Ankal hii ni kwa madereva na wamiliki wa mabasi ya mikoani.
Wenzetu hapa Sauzi, hakuna kuchimba dawa, njiani kwenye vichaka kama baadhi ya mabasi yetu hapo bongo wanavyofanya. Hapa mabasi yanasimama kwenye vituo vya mafuta – maarufu kama ‘gereji’ na wananchi wanapata kuchimba dawa na kujipatia mahitaji mengine kama vinywaji na msosi.

Sasa najiuliza bongo si itakuwa kasheshe maana ilitangazwa mabasi hayaruhusu kuingia vituo vya mafuta yakiwa na abiria ! Ni utaratibu nahisi wamejiwekea hata wamiliki wa ‘gereji’ wamehakikisha wana maduka ya chakula – twaweza kuita supamaketi ndogo, na pia wana vyoo vingi. Hii ni kwa safari zote za mikoani na miji mikubwa kama Pretoria, Joberg, Cape Town, Durban. Pichani ni moja ya mabasi yanayotoa huduma za usafiri wa mikoani hapa Sauzi.

Mdau John.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wanunue mabasi yenye vyoo kama ughaibuni! Wasauzi usilinganishe na bongo, mabasi yanamilikiwa na makampuni makubwa amabyo yanaweza kuwekeza kwa vituo vya mafuta na vituo vya kupumzikia. TZ mabasi yanamilikiwa na wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wana vibasi viwili vitatu pengine kila siku viko gereji kutengenezwa, hivyo hawawezi kujenga vituo vya kupumzikia mabasi yao na abiria. Hapo sasa inabidi serikali ingie na kujenga sehemu za kupumzikia wasafiri maana abiria wanalipa kodi kwenye tiketi, mabasi nao wanalipa kodi, sasa hii kodi inaenda wapi?

    ReplyDelete
  2. Hoja yako mdau mpiga picha ni ya kawaida sana, hivi wewe umeondoka lini Bongo? Ndio ninyi mkiulizwa kuhusu nchi yenu mnakuwa hamjui hata jiografia ya nchi yako, yaani huwezi hata kujua nchi yako ina ukubwa wa kilometa za mraba ngapi. Kwa taarifa yako hii nchi ina ukubwa wa zaidi ya km za mraba 940,000 na ina watu mil. 40 tu hadi sasa na asilimia karibu 80 wanaishi vijijini. Back to ur point; Siku hizi kuna mabasi ambayo yana vituo maalum mfano Dar express, Sai baba, Scandinavia, n.k. watumiaji wa mabasi haya watasema, lakini kuna utaratibu maalum wa kusimama kwenye vitu maalum na kupata chakula au kuchimba dawa, ndg mdau Bongo siku hizi si km zamani, mambo ya zamani yanapita taratibu. Wale wanaoenda Dodoma, Singida na Mwanza wanajua huwa wanasimama vituo gani. Na wale wanaoenda mikoa ya kusini wanajua wanasimama maeneo gani, ila sio kila mara porini km mdau unavyodai. Nakubali kuwa hatujajitosheleza, ila tunaelekea huko, cha msingi ni kuimarisha tulivyonavyo, kuboresha na kupanua zaidi. Kuhusu kuzuiwa magari kusimama kwenye gas station, nadhani wabongo bado wako careless kidogo, mtu anaweza kujisahau akawasha sigara huku akiwa kituo cha mafuta..hiyo hutokea sana, kwa hiyo serikali sio kwamba haioni mambo mengine km hayo. Bongo elimu inahitajika zaidi, na tukiamua kuwa serious tunaweza. Lakini mwisho nikuombe urudi home kidogo ili upate picha kamili ya Bongo ili upate cha kushuhudia huko pia. Hata ukiulizwa kuhusu nchi yako uwe unajua kidogo mkuu. Msipende kusifia vya wenzenu huku vyenu mnaviponda. Mbona siwasikii Wakenya wakiponda kiivyo kenya yao licha ya matatizo yao kibao, hata Bongo nafuu..sikatai kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Afr Kusini na Bongo, mimi naamini tukiwa serious tutaviboresha tulivyonavyo na kuwapita hata waliotangulia!

    ReplyDelete
  3. mdau hapo siyo masuala ya uchimbaji dawa !!!hilo ni sehemu ya kuhifazi miziko ya abiriya mdau wa africa kusini wengi wao wanaishi maisha ya ajabu hata vyoo hawana kwenye nyumba zao wanaishi kwenye skwata vibanda viliojengwa na mabati mabovu na mbao na mabox

    ReplyDelete
  4. Tuliua KAMATA; zamani ilikuwa na Maeneo ya kupumzika Mazuri tu enzi hizo

    Lakini Ulafi wetu na ukame matumboni mwetu tulihakikisha tunaliibia mpaka

    Kufa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...