Wataalam wa precheck wakijiandaa kutoa mafunzo kwa walimbwende

KAMPUNI inayojihusisha na masuala ya afya ya Prechek, ilimetoa mafunzo ya afya kwa walimbwene wanaoshiriki Vodacom Miss Tanzania 2011 juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na afya .

Mafunzo hayo yalifanyika katika Jumba la Vodacom na yaliendeshwa na wataalam waliobobea kutoka kampuni ya precheck  ambao ni Dr G. Mgomella, Dr A. Komba , Dr C. Mselle na Dr D. Soka ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Precheck.

Mafunzo hayo yalihusu mambo mbalimbali kama vile Madhara yatokanayo na kula sana / kidogo (eating disorders), Afya ya kinywa na meno, Kinga ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto nk

Akizungumzia Mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Precheck Dr soka alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha walimbwende hao sit u kwa  manufaa yao wenyewe bali  pia kuwajengea uwezo ili waende kuelimisha jamii zao kule watokako kwani kwa sasa wao ni kwa sasa ni watu muhimu katika jamii.


Dr. C. Msele akitoa somo la afya ya kinywa
Dr. G . Mgomella akijibu maswali ya walimbwende
Picha ya Pamoja baada ya mafunzo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongereni sana wadau wa PreCheck... namuona Albert, Mgomella, Soka na Mselle. Timu imekaa vizuri. Kila la kheri. Mdau Tallinn.

    ReplyDelete
  2. Somo la afya,yaani vinywa , vikwapa,ukimwi,magonjwa ya zinaa nk. ni kwa mamodo(warembo) tu au ni kwa jamii nzima?

    ReplyDelete
  3. Hawa ndugu wa Precheck wanajishughulisha na prevention and control of dietary and lifestyle related non-communicable diseases; This is truly a highly needed service to our country ukizingatia taarifa za WHO zinaonyesha kwamba magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanasababisha vifo takriban 60% (takwimu zikizidi yale ya kuambukizwa), na pia inasemekana nchi zinazoendelea zinabeba zaidi ya 80% ya matatizo haya. Kwa kweli nikiwa mdau ambaye nimenufaika na services za hawa ndugu zangu i.e. nimepungua kilogramu zipatazo 18 kwa miezi miwili tu na nimeacha kutumia dawa za pressure, natoa rai kwa vijana wenzangu, kama mnahitaji kusaidiwa kupunguza uzito, kupunguza vitambi, kuongeza fitness - hawa watu watawasaidia. Ukitaka taarifa zao niarifu ili niweke nambari zao za simu mtandaoni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...