Watu 10 wamefariki papo hapo baada ya basi la Grazia lililokua likitoka Njombe kwenda Dar es Salaam kupinduka  eneo la Mwidu jana jioni, karibu na Ubena Zomozi, kilometa chache kufika Chalinze, kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Afande Mbaga.
 Baadhi ya maiti wakiwekwa garini
Wananchi wakishuhudia
Basi la Grazia likiwa limepinduka hapo Mwidu
Picha na Mdau George

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. mwaka huu wetu mungu tuhurumie kama kunakosa ,mungu alize horo za marehemu pema

    ReplyDelete
  2. watanzania tutakwisha kwenye hizi ajari zinazozuilika.. Doh!

    ReplyDelete
  3. Duh!.. ajali tena?? Ebwana Michu hii lini tena hii?? Laillah Illaulah!!

    ReplyDelete
  4. Naona sasa serikali iunde Wizara ya Ajali na Thamani ya binadamu ili waziri mhusika ahinde barabarani na majini anachunga magari na meli. Tanzania sasa ni kwishnei. Degelavita.

    ReplyDelete
  5. Tumechokaaaaa.. aaagh!!

    ReplyDelete
  6. mdau namba nne naona umesema kweli,,naona ikiundwa wizara ya ajali huyo waziri ata constraint katika hizo tu ajali,huwenda ikaokoa maisha yetu Tanzania!,,ajali zote ni uzembe tu,,sijui hawa asikali wa barabarani huwa wanafanya nini,,ikitokea ajali ndio wanaangaika kusimamia baada ya muda huwa wanasahau kisha wanaanza upwa,huu ni uzembe wa hali ya juu,,nchi nyingi wameweka alama au camera au maasikali kusimamia madriver wanaoendesha kwa kasi na kuona kama si walevi,,kama nchi za Ulaya na huko uarabuni,kwa hiyo kusikia ajali kama za Tanzania ni nadra sana,,,Hivi sijui kama kiongozi yeyote kwetu anajali kuongoza watu tunaokofa makundi kwa makundi kwa sababu ya uzembe wa watu wachache..mpaka afe kiongozi kwa uzembe basi mtu huyo atatangwazwa Dunia nzima na kusurubishwa!!!Hii inauma sana sana kila ukifungua kwa michuzi ni Ajali tuuuuuuu!OOOh Mwenyezi Mungu Atukinge nazo!Naona watu sasa Tuingie Misikitini Makanisani!Tufanye Ibadah maalum kwa ajili ya hizo ajali uwenda Mola akatusikia na kutupokelea maombi yetu,tukisema tusubiri uongozi ujirekebishe TUTAKWISHA NDUGU ZANGU!
    Ahlam,,,UK

    ReplyDelete
  7. Mungu na ndugu zangu mnisamehe kwa hukumu hii.jambo mojawapo linalochangia ajali za barabara ni ulevi wa waendesha magari haya,kwa kipindi kirefu sasa usindikaji wa pombe kali katika makaratasi umeathiri jamii yetu.watu wamekuwa wakifyonza hata hadharani.mbaya zaidi ni hata watoto,wanafunzi wanashiriki kileo kwa kutumia hivyo viroba,wauzaji wametengeneza groceries zisizofungwa masaa24 vituo vya mabasi abiri na madereva ni wateja wakubwa.ukizingatia sehemu zenye ubaridi vileo vikali ndio vinywaji vyao vikuu,bei zake ni rahisi huanzia tshs500/=vikihifadhiwa mfukoni vinanyonywa taratibu na kustarehe kwa dhamana ya roho za abiria.huko nyuma maji ya kunywa yalipigwa marufuku kufungwa katika viroba kwa sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira.tazama sasa hali ya mitaro na barabara jinsi vivyozagaa na kuziba.lakini kibaya kuliko yote ni jinsi watoto wanavyopata kwa urahisi bila ya jamii kujali athari ya kizazi kijacho kinachoundiwa mazingira hayo.tulaumu nani katika hili na nani anaweza kulitia macho lifanyiwe kazi inayostahili marekebisho kwani hata ndugu zetu wa uslama wawapo zamu za usiku ni washirika maalum huenda hata matukio ya uovu kutofanywa kwa wakati ni kutokana na hivyo cheap viroba vikichangamkiwa na wanavilinda vigurudumu vya wauzaji laa basi tungeona vikisitishwa kama sio kukomeshwa kabisa na kunusuru majanga tunayoyita na kuamini hali ni shwari.nawasilisha

    ReplyDelete
  8. Ajali inapotokea inatakiwa ufanyike uchunguzi kwa nini ajali hiyo ilitokea, baadae zinafanyiwa kazi zile sababu zilizosababisha hiyo ajali zisilete tena ajali nyengine. Lakini TZ hakuna kitu hicho isipokuwa kuchekana tu basi ndio maana ajali haziishi. Kuna siku BMW X5 yangu ilingongwa kwa makusudi na mwenye daladala basi wale abiria wake wote vicheko na kunishutumu kuwa mimi fisadi, wakati pesa yangu nimeipata kwa kupiga box kwa mama ukerewe!!

    ReplyDelete
  9. Mdau wa hapo juu uliyezungumzia kuhusu ulevi wa madereva, hii ndiyo sababu TBL ndiyo imekuwa mlipa kodi namba moja kushinda migodi ya dhahabu, tanzanite na hata makampuni ya simu yanayotuchuna kila siku.

    Sasa ndiyo tunaona athari ya ulevi wa kupindukia kwa Taifa.

    Kisingizio chengine kikubwa kila inapotokea ajali ya gari utasikia mpira ulipasuka. Inakuwaje wenye magari wananunua matairi yaliyotumika au feki, kwa nini kila siku visingizio hivyo hivyo?

    TBS tunaomba mushughulikie hili tatizo la matairi maana ikiwa ni kweli basi tutaendelea kuhatarisha maisha ya wananchi wasio na hatia kila siku.

    ReplyDelete
  10. Umenikumbusha, acha nikachukue kiroba changu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...