Foleni ya wese kituo cha GAPCO mtaa wa Samora na Pamba jijini Dar jana jioni. Japo kwa foleni lakini waliuza wese
Ankal,
Wananchi wengi wamepumbazwa na kampuni ya BP kujiunga katika mgomo wa kutotoa mafuta wakati nusu ya hisa ni za Serikali. Walipoulizwa kwa  nini hawauzi mafuta walisema tenki zao hazina mafuta. Hii haiwaingii akilini wananchi wengi kwani BP Tanzania ina hifadhi zake za mafuta kule Kurasini. Tunaomba utufikishie ujumbe wetu kwa wahusika kamba vigogo wote wa BP Tanzania waliopo wapigwe chini maana ni wahujumu uchumi. Pia serikali iondoe hisa zake na kuzipa kampuni ya TPDC iliyopewa kibali kuuza mafuta, na vituo vyote vya BP Tanzania wakabidhiwe hao TPDC maana hawana adabu hawa watu kabisa....
-Wadau Kariakoo


Kuhusu BP Tanzania
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Sheli ya Gapco? Hapana ni kituo cha mafuta cha Gapco Hii ni kama kusema Honda aina ya Suzuki. Tuelimishane jamani.

    ReplyDelete
  2. Hii ni kielelezo tosha kwamba kampuni ya mafuta ya SHELL ilifanya kazi kubwa sana miaka ya enzi ya mwalimu kiasi kwamba watz wengi wamejisahau na kudhani neno shell ni kituo cha mafuta kumbe ni kampuni ya mafuta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...