Mdau aliyejitambulisha kama Prisca akifurahia kuambulia japo lita 5 za kumfikisha nyumbani baada ya kusota kwenye foleni ya wese kwa masaa kadhaa maeneo ya Sinza jijini Dar es salaam.


EWURA imetoa Compliance Order ( amri ya kutii amri) kwa makampuni manne ambayo ni BP, Engen, Oilcom na Camel Oil, ambapo wanatakiwa watekeleze hatua zifuatazo:

      1. Mara moja wanatakiwa kuanza kutoa huduma katika maghala yao ikiwa ni pamoja na kuanza kuuza mafuta katika vituo vya rejareja ikiwemo vituo vilivyo chini ya miliki zao;
      2. Waache mara moja kitendo chochote kitakachosababisha upungufu wa makusudi wa mafuta ya petroli katika soko la Tanzania; na
      3. katika kipindi cha masaa 24 wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria dhidi yao kwa kukiuka matakwa ya Sheria ya Mafuta pamoja na Sheria ya EWURA.
      4. Kupata tamko kamili la serikali kuhusiana na kadhia hii
      5. BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Nashindwa kuelewa kama hao wamiliki wa makampuni wamevunja sheria na kusababisha usumbufu wa kutosha na kuharibu maendeleo ya kila siku ya mwananchi wa kawaida na mfanyabiashara kwa usitishiaji wa huduma ya mafuta kwa matumizi mbalimbali ya kimaendeleo... badala ya serikali na wizara husika kyaadhibu hayo makampuni moja kwa moja na sheria kuchukua mkondo kwa viongozi husika serikalini kwa usimamizi mbovu wa biashara ya mafuta pamoja na kumsaafisha waziri mhusika wa wizara ya nishati.. badala yake wanapewa muda wa kujitetea kwanini wasiadhibiwe.. kweli viongozi wetu muozo mtupu ..hawajui kazi..tutafika tu huko cmnoana ilianzia uarabuni imefika ulaya na itakuja tu east africa na nafikiri suluhisho linatapatikana !!

    ReplyDelete
  2. I was planning to return home and invest, but I've now changed my mind.
    The government is telling investors on how much the fuel prices should be???? That is pure socialism which had failed in Tanzania in the past 30-years. Cuba and Venezuela is Sinking down each decade so is TANUnzania. Business people and Investors should rise and defeate the corrupted leader. I dont care if your CCM or ChaCCdema you all guys are joke!!
    Soon,if not soon my motherland will collapse due to the lack or leadership and assasination of Entrepreneurs. People lets go back to Free market where a seller has the rights to charged any price willing to sell. Soon, They will go after Michuzi and say: Wapigapicha wa Maharusi walipwe Tsh 7000 kwa harusi"
    Where are we heading?? Financial collapse is on the way, get prepared
    If you can't pay for the fuel, Walk or run to work.
    People if you can't afford fuel move to farms and become a farmer.
    You can't operate your generator, install solar panels.
    What is wrong with you people. What I we proud about Tanzania.
    We cant even manupulate our own Natural resorces????Mererani, Mwanadui, Bacliff, Nyarugusi, Songosongo, Kilimanjaro or even Serengeti. Why do we even vote at the first place??? Investors hate Tanzania now, BAD POLICY BAD PEOPLE BAD LEADERS BAD THINKERS AND THE LIST GOES ON, is this the end of the world???? If you dont get my point your one of them!!

    ReplyDelete
  3. Dick DesterdlyAugust 10, 2011

    Uncle,Kuna udhaifu nauona mahali.Inashangaza Serikali ina hisa silimia 50% katika BP Tanzania,Sielewi kwanini BP nao wako kwenye mgomo.Wadau tusaidiane katika hili

    ReplyDelete
  4. karibuni sana TZ wajameni nchi ya 'maziwa na asali' kila kitu bwerereeee! No problems at all!hahahaaaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  5. Haya makampuni ya kigeni, yana-test kama serikali ina meno; kitendo walichokifanya hakikubaliki Tanzania na hata mahali popote ulimwenguni. Wamekuwa wanapata super profit toka kwa Watanzania lakini hawawathamini wananchi; je kuna mtu aliwalazimisha kuleta hii huduma? Waliiomba serikali na kuhaidi kufuata masharti yote!

    ReplyDelete
  6. Mmmm!!!!! no coment!!!!

    ReplyDelete
  7. "Kuna simba na vifaru na sokwe wenye mikia"
    "Kuna mito na mabonde na Mbega walio huru"
    "TUIPENDE TANZANIA NCHI TULIYOZALIWAAAAAA."

    David V

    ReplyDelete
  8. KUNA ZILE AJALI ZA TANK KUANGUKA NA WATU KUIBA MAFUTA, NA MADHALA YAKE KILA MMOJA WETU ANAYAFAHAMU. NDICHO NINACHOKIONA KINATAKA KUTOKEA. JE HAKUNA ANAYELIONA HILI?, POLISE MPO WAPI KWENYE HII MISULULU NA WENGINE MNAOHUSIKA?.

    ReplyDelete
  9. NO COMMENT!

    ReplyDelete
  10. Tatizo watu hamuelewei Free Market inavyofanya kazi. Price ceiling haiwezi kufanikiwa. Let the market control the price. Demand & Supply ndio inayofanya price iwe juu au chini. Serikali is wrong on this one.

    ReplyDelete
  11. kaka uliyetaka kuinvest ukashindwa, huelewi unachokiongea njoo Tanzania uone hali halisi ndio uongee. Serikali ina wajibu wa kurekebisha bei ya bithaa yoyote pale inapoona wananchi wanaumia na wanafanya kwa vitu vinavyoathiri zaidi uchumi kama mafuta, umeme. use your common sense mpiga picha hawezi kuathiri nchi kwa hiyo serikali haiwezi kuingilia vitu kama hivyo. kama huna capital hiyo ya kurekebisha bei isiwe kisingizio cha wewe kutokuja kuinvest

    ReplyDelete
  12. Kuna mdau anasema alitaka aje ku-invest Tanzania lakini kasitisha zoezi lake. Kwa Taarifa yako hata kama hutakuja kuwekeza Tz sisi tunaweza kusonga mbele. Umeongelea wafanyabiashara wajipangie bei ya kuuza bidhaa zao..mimi naona wewe ndo mnyonyaji namba 1. Mafuta yanagusa moja kwa moja wananchi, chakula, madini, misitu, maji, umeme, usafiri, n.k. huwezi kuanza tu kujipangia bei unayotaka wewe, lazima uelewe hivyo ndg mdau. Hata huku Uingereza na kwingineko, vitu vinavyogusa wananchi prices zake are controlled by the Gvt. Ukitaka nenda Tanzania kawekeze kwenye mitumba, maduka ya simu, unaweza kuuza bei unayotaka wewe. Ila wewe tuachie usocialism wetu, nenda ka-invest nchi nyingine. Tanzania just needs strong Leadership, but there are best thinkers ever, and very smart people out there, wewe acha kutukana Watanzania, violence does not help Tanzanians, but love and peace among Tanzanians are the greatest treasure ever. If our Leaders decide to change now, you will see how Tanzania will become a haven. We have a HOPE, we will eventually come to that state. Therefore stop insulting our country Mr/Ms whatever you call yourself. Hata usiporudi wapo watakaorudi, na ndio watakaoleta mabadiliko, wewe endelea kuwa mtumwa huko uliko! Tanzania itajengwa na watu wenye MOYO SAFI.

    ReplyDelete
  13. Tanzania mungu baba utusaidie,maana tumeshateseka hapa duniani vya kutosha,baba wa mbinguni kama nchi yetu kuna lawama ninakuomba utusamehe tuwe huru kama matafa mengine.Tumechokaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  14. Nyie mtalalamikaaaaa lakini hakuna kitachofanywa.

    ReplyDelete
  15. Wewe mdau unayetaka kuinvest hapa Tz hauko serious, kwani tunajua hayo mainvestment yenu huko ulaya hayana uhuru kama wa kwetu hapa.

    Ndiyo maana huko kwenu bado munakuwa masikini fulani hivi, lakini hapa kwetu kiinvestment kidogo tu basi unakwepa kodi na ujanja ujanja unakuwa milionea pedeshee - raha iliyoje! Unajulikana Dar nzima na unaendesha hammer au yale magari makubwa makubwa kuonyesha utajiri wako, sasa kero ya nini?

    Tuwachie tutambe bwana wewe baki huko huko. Wese tutaweza kuli manage hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...