| Waziri wa Nchi,Fedha,Uchumi,Mipango na Maendeleo Omar Yussuf Mzee |
Na Fatma Kassim,Maelezo Zanzibar .
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa inachukuwa kila jitihada za lazima kuona kuwa Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) iliopo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar inafanya kazi mapema iwezekanavyo.
Waziri wa Nchi,Fedha,Uchumi,Mipango na Maendeleo wa Zanzibar,Omar Yussuf Mzee amesema kuwa Wizara yake itafanya jitihada kubwa hivi sasa kutafuta Fedha ili ujenzi huo uanze haraka sana ili kufanikisha utowaji wa huduma za Chumba cha Wagonjwa hao.
Amesema kuwa licha ya Serikali ya China kuahidi kujenga Chumba hicho hivi sasa,Wizara itatowa fedha kuanza kufanya matengenezo haraka kwani hali ya Chumba hicho sio yakuridhisha kutokana na vifaa muhimu kutofanya kazi.
Mheshimiwa Omar ameyasema hayo hivi leo katika kikao maalum baina ya uongozi wa Wizara yake na Wizara ya Afya kilichofanyika katika Wodi hiyo ya Wagonjwa Mahtuti katika hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Alisema kuwa kila kitengo muhimu katika hospitali hiyo ikiwamo sehemu ya Upasuaji,Wodi ya akinamama watahakikisha kuwa Chumba cha Wagonjwa Mahtuti kinakuwepo.Nae Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji amesema kuwa jumla ya Shilingi Billioni moja zinahaitajika katika ujenzi wa Wodi hiyo hadi kumalizika kwake..
Amesema kuwa Wagonjwa waliopo katika Wodi ya Wagonjwa Mahtuti hisi sasa wanawatafutia sehemu maalum ya kuwaweka ili ukarabati huo uanaze mara moja na wodi hiyo iweze kufanya kazi zake kama inavyotakiwa.
Katika Bajeti ya Wizara ya Afya iliopitishwa hivi karibuni Waziri wa Nchi Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf Mzee alimuahidi Muwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Zanzibar Hamza Hassan kuwa Wizara yake itafanya kikao maalum mara tu bajeti itakapomalizika ili kuondoa tatizo la Chumba cha Wagonjwa Mahtuti (ICU) kiliopo hospitali ya Mnazi Mmoja ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakifanyio kazi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...