MGOMBEA ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu akitambulishwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde 'Kibajaji', baada ya kutua la helkopta katika kijiji cha Lugubu Kata ya Itumba, leo. Mkutano huo ulikuwa wa mwisho kati ya mikutano 16 aliyofanya katika kata kadhaa alikofika kwa helkopta hiyo.
Mgombea Ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Dalaly Kafumu akihutubia umati wa wananchi katika kijiji cha Igoweko, leo.Picha na Bashir Nkoromo.
NA BASHIR NKOROMO, IGUNGA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wananchi wa jimbo la Igunga mkoani Tabora kumchagua mgombea wake Dk. Dalaly Kafumu kwa utekelezaji wa mipango ya kuendeleza jimbo hilo usikwame.
Wameambiwa mgombea wa CCM litakuwa chaguo sahihi kwao kwa sababu ndiye atakayeweza kusimamia mipango ya maendeleo iliyokwisha ratibiwa, tofauti na kuchagua mbunge wa upinzani ambaye atatumia muda mwingi kulalamika badala ya kusimamia maendeleo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni za CCM iliyofanyika katika Kata za Nanga na Ziba, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alisema,ulazima wa kumchagua mgombea wa CCM unatokana na sababu nyingi za msingi.
Lusinde alisema, baadhi ya sababu hizo ni kwamba uchaguzi mdogo hautabadilisha serikali ya sasa wala ilani inayotekelezwa ambayo ni ya CCM kwa kuwa ilani na serikali inayotekelezwa kwa sasa ni ya CCM kwa kuwa ndiyo ilipewa ridhaa na wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana baada ya kuipa ushindi CCM kwa kura nyingi za urais na wabunge.
"Jamani mtu mwenye akili kama nguo yake nyeusi ikitoboka atatia kiraka cha rangi ile ile nyeusi au nyingine?, kwa vyovyote hawezi kuweka rangi tofauti na nyeusi kwa kuwa ndiyo rangi ya nguo yake, hivyo kwa kuwa mgombea aliyeondoka alikuwa wa CCM hakuna sababu ya kuweka wa upinzani", alisema Lusinde.
Akimnadi mgombea wa CCM, Dk. Kafumu, Lusinde alisema, ni mgombea mahiri ambaye akilinganishwa na wagombea wa vyama vingine kama CHADEMA na CUF hawawezi kumfikia tangu katika uwezo kielimu na hata uadilifu.
Akiomba kura kwa wananchi, Dk. Kafumu aliwaomba wananchi wa Igunga wana-CCM, wapenzi wa CCM, na wale wa vyama vya upinzani na wasio na vyama kumchagua yeye kwa kuwa anao uhakika kwa asilimia mia moja kwamba ataweza kuibadilisha Igunga kimaendeleo.
"Hapa tunachotafuta kwa kweli si ushindani wa vyama, tunatafuta maendeleo na kwa minajili ya maendeleo nichagueni mimi hata bila kujali itikadi za vyama vyenu kwa kuwa ninao uwezo mkubwa wa kusimamia na kuharakisha upatikanaji maendeleo hapa Igunga", alisema Dk. Kafumu.
Aliwataka wananchi wa Igunga hasa vijana kuachana na siasa za chuki akisema kwamba kufanya hivyo hakutaleta manufaa yoyote zaidi ya maafa baada ya uchagfuzi jambo ambalo litasababisha wana Igunga kubaki wanauguza majeraha ya magomvi wakati waliowashawishi kuvunja amani yao wakiwa wameshaondoka kurejea kwao.
"Tahafadhalini sana vijana, jitahidini kusikiliza sera na kutafuta kwa makini mgombea atakayewaletea maendeleo hapa Igunga ambaye ni mimi, msiwe na haja ya kupigana na kuumizana kwa ajili ya uchaguzi ila uchaguzi uwe sababu ya ninyi kushikamana zaidi" alisema.
Mgombea huyo alianza kampeni zake kwa helkopta tangu juzi ilipowasili na jana peke yake alitarajiwa kufanya mikutano 30 katika maeneo na kata mbalimbali jimboni hapa.
Uchaguzi mdogo jimbo la Igunga umepanagwa kufanyika Jumapili wiki hii, baada ya kampeni za muda takribani mwezi mzima ambazo zitazifikia kikomo Jumamosi wiki hii.
kwako michuzi na mwandishi wa habari inakuwaje hatupati habari za chadema kila siku huu mtandao unapambwa na picha za ccm inakuwaje sera zao tunazijua kwa miaka 50 sasa tunaomba mtupatie basi habari za vyama vingine.
ReplyDeleteJamani Igunga ni kubwa kiasi gani mpaka watumie helikopta??
ReplyDeletechadema wameshachemsha wamerudi kulala,we unataka michuzi arushe habari gani sasa? ccm ndio washindi wakifuatiwa na cuf. chadema zero (wamezungusha) sababu za kushindwa chadema ni zilezile. ubaguzi,fujo na ukabila.
ReplyDelete