Waziri wa Nishati na Madini,Mh. William Mganga Ngeleja
Mheshimiwa Spika,
  1. Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kulishukuru Bunge lako tukufu kwa kunipa fursa hii ya kutoa taarifa kuhusu hali ya biashara ya mafuta ya petroli hapa nchini.
  1. Kama tunavyofahamu, mafuta ya petroli ni muhimu sana  kwa uchumi wa nchi yetu kwani viwanda, vyombo vya usafiri, na huduma nyinginezo nyingi hutegemea mafuta na bidhaa zake. Bei ya mafuta inapopanda, bei zingine nyingi hupanda kwa mfano bei za usafiri zinapanda, bei za vyakula zinapanda, bei za bidhaa za viwandani zinapanda; nakadhalika.
  1. Mheshimiwa Spika, tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, alitoa maagizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta. Hatua ambazo ziliagizwa kuchukuliwa ni pamoja na:
  1. Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);
  1. Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
  2. kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
  3. kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financiang Charges); na
  4. Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

    Michuzi Blog

    Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

    Toa Maoni Yako:

    Kuna Maoni 3 mpaka sasa

    1. Tunarudi kule kule tulikotoka. Serikali ina hela. Kwa nini isitumie hela ilizonazo kuchangia kiasi kilichokosekana katika mlipuko huo wa bei ili kupunguzia hasara wafanya biashara? Tuko kwenye soko huria, hakuna anayetaka hasara? Kama serikali haitaki kuingia hasara kwa kusaidia, ni vipi wafanyabiashara watakavyokubali kula hasara na kufiriskia? Ni vigumu kwa serikali kufirisika,lakini ni rahisi kwa wafanyabiashara wa wese kufirisika! Nadhani tusiwaonee. Serikali inahitaji kubail out sekta hii, pesa inazo ndio maana hata mafisadi wanazifisadi!

      ReplyDelete
    2. Hakuna hasara wanayoipata ila faida imepungua kidogo ukilinganisha na jinsi walivyokuwa wanawanyonya wateja. Mahesabu yalipigwa sio kwamba serikali imekurupuka tu. Wanachofanya hao wenye mafuta ni kuweka ngumu ili faiada yao isisshuke.

      ReplyDelete
    3. kwanini tuliuwa TPDC leo mafuta yanatutokea puani.

      ReplyDelete

    Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...