Makamu Mwenyekiti  wa Simba Sc Nyange Kaburu na Afisa Habari wa Yanga Louis Sendeu wakifurahia vifaa vipya vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 70 walivyokabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Kilimanjaro Lager ikiwa ni sehemu ya udhamini wa TBL  kwa timu hizo kongwe, tayari kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom inayoanza mwezi ujao. Shoto ni Meneja wa kilaji hicho george Kavishe
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira nchini TFF, Angetile Osiah, akiongea wakati wa hafla hiyo
 George Kavishe akikabidhi vifaa vya Yanga
 George Kavishe akikabidhi vifaa vya simba
 George Kavishe akiongea
 Viongozi wa Yanga, Simba na TFF wakionesha vifaa hivyo
Wachezaji wa Simba na Yanga wakionesha vifa.
Picha zote na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2011

    JAMANI TOENI MAONI YETU KWENYE MTANDAO, MBONA MNABAGUA MAONI YA KUTOA WAKATI SISI WADAU INAPASWA TUJADILIANE NA NDIO MAANA YA BLOG

    Wanachofanya TBL ni kuangamiza mpira, Bia zao zinanywewa nchi nzima na wapenzi wa Simba na Yanga wapo nchi nzima. Ni kwa nini TBL wanawaongezea nguvu timu mbili tu ambazo tayari zina uwezo wa kujiendesha kwa sababu zina mapato makubwa? Zina wafadhili na zina sapoti ya serikali, TFF, waandishi wa habari nk. Matikeo yake ni kwamba ligi itakuwa ya Dar tu na ya timu mbili, itazidi kuboa kwa sababu bingwa atakuwa Simba ama Yanga.

    TBL wanapaswa kuiga vodacom ama Barcklays England, waelewe kwamba biashara yao sio Dar tu ni nchi nzima na ili watu wengi wahamasike na ligi ni lazima kuwe na ushindani sawa i.e fair play. Viwanja vinakosa watazamaji na hivyo biashara haitangaziki vizuri.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2011

    Yanga mnanishangaza. Hiyo jezi ya kijani ina mlima mweupe hapo mbele, kwani Yanga mna rangi nyeupe? Za kwenu ni Kijani, Njano na nyeusi. Kwa nini mkakubali kupewa lijezi lenye rangi nyeupe kifuani? Sisis washabiki wenu hatuitaki hiyo jezi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2011

    Mdau uliyezungumzia rangi nyeupe katika jezi ya Yanga, naomba nikusahihishe kidogo. Mimi ni mwanachama wa Yanga. Kuna wakati na mimi, kama unavyosema, nilidhani rangi nyeupe haipo katika Yanga; nikaja kugundua kuwa ipo, angalia nembo ya Yanga, utaona kuna njano, kijani na nyeusi, lakini pia utauona mpira wenye rangi nyeupe na nyeusi. Na hata mpira wenyewe, umezungukwa na rangi nyeupe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...