Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon , akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Asha Kipangule , mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa maonesho ya wakulima Nane Nane , wa Mwalimu Julius K Nyerere, , kabla ya uzinduzi wa maonesho ya hayo kanda ya mashariki,Agosti Mosi, mwaka huu.
Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon akiputa mpunga pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Issa Machibwa wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Nanenane,mkoani Morogoro leo.
Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu na viongozi wengine wakiangalia zana za kilimo, matrekta madogo kwenye maonesho ya wakulima nane nane, kanda ya masharikiAgosti Mosi, mwaka huu.
Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon akikabidhiwa zawadi ya kinyango na uongozi wa Taso Kanda ya Mashariki kupitia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya , baada ya uzinduzi wa maonesho ya wakulima kanda ya mashariki,Agosti Mosi, mwaka huu.
Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon(pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa uzalishaji wa vifaranga vya kuku pindi alipopita kwenye banda la JKT.
Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon ,( wapili kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Issa Machibya ( wakwanza kulia) kwenye banda la Tanapa – Mikumi, kabla ya mara baada ya kuzindua maonesho ya wakulima Kanda ya Mashariki, Agosti Mosi, mwaka huu.
Mwakilishi Msaidizi mkazi wa KOICA hapa nchini, Shin Soyeon , akitoa maelezo mbele ya Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon , ( hayupo pichani) na viongozi wengine ambao nao hawapo pichani , mara baada ya Balozi huyo kufungua Banda la KOICA katika viwanja vya maonesho ya wakulima Nane Nane , wa Mwalimu Julius K Nyerere, kanda ya mashariki,Agosti Mosi, mwaka huu.
Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Kim Young- Boon na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya , wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa kutoka nchini humo pamoja na watanzania , mbele ya baanda la KOICA , baada ya kulifungua , siku ya uzinduzi wa maonesho ya wakulima kanda ya mashariki,Agosti Mosi, mwaka huu.Picha zote na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi mbona siku hivi maonesho ya kitaifa hayafanyiki tena Morogoro???? naona ni Dodoma, Arusha na Mbeya. Kuna issue hapa? naomba kujuzwa.

    Mdau wa Moro, UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...