYA WAKUTAKA MADARAKA WAMEIGEUZA NJE YA BUNGE KAMA JUKWAA LA TAARAB MDUARA WA MISUTO NI AIBU, SASA MWISHO WATAKUWA KAMA CCM. NYIE NI WATU WENYE ELIMU JIWEKENI INAVYOTAKIWA SIO HII MISUTI YA VIDOLE MMPAKA WANAUME BWANA. JAMAL.
ReplyDeleteBunge linapokuja kibarazani......
ReplyDeleteHivyo ndivyo inavyotakiwa hakuna haja ya kuwaheshimu CCM, wamezidi wanaongoza nchi kibambe sana, mi napenda viongozi kama mbunge wa Nyamagana, maana hawa CCM bila kulazimisha jambo watatutokea puan CCM wanakera sana. Sasa hizo samaki ziko nchini na inaelekea aliyeagiza ni kiongozi wa CCM< yeye hajali afya za watanzania maana anajua yeye na watoto na watoto wa nduguze hawatakula hizo samaki. ndo maana mbungeni hawataki hizo choko choko. Mi nimechoka na chama tawala jamani, watanzania tunateseka bila sababu, wakati Mungu ametubariki kwa vitu kibao.
ReplyDeletebalaa kilo saba na nusu, mungu ibarikiwe tanzania. tunakokwenda ni mbali. lakini haya ni mambo ya utandawazi ndio nyerere alisema tusiwe na tv kwasababu naona hawa wabunge wamechungulia sana youtube huko kuna filamu za wabunge wa korea, singapore, wakenya na waturuki wakipigana bungeni basi na wao, wanasutana!?
ReplyDelete- - -
buffalo,
new york
Jamani hivi bungeni kunakusutana? Mbona wabunge wetu wanatudhalilisha kiasi hiki? Kwani sheria za bunge si ziko wazi??? Kama huyo mbunge alivunja sheria au kumkosea ustaarabu kuna kosa gani mheshimiwa Filikunjombe to stand saying the truth?? Na kama huyo mbuge wa Chadema hakufanya kosa lolote kwa nini alitolewa nje. Yale yale kama ya huku Marekani watu wanaanza kutekeleza mambo muhimu ya bunge kwa kuangalia mbunge huyu ni mwenzangu wa Chadema au CCM. Hata mungu ametuamuru kusema ukweli. Hivi wanatambua uzito wa kiapo walichoapa baada ya wananchi kuwapigia kura. GO TO THE BUNGE AND DO THE RIGHT THING STAND BEHIND SHERIA TARATIBU ZA BUNGE ZIPO WAZI NA KILA MTU HUYO HURU KUMKOSOA MTU YEYOTE ANAYEVUNJA SHERIA BILA KUJALI ITIKADI YAO THIS IS TRU POLITICS SIO KUSUTANA KAMA WATOTO WASHULE NJE YA UKUMBI, IF YOU HAVE POINT RAISE IT INSIDE THE BUNGE SESSION RUNING UNDER REGULATIONS. THIS IS WHY UPINZANI WILL CONTINUE TO LOOSE. HEMBU ANGALIA HIZI PICHA. WHAT A SHAME???????????????? MIJITU MIZIMA INAACT KAMA ILITERATE!!!! NDIYO MAANA HUWA NAJIULIZA HAWA WANAOJIITA MA DOCTOR PROF KWELI WAMETHIBITISHWA KUWA WALISOMA HIZO DEGREE, UKIELIMIKA LAZIMA U-BEHAVE AS SUCH!
ReplyDeleteIT'S SAD!
duh hii kali keshokutwa tutageuka bunge la japan ngumi kwa kwenda mbele
ReplyDeleteMliotangulia wooote mmeruka hoja ya msingi, kuna suala la watanzania kula samaki wenye radioactive, hiyo consignment ya tani 124.9 imeingia Tanzania na awali TFDA kupitia maafisa wake walikubali ipite na wao hao baadaye wanaizuia huku zaid ya tani 3.5 zikiwa imeshaingia sokoni. Sasa kama ikigundulika ni kweli hao samaki wanaradioactive na tayari wananchi wenzetu wameshakula itakuaje? Binafsi suala la kumkalisha mbunge chini au kusutwa kwa Filikunjombe kama alivyoandika hapa ripota sioni kama linauzito zaidi ya afya za watanzania wenzangu ambao wapo hatarini kupata madhala kutokana na radioactive kama ikithibitika ni kweli zipo (mimi nashawishika kutokana na bei ya samaki hao kua chini. Kwa mimi kama raia wa kawaida ambaye nimesitisha kula samaki nikihofia hiyo hali tete ningependa kuungana na Ezekia Wenje bila kujali itikadi za vyama katika kujua ukweli halisi wa kimaabala kuhusu usalama wa samaki hao. Sioni kama kunakosa kwa Wenje kutokana na umuhimu wa alichokiuliza kuwa na faida zaidi kwa watanzania( hasa wa dar,moro na kilombero huko na sio nyamagana jimboni kwake), hata kama lilikuwepo basi ingetumika golden rule kuweka mambo sawa ili wala samaki kama mimi tuweze kujua ukweli na mustakabala wa wale watu wa kwanza toka TFDA walioruhusu kuingizwa huo mzigo wanawajibika vipi, Ninyi wenyewe mnapata picha gani juu ya mamlaka hii muhimu kutokana na mkanganyiko huu, kumbuka kuna vitu vingapi wnahusika navyo hawa watu wa TFDA viingiavyo toka nje? Jaribuni kujadili mambo kwa mapana zaidi na si kuingia kwenye mitego ya kisiasa maana hapa mi nimeon issue ni je samaki wanaradioactive hawana? kama wanayo je mnaipersive vipi hii mamlaka nyeti hivi? je kama hawana hii contradiction inatoa picha gani kwenu Watanzania?
ReplyDeleteToba mpaka Vidole juu kama wanaimba mipasho ya Khadiaja kopa?? Kweli bunge limepata watu. Spika Mama Anna unaona yanayotokea nje ya milango ya bunge????Mbona enzi hizo za Bunge likikutana Dar viwanja vyote vya bunge ni eneo la heshima ya hali ya juu, nilikuwa mdogo nikiwa ndani ya gari kumshusha dingi alikuwa mbunge na once tukiingia kwenye drive-way tuu utaona wabunge wamekaa vikundi na mijadala ikiendelea kwa amani na utulivu na utaona kwamba kulikuwa na ulinzi wa hali ya juu na hakuna anayejaribu kufanya misuto kama hii. I'm sure walikuwa wanapayuka kama vile wako sokoni, jamani eneo hili linapaswa kuheshimiwa. Picha zinaonyesha kama ilikuwa karibu na lango kuu, Spika hembu tufafanulie hili in terms of jurisdiction na mambo yasiyotakiwa kufanyika katika maeneo ya bunge, what if anayesutwa akahamaki akamtandika konde mtu? Ina maana ngumi zitaanguka kama China? Kaaaaaaaaaaaaaaa.
ReplyDeletesamaki wa sumu nasikia wapo mitaani kila kona,lakini poa tu maana hakuna atayezaa tena baada ya hapa, maana viongozi washatuchoka wacha tufe wabakie wao wamalize rasilimali za nchi.
ReplyDeletevyakula vya sumu kibao vipo bongo now toka japan,baada ya miaka kadhaa ndio tutakimbiana
ReplyDeletekama watu wanaweza kuuza supu ya ng'ombe waliokufa ,hawashindwi kuuza samaki zenye mionzi ya sumu
Viongozi wetu ni wataalam sana wa kuandika bajeti na jinsi zinavyotumika kwenye makaratasi,lakini waambie kutatua tatizo la maji ambalo kuna mabomba,mabwawa,mito,maziwa,you name it -humuoni hata mmoja na madegree yao yote wanatia kapuni.
ReplyDeleteANOY WA 08.33 AFAHAMU PIA KWAMBA HATA HUYO MWENYE JINA LA REFU ANGEWEZA KUTOA HILO ANGALIZO LAKE NDANI YA BUNGE KWA NINI ALIENDA KUWEKA CHUMVI KWENYE KIDONDA? UKWELI UNABAKI PALE PALE KWAMBA JAMAA ALIKUWA ANAMWIGIZA MAKINDA ALIKUWA AMETAHADHARISHWA KUHUSU SUALA LA SAMAKI WA SUMU NDIO MAANA ALIMSHTUKIA WANJE KUWA ANATAKA KULIPUA BOMU AKAKATAA KUMPA RUHUSA YA KUTOA MAONI. WATU WANA UCHUNGU NA NCHI YAO SIO TU KUANGALIA MIAKA 50 YA UHURU HALAFU LEO PAMOJA NA KUWA NA BAHARI NA MAZIWA NA SAMAKI KIBAO BADO ETI MNAAGIZA SAMAKI KUTOKA NJE TENA WENYE SUMU HALAFU BADO MNAJARIBU KULINDANA TU. ZAMANI WAKATI WA CHAMA KIMOJA, BUNGE LA CCM LILIKUWA NA KAZI YA UKWELI WALIYOTUMWA NA WANANCHI YA KUIKOSOA SERIKALI (UNAKUMBUKA ENZI ZA KINA MREMA, SANGA G50?). LAKINI KWA SASA HALI IMEBADILIKA. LAKINI KWA BUNGE AU WABUNGE WA SASA WA CCM KAZI YAO KUBWA NI KUITETEA SERIKALI NA HIVYO KAZI YA WABUNGE WA UPINZANI NDIYO IMEKUWA YA KUWATETEA WANANCHI WALIOWACHAGUA. SASA MISAMAKI INA MIONZI UNAILETA TZ KUWALISHA WATANZANIA HALAFU WABUNGE WENYE KUONA MBALI KAMA WENJE WAKAE KIMYA TU. FUNGENI MACHO JAMANI NYIE WENGINE MNAKAA ULAYA NA MAREKANI TU HAMJUI KWAMBA NCHI YETU INA MATATIZO. HUO MSUTO NI SIZE YAKE KABISA NA UZURI WAPIGA KURA WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO WANALIONA HILI MTAWAKUMBUKA 2015 MTAJUA KAMA ANAYESUTWA NA ANAYESUTA NANI YUKO SAHIHI
ReplyDeletemliotoa maoni na kuilaumu CHADEMA sijui kama mnajuwa tatizo lilikuwa nini au mnataka kuona kuwa kila kinachosemwa na vyama vya upinzani nikosa sasa mnapoelekea nikuwa akili zinazidi kudumaa.Watanzania hatuitaji kuburuzwa kama hatuna watetezi tunawashukuru wabunge wa upinzani kusimamia m,asirahi ya Watanzania.Pia kuhusu usomi wao nadhani toka mwaka juzi watu waliandika degreee za wabunge na mawaziri wa CCM degree zao feki siwao wala chama kilichopinga.
ReplyDeletewewe anony wa 08:33, style yako ya arguments inasema mengi kuhusu wewe! nadhani ungetoa kwanza boriti kwenye jicho lako ndio utaona vibanzi kwa wenzio.......hivi uliona mchakato wote bungeni au ndio ma expert behind computers na kujifanya unajua kila kitu! wewe unafahamu madhara ya hao samaki toka Japani??? wacheni partisan politics...wewe ndio uta ''LOOSE'' but a TZ wont lose...
ReplyDeleteHapa watu mnawasema chadema bure, hiyo picha ilipiogwa bunge likiwa linaendelea ndani, WQenje akiwa katoka na wabunge wengine wa upinzani wa CHADEMA, NCCR NA CUF walitoka wakimuunga mkono Wenje, huyo mbunge wa CCM alitoka kushabikia kutolewa kwa Wenje ndio akakutana na hao viti maalum maaan hawana majimbo
ReplyDeleteIkumbukwe Mwenyekiti wa kamati ya Bunge alitambua alifdanya kosa na kumrejesha Wenje kwa kisingizio cha ubinadamu.
Do not comment kama hauna fact na kutegemea Picha.
Huyo deo wacha asutwe tu,maana ameacha wilaya yake inakufa kazi kujiproud tu mbele za watu,hana lolote huyo,upeo wake mdogo sana.
ReplyDeleteYan badala ya kuongelea swala la samaki matu wanaongelea misuto. jamani samaki wana sumu hao inayosababisha kansa.hivi kwani tumeishiwa na samaki mpaka tu import frm FUKUSHIMA.WA CCM UTAWAJUA TU HAWANA POINT KABISAAA
ReplyDeleteKUNA MIJITU HUMU NDANI HAINA AKILI KABISA TENA WEWE ULISEMA SIJUI CHADEMA NINI KOMAAAAAAA PEPO WEWE,WEWE UNAJUA MADHARA YA HIZO SAMAKI???? KAA CHINI UFIKIRIE ZIMEINGIAJE HUMU NCHINI KAMA SI UFISADI WA MTU MMOJA KUTAKA KUTUUA NA HAO SAMAKI, CHADEMA WAMEFANYA JAMBO LA BUSARA SANA KUTOKA NJE KWANINI SPIKA ASEMA YULE MBUNGE AKAE CHINI WALIONA ATATOBOA SIRI EEEEEEE SASA 2015 AMA ZAO CCM AMA ZETU WANANCHI TUMECHOKAAAAAAAAAAAAA NA MAOVU YA HAWA VIONGOZI MAFISADI MAVITAMBI TUU NAKUJILIMBIKIZIA MALI NDIO TABIA ZENU ,TUNATESEKA VITU VINAPANDA MAISHA MAGUMU NYIE KWENU BURUDANI SASA SISI SIO WANANCHI WA KARNE ILE SASA HIVI TUNA AKILI TIMAMU
ReplyDeleteEEEEeeeeeh! Kazi kweli kweli, kumbe waheshimiwa kwa mipasho hawajamboo!
ReplyDelete