Mh,Balozi Mwanaidi Maajar akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na Bloggers wa DMV akiwaelezea kuhusu matayarisho ya Miaka 50 ya Uhuru na mkutano wa DICOTA na kuwaomba BLOGGERS wote Marekani wasaidie kusambaza habari za sherhe hizi za Uhuru na mkutano wa DICOTA zitakazofanyika Sep 22-25,2011 Marriott Hotel iliyopo DULLES AIRPORT pia maeomba Watanzania wote Marekani wajiandikishe kwa wingi na anaomba kama inawezekana uchukue likizo mapema kusudi uwepo Washington,DC kuanzia alhamisi ya Sep 22,2011,kwani Miaka 50 ya Uhuru si kitu kidogo
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akichangia katika mkutano huo wa Bloggers wa DMV
Kulia ni Blogger Mubelwa Bandio(www.changamotoyetu.blogspot.com) akiwa makini kumsikiliza Mh.Balozi Mwanaidi Maajar na shoto ni afisa Ubalozi,Suleiman Saleh.
Blogger Sunday Shomari(www.sundayshomari.com)akifurahia majibu mazuri kutoka kwa Mh.Balozi Mwanaidi Maajar(hayupo pichani) baada ya kumuuliza swali.
Mh.Balozi Mwanaidi Maajar(wa pili kutoka shoto) akiongea na Blogger DMV,wa pili toka kulia ni afisa Ubalozi Suleiman Saleh,shoto ni Sunday Shomari na kulia ni Mubelwa Bandio
huyu Mheshimiwa balozi ananifurahisha sana. Yeye yuko open, na anapenda kukutana na wanahabari kuonyesha mfano kwa wenzke wanaojiona kuwa wamegeuka Miungu. Big up Mama Maajar
ReplyDeleteBalozi Mhe. Maajar na Afisa wake Suleiman Saleh ni watu ambao wamekuwa mfano wa Balozi nyinginezo kwa kuwa ni watendaji wenye ufanisi wa hali ya juu na uwazi uliotakasika. Nina hakika watanzania watafurahi na sherehe hizi kwa sababu habari zinasambazwa kwa wakati na kusema kweli tunajisikia raha sana kwamba tuna Balozi anaejaliwananhi wake. Hata keo za pasi zimepungua kwa kiasi kikubwa. Zitakuwa sherehe bomba inaonyesha.
ReplyDeleteMdau Houston, Texas.
Mimi nilisoma marekani na wakati nikiwa huko balozi....... alikuwa kama Mungu mtu. Ubalozini ukienda kujitambulisha wanakuyeyusha, hakuna mtu ana mpango na wewe. Hata taarifa za namna ya kupiga kura hatukupata. Nilituma e mail nyingi ubalozini hazikujibiwa!!! Ubalozi haukuwa unajua watu wake walioko huko na haukuwa na interest kujihusishwa nao. Huu mwamko wa balozi kuwa karibu na watu wao nauunga mkono sana
ReplyDelete