![]() |
Waziri wa Nishati na Madini,Mh. William Mganga Ngeleja |
- Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kulishukuru Bunge lako tukufu kwa kunipa fursa hii ya kutoa taarifa kuhusu hali ya biashara ya mafuta ya petroli hapa nchini.
- Kama tunavyofahamu, mafuta ya petroli ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu kwani viwanda, vyombo vya usafiri, na huduma nyinginezo nyingi hutegemea mafuta na bidhaa zake. Bei ya mafuta inapopanda, bei zingine nyingi hupanda kwa mfano bei za usafiri zinapanda, bei za vyakula zinapanda, bei za bidhaa za viwandani zinapanda; nakadhalika.
- Mheshimiwa Spika, tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, alitoa maagizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta. Hatua ambazo ziliagizwa kuchukuliwa ni pamoja na:
- Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);
- Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
- kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
- kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financiang Charges); na
- Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
Tunarudi kule kule tulikotoka. Serikali ina hela. Kwa nini isitumie hela ilizonazo kuchangia kiasi kilichokosekana katika mlipuko huo wa bei ili kupunguzia hasara wafanya biashara? Tuko kwenye soko huria, hakuna anayetaka hasara? Kama serikali haitaki kuingia hasara kwa kusaidia, ni vipi wafanyabiashara watakavyokubali kula hasara na kufiriskia? Ni vigumu kwa serikali kufirisika,lakini ni rahisi kwa wafanyabiashara wa wese kufirisika! Nadhani tusiwaonee. Serikali inahitaji kubail out sekta hii, pesa inazo ndio maana hata mafisadi wanazifisadi!
ReplyDeleteHakuna hasara wanayoipata ila faida imepungua kidogo ukilinganisha na jinsi walivyokuwa wanawanyonya wateja. Mahesabu yalipigwa sio kwamba serikali imekurupuka tu. Wanachofanya hao wenye mafuta ni kuweka ngumu ili faiada yao isisshuke.
ReplyDeletekwanini tuliuwa TPDC leo mafuta yanatutokea puani.
ReplyDelete