Baadhi ya Watuhumiwa wa kudurufu kazi feki za Wasanii wa Muziki hapa nchini wakiwa chini ya ulinzi Kwenye kituo kikuu cha Polisi mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Godlisten, katikati ni Ernest na Kushoto ni Steven wote wafanyabiashara mjini Dodoma.
Baadhi ya mitambo ya kudurufu kazi feki za wasanii wa muziki hapa nchini kama zilivyonaswa na camera yetu zikiwa nchini ya ulinzi kwenye Kituo kikuu cha Polisi Mjini Dodoma hiyo ni kutokana na jitihada za zinazofanywa na kampuni ya Msama Auction Mart,kupitia Mkurugenzi wake Alex Msama.
Pamoja na kwamba hizi ni jitihada za kizalendo za uchungu wa jasho la sanaa na kazi zetu, still huwezi kuangusha mbuyu kwa kuanza kuupruni majani, tena yale mateke kabisa kule juu. Tafuta a big ass electric n motorised saw ukate shina kabisa halafu chimba kisiki ukatengeneze fanicha!
ReplyDeleteStill, good job Msama, but I think your dog is barking at the wrong tree! Angalia hizo mashine zao, hao vijana wanajitafutia unga wa ugali tu kulisha familia zao. Ndomana wengi tunaamini hapa ni jitihada za sirikali tu ndo zaweza kutoa suluhiso, ikitaka!
Hii itapungua tu lakini haiwezi kwisha, wekeni vizuizi kwenye cd zenu Password mtu akitaka kucopy inamuomba code.
ReplyDeleteWEE ALEX UNAKAMATA VI MACHINGA NENDA KARIAKOO KAWAKAMATE WAKINA MAMUU NA WADOSI WENGINE....AU KUNA KITU UNAPATA?
ReplyDeleteI concur with Vonostus, hilo ndio suluhisho tu. Unfortunately, for that to happen, the government has to be fully involved from A to Z. Mfano mzuri, kuna game za PS2, PS3 nk na CD zake hazichezeki huku Afrika, kuna website hazifunguki huku Afrika, kuna movies hazichezeki kwa player za ukanda huu... hii ni mifano hai ya mapambano dhidi ya piracy. Ila swali kwa Msama alijibu, mpaka uvuke kilomita zote hizo uje aende Dodoma kwa vijana hao maskini, huku Dar, haswa hapa Kariakoo amekosa kabisa sehemu ya kuanzia? Hata kama hizo ni publicity stunts tu. Tuacheni unyanyasaji wa watu wadogo jamani, tuone aibu walau kiduchu. Anza kwa vigogo wa hiyo piracy ambao I am 110% sure wanajulikana huko mjini Daslam...
ReplyDelete