Mamlaka ya udhibiti katika sekta ya nishati na maji (EWURA) imeagiza kampuni kubwa nne za kuuza mafuta ambazo zimedaiwa kuwa vinara wa mgomo wa kuuza mafuta nchini, kuanza kuuza bidhaa hiyo mara moja ambapo pia imetoa onyo kali kwa kampuni zinazoendelea na mgomo huo.

Kampuni zilizotakiwa kurejesha huduma ni BP, Engen, Camel pamoja na Oil Com. Kampuni hizo pia zimetakiwa kujieleza ndani ya saa 24 kwa nini zisichukuliwe hatua za kisheria kwa kuvuruga ugavi wa nishati ya mafuta nchini.

 Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Bw Haruna Masebu, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wa EWURA, agizo hilo ni sawa na agizo la Mahakama Kuu ya Tanzania.

“Agizo hilo pia linawataka kutojihusisha na matendo yeyote ambayo yatavuruga mwenendo wa ugavi wa mafuta katika soko,” Bw Masebu alisema katika mkutano huo na waandishi wa habari.

Maagizo hayo ya EWURA yanafuatia mkutano wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili hali ya mgomo wa mafuta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Haya ndiyo matatizo ya kuua TIPER ili wajanja wachache wawe wanatuletea mafuta kwa vidumu. Serikali irudishe TIPER mara moja ili tuagize mafuta kwa wingi na kurefine wenyewe, kisha hayo makampuni yawe yananunua huko kwa ajili ya usambazaji. Kwa hali ilivyo sasa, sidhani kama serikali ina uwezo wa kuwabana wafanya biashara, labda iwe hiyo serikali ndiyo inayowauzia mafuta!

    ReplyDelete
  2. hii yote ni kiburi ya pesa hapa lazima mmoja azidiwe nguvu na watanzania tunasubiri nini kuandamana kama umeme,maji na sasa mafuta shida?

    ReplyDelete
  3. SHELI ZA BP?

    ReplyDelete
  4. Unakumbuka Plan B wakati kumekucha?

    Nafikiri kwa sauti, kwa nini COPEC haikuwepo siku zote baada ya kuruhusu biashara huria? Ni nchi holela pekee ndio inaruhusu kwa asilimia 100 wafanyabishara kuendesha shughuli za nishati....

    Anyway lets take a lesson... na operation ya COPEC iwe ya kisasa na haraka na inabidi wawe na 51% kwenye kila Oil Tanker linaloingia hapa...

    ReplyDelete
  5. Nyie vipi? Tunapunguzaje bei wakati mpango wetu wa kurudisha mapesa yetu haujakaa sawa????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...