Hello Uncle Michuzi
Kila nikiiangalia jiji la Nairobi huwa nabaki mmmh,angalia flyover hizo yaninina hakika baada ya miaka michache jirani zetu watapiga hatua mia moja Salama salama,mfungo vipi unapanda? za maendeleo.
Home
Unlabelled
watani wa jadi oye!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
they have flyovers but are not happy compared to us. i'd rather be happy. tanzania oyeee, oyeeee.
ReplyDeleteWa Tz tunajua kuchonga tu wenzetu wanaongea kwa vitendo. Mh Kazi ipo. Sijuhi kwa nini nimkuwa mtanzania lol
ReplyDeleteWewe unayesema uko happy, uko happy na kitu gani hata ukiwa na gari mafuta huna? una nyumba huna umeme ndani wala maji? Una biashara mjini huna umeme wa ku-run computer? Biashara zote kubwa sasa hivi zinaanza kumilikiwa na Makaburu na wazungu wa ulaya na US...na waarabu na wahindi? sasa wewe furaha yako ni nini? Mtanzania akili fupi sometimes, akiwa na kajumba, gari na wanawake (nyumba ndogo) anaona kafikaaa....na kasimu ka mkononi, na ka laptop basi anajiona basi tena....acheni kuwa na akili fupi.
ReplyDeleteMimi nikon happy na kila kitu cha bongo, umeme, maji, foleni za magari, kipindupindu. Kwetu hapa na sina tamaa ya kutumwa na mzungu.
ReplyDeleteMDAU UNAYESEMA KUWA HUNA HAJA YA KUTUMWA NA WAZUNGU ELEWA KUWA KUNA WAZUNGU WANAOTUMWA NA WAZUNGU WENZAO AMBAO SEHEMU YA KODI WANAZOLIPA NDIZO ZINAZOSAIDIA NCHI MASIKINI KAMA TANZANIA. UNAPOKULA UKASHIBA KODI ZA WANAOTUMWA NA WAZUNGU, USILEWE NA KUANZA KUTUKANA WATU. KAMA HUWEZI KUWASHUKURU WALIOKUNUNULIA CHAKULA UKALA UKALEWA KUTOKANA NA KODI ZAO, BASI MSHUKURU MUNGU. KAMA ULILELEWA KATIKA MAADILI MEMA, UKABAHATIKA KUPITA SHULE NA UKAWAELEWA WAALIMU, BASI NI VEMA UTUMIE NAFASI HII KUOMBA RADHI WATU, WAKIWEMO WAZUNGU, WANAOTUMWA NA WAZUNGU.
ReplyDeleteMdau hapo juu unapenda kutumwa na wazungu ila umekosa visa,mbona wakija mnawababaikia? umebadili passport na majina mara kibao lakini bado upo minazi mirefu,mbona unatumwa na wahindi na waarabu?yupi bora mzungu au gobacholi?
ReplyDeleteBongo tajiri na masikini wote wanataabika tu,hata ukiwa na pesa unaweza kuwa maskini siku ya pili.
Ni wachache sana wanaofanya kazi kihalali kwa kujituma na wakapata mahitaji yao yote,wengi mnachakachua kiaina,maana mishahara na maisha havilingani kabisa.
Kama viongozi na wafanyakazi wote wa serikali na sekta binafsi wakifanya kazi kwa ufanisi wa kujenga nchi na sio ubinafsi na uvivu basi kweli hata sisi sote tungerudi kuendeleza nchi.Lakini ubinafsi ndio umetawala kila kona.Hata kazi kupata ni kujuana.
kwakweli sitaki wivu na ukweli wa mambo kenya imetushinda kwa barabara, elimu na mambo mengine. nairobi na miji mingine ya kenya karibu kila sehemu za miji kuna barabara za lami, maji na umeme. tanzania haishi kugawa sehemu za watu kujenga nyumba lakini ina chukua miaka kuweka lami,, maji na umeme. angalia sehemu kama mikocheni ambazo ni prime area lakini lami iko kwenye main roads only. mji wa arusha ambao ni wa kimataifa na unatakiwa kuwa city. maji ni shida sana na barabara za lami ni chache. i know this place called sakina in arusha which is very close to downtown na kuna majumba mazuri kweli lakini hakuna maji wala barabara. i think tanzania should borrow a leaf from kenya when it comes to infrastructure. serikali iko busy kutafuta wawekezaji na kusaini mikataba mibaya na tanzania haifaidi much.
ReplyDeleteWewe annoy wa Aug. 10, 12:01:00 AM 2011, Kwa taarifa yako utumwa unarudi tu....hamna pa kwenda..kama hautakukumba wewe watoto wako na wajukuu wako hawatauepuka kwavile una akili fupi leo hii. Wewe si umeona Rais wenu alivyofanya safari za nje kuliko rais yeyote duniani. Unadhani anapoenda huko si ni namna ya kuwakaribisha wageni. Unadhani kuna mtu atakupa cha bure? Wewe endelea kujikuna tu useme una raha na umeme, maji, foleni za magari na kipindupindu ukija kushtuka utajikuta huna kitu. Tumieni Medulla zenu. Mdau-CA, USA
ReplyDeleteNdo maana Meya wa jiji anasema watu akili zipo kwenye makalio! ni kweli kabisa manake tunafikia kinyume nyume. no maendeleo! tilalila nyingiiii.
ReplyDeleteTatizo letu tanzania ni SIASA ndizo zimetufikisha hapa tulipo! hakuna mipango MIJI kila kitu kinaratibiwa na WANA SIHASA! Tumebaki kuwa MATASA WA AKILI, nenda Ka nchi kama swazilandi ambako sie tunasema ni maskini pale Mbabane nao wamejenga fly overs ambazo wahandisi ni Watanzania ambao wanasema walikimbia si-hasa za ovyo za BONGO! Shame upon us
ReplyDeletewambie haooooo. upuuzi tu. eti im happy. inaonyesha shule ndogo, maisha ya kuunga unga kupitia ndugu.No vision, No mission. Ndo maana wanaona wako happy. Wivu pia, nani anatumwa na mzungu, kama natumwa na mzungu nalipwa kwa pounds mshahara wangu wa mwezi, ni wako wa mwaka. hapo vipi. kuwa na fikra vijana. acheni upuuzi.
ReplyDeleteAsante mtoa picha. Nilikuwa huko Juzi na kuona flyover hiyo inayojengwa. Wanazo nyingine nyingi tu ambazo zimejengwa ndani ya miaka 10. Kwa kweli inasikitisha sana kuona sisi huku habari za flyover na kupunguza foleni zinakuwa kwenye mikutano ya siasa na kampeni tu. Sijui lini tutaamka!
ReplyDeleteAsante anony wa tatu hapo juu.Umepiga nyundo kwenye kichwa cha msumali. Wa-TZ akili fupi. Anony wa kwanza angesema wa-TZ tuna woga wa fisi na tena tumezoea shida hata mimi ningemuelewa.
ReplyDeleteWewe anony wa nne. Umesema hutumwi na wazungu, sawa. Ina maana hufanyi kazi au una shughuri yako binafsi. Hongera. Makampuni makubwa yanapoingia vikampuni vidogo vinakufa. Siku moja utaajiliwa tu na hawa jamaa.
Ni vema kuwa na shuguri yako, lakini kumbuka watoto wako na watoto wa watoto wako, na watoto wa watoto wa watoto wako. Je, umewaandalia chochote? Hawa mazugu, wahindi na waarabu unaowaona hapa bongo hawana shida ya njaa, wengi wao wana pesa ya kuishi vizuri mpaka kufa hata wasipofanya kazi. Lakini wako hapa kwa ajili ya watoto wao na watoto wa watoto wao na pia hata kwa ajili ya watu wangine amboa wanafanana nao ki-rangi! Hivi ndivyo ilivyo na hawawezi kutueleza mimi na wewe tuliolala usingizi mzito. Nasikitika mawazo yako maana wawazo yetu wa-TZ na waafrika ni mimi, mke wangu na watoto, tukienda zaidi basi kabila na udini. POLE.
Hawatupi misaada ila wanarudisha mali walizochukua, hakuna cha bure hapa Duniani.
ReplyDeleteZikijengwa Bongo baada ya siku mbili mtakuta viduka na vibanda kibao pembeni.Lakini mjue zikijengwa Bongo bomoa bomoa ya kufa mtu itatokea. Mambo haya yanafanyika sababu serikali yao ina mikakati mizuri kuliko yetu, viongozi wao wanaangalia maili 5 zaidi ya viongozi wetu.
ReplyDeleteTatizo mnapenda kujidharau sana. Mimi nimekuwa Nairobi mda mrefu sikuona kitu cha ziada. Nendeni vijijini kwao ndio mtajua kwamba hakuna cha ziada. Na zaidi ya hayo uchumi wao kwa sehemu kubwa upo mikononi mwa hao mnowaita wakerewe. Tofauti na bongo amabpo uchumi upo mikononi mwa wabongo wenyewe. Kwa kweli naishukuru ccm kwa hili japo ilipaswa iwe imetufikisha mbali zaidi ya hapa.
ReplyDeleteSomeni CIA world fact book 2002 na 2005; na UNDP 2010, mtaona population ya Tz inayoishi chini ya dola moja kwa siku ni 36% ambapo hao watani ni 51%. Jivunieni kwa kile mlicho nacho ila juhudi zaidi inatakiwa.
Flyovers hata Bongo zimeshaanza kujengwa kwenye juction ya TAZARA na kama bado basi Magufuli alidanganya bunge juzi. Huyo Anony anayesema flyovers zipo kenya miaka 10 iliyopita ni muongo. South Africa ndio walikuwa na flyovers mda mrefu lakini sio Kenya. Wacha kutudanganya.
Hivi vitu Tanzania tutavisikia sana na kuviona kwa wengine. Tumebweteka na ulimbukeni. kama jamaa aliyesema mbongo akiwa na kibanda chake, tv ,gari anaona hayo ndo maisha, hata kama hajui yeye na familia yake watakula nini kesho.
ReplyDeletetetemeko la ardhi likitokea wataweza kuokoa watu toka ktk kifusi cha fly-overs na kujenga tena flyover mpya? Bora barabara za chini kutokana na kutokuwa na makandarasi wazawa wenye uwezo wa kukbiliana na majanga asilia kama tetemeko la ardhi.
ReplyDeleteMdau
Babdari Salama
Kenya, Uganda Tanzania hawaachani sana. Ni sawa, GDP ya Kenya ni kubwa kuliko ya TZ. Lakini mnajua jinsi ya kupima GDP? Akatokea mtu mmoja kuwa na pesa nyiiiiiiingi sana katika nchi halafu zikachanganywa na vijisenti vya watu wachache zikagawanywa kwa watu waote wa nchi ile, GDP inawezekana ikaonekana kubwa. Kumbe ni mtu mmoja ameipandisha. Nmuunga mkono Anony mmoja aliyesema tuache tabia ya kujidharau. Inarudisha maendeleo nyuma kwani kila siku badala ya kubuni mbinu za kujiendeleza tunaendeleza uswahili kwa kusifia wengine. Shame on us!!!
ReplyDeleteKatika hawa wengi waliotoa maoni hapa inaonyesha wanakitu kinaitwa tamaa. Huwezi kung'ang'ania kuwa na kitu ambacho huna uwezo nacho. Kujenga flyover na kujenga shule lipi bora? Kuna shule wanafunzi wanakaa chini, zahanati ya kijiji iko maili 100, hospitali ya muhimbili ina gari 3 za wagonjwa. Jana profesa mmoja wa uchumi hapa UK anasema ikiwa serikali yao italipa deni lake basi UK itakuwa sawa na nchi za dunia ya tatu. Uchumi wao haukujengwa kwa misingi ya kufanya kazi kwa bidii bali umejengwa kwa mikopo na kupora nchi nyengine. Kama TZ tutaweza kutumia mfumo wa mikopo basi maisha ya watu wengi wenye bidii yatageuka kuwa mazuri. Jembe la mkono linafanya wanakijiji washindwe kulima sana. Ufugaji wetu utabaki kuwa wa kizamani maana watu hawana uwezo wa kununua chakula cha mifugo. Huko USA kuna majimbo sawa na bongo, maana hawapewi mikopo. Lazima uongozi wa nchi sasa TZ wakae chini kutafakari jinsi ya kutatua matatizo yetu. Kuita wawekezaji kila sehemu sio jibu pekee maana wengine wamekuja kutengeneza pesa za upesi upesi waondoke warudi kwao. Viongozi ndio wenye majukumu haya sasa TZ.
ReplyDeleteAnonymous 02:24pm,ni wapi USA kuna majimbo kama Bongo?we lazima una insanity en u need ur brain get worked,hakuna sehenu hata mmoja hapa yenye makazi ya watu ambayo haifikiwi na barabara ya lami, maji, umeme, gas, magari ya fire, ambulance,u need take back yo comment, USA is a 1st world en how in world wud u compare with the poorest country in world?
ReplyDelete