Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Kabwe Zitto (Chadema) akichangia kuhusu sula la matatizo ya mafuta yanayoendelea nchini hivi sasa,kwenye kikao cha Bunge leo ambapo ametaka serikali iwachukulie hatua wafanyabiashara watakaokuwa wakaidi kutii amri ya serikali kuhusu uuzaji wa nishati ya mafuta.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini,January Makamba akitoa hoja yake binafsi ya dharura kuhusu tatizo la mafuta ya petroli nchini na ameitaka serikali kutoa tamko rasmi jinsi ya kumaliza tatizo hili ambapo wananchi wengi nchini wanapata taabu kuhusu usafiri katika maeneo mbalimbali.
Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa akichangia hoja ya dharura ya suala la mafuta Bungeni leo.
Mbunge wa Same Mashariki,Anne Kilango Malecela akichangia leo Bungeni kuhusu tatizo la suala la mafuta,kutokana na hoja ya dharura aliyoitoa Bungeni leo Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba kuhusu tatizo la mafuta nchini.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) pamoja na Naibu wake Ali Malima (kulia) wakiteta ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Cyril Chami (kushoto) akiteta na Naibu Waziri wake Lazro Nyalandu kabla ya kusoma Bajeti ya Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 leo Bungeni Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakiunga mkono hoja ya dharura alioyoitoa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba kuhusu tatizi la mafuta nchini.Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hayo ndio matatizo ya nchi ya wadanganyika mkiambiwa kuwa nchi yetu haina huduma kwa jamii mnashindwa kufahamu

    tatizo kama hilo lisingelikuwepo kama serikali ingelikuwa na huduma kama hizo kwa jamii

    serikali inategemea watu wake kutoa huduma kwa jamii

    serikali haina maduka
    serikali haina usafiri kwa uma
    serikali haina majumba kwa uma
    serikali haina mahospital ya kutosha kwa uma

    huduma ya usafiri wa uma kwajili ya kuwafikisha wana jamii kufika kazini matokeo yake hao raia wenye kutoa huduma ya usafiri siku wakigoma basi ujuwe serikali imelala maana watu hawatofika kazini kwa muda unaotakiwa

    hao wafanya biashara wakigoma kuuza mafuta basi serikali itapata shida sana maana usafiri utakosekana kwa jamii

    hao wamili wa mahospital ya kujitegemea wakigoma basi wagonjwa wataongezeka na vifo vitakuwa vingi zaidi kwa kutegemea hospitali finyu za serikali

    hao wafanya biashara wenye maduka ya vyakula n.k wakigoma basi wananchi watateseka sana kwa kukosa huduma za vyakula na madawa

    bado mtazidi kujifagilia eti nchi ina maendeleo maendeleo hayo ni yepi?
    maendeleo ya kujengwa majumba wakati parking za magari hakuna?

    maendeleo ya kujenge majumba wakati umeme na maji ni mzozo?

    ni wakati wa serikali kuamka na kufikiria upya suala la huduma kwa jamii tusipoangalia tutakuwa tunajenga nyumba kwa matofali ya barafu

    hao matajiri wanaofanya mgomo wala wasionekane kuwa wana makosa maana serikali yenyewe ndio inayoshindwa kujisimamia kwa kutoa huduma kwa jamii.


    mdau mwenye upeo wa mbali ughaibuni.

    ReplyDelete
  2. Hivi wewe Kijana January unajifahamu lakini kwamba una akili ziada?? Unastahili pongezi kwa kuliona hilo haraka ingawa najua wewe ukihitaji mafuta 'yatapatikana'.Hii tatizo sasa ni dharura.Serikali hao wanaogoma hiyo jehuri wanaitoa wapi jamani..Lazima humo serikalini kuna bahadhi ya viongozi wana 'mkono'..Nyerere alishawahi kumweka ndani mgiriki moja aliyedai eti Serikali ya Tanganyika?/TZ ilikuwa mfukoni mwake!!

    David V

    ReplyDelete
  3. ANKAL itabidi uchukue ile baiskeli yako uliyoiweka NDANI ili uweze kutuhabarisha la sivyo blog itafungwa kwa gari yako kukosa mafuta

    MDAU KIFANYA-NJOMBE

    ReplyDelete
  4. umeongea vizuri sana mdau hapo juu :)

    ReplyDelete
  5. wewe mdau wa wapo juu wa tue aug 09.06;30;oopm umeongea vizuri sana napenda maoni yako yana akili sana kama ulivyosema mwenye upeo wa mbali hujakosea kabisa kweli una upeo ubarikiwe sana

    ReplyDelete
  6. Advocate JashaAugust 09, 2011

    Ankal rekebisha maelezo katika picha ya waziri wa viwanda na naibu wake wakiteta jambo bora isomeke wakiuchapa usingizi wakati wa kikao cha bunge kikiendelea.

    ReplyDelete
  7. Jamani watanzania, si kila suala la kukurupuka na siasi, hii ni biashara kama ilivyo biashara nyingine na kama wabunge wana uchungu sana na wananchi nawashauri watafute njia nyingine badala ya kutumia ubabe. Hakuna ubabe kwenye investment ya mtu mwingine. Consequences ni kubwa sana. Tufikiri zaidi katika hili.

    ReplyDelete
  8. Asante sana anony wa kwanza Augosti 09.06:30:30pm
    Umemwaga pointi.

    ReplyDelete
  9. mnayo zungumza wadau ni ya ukweli, sijui nchi hii nilini itapiga hatua mbele na kumaliza umimi.mnayo zungumza wadau ni ya ukweli, sijui nchi hii nilini itapiga hatua mbele na kumaliza umimi.

    ReplyDelete
  10. Hao viongozi wa Tz wanapiga domo wasikike ktk media hakuna lingine. Matatizo yamekuwepo Bongo miaka mingi na kila siku wabunge na mawaziri wanabwabwaja utumbo wao.NO serious actions. Cha ajabu bado kuna wajinga wajinga utawasikia wanasema mbunge fulani kafanya hiki na kile,Rais fulani kaleta hiki na kile hawaangalii kipi kimebadilika significantly ktk maisha ya mtanzania wa chini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...