Ndugu zangu Watanzania nawaomba tumsaidie mtoto Halima Kassimu (12) pichani wa Nanenane Morogoro kwani mateso anayoyapata ni makubwa sana. Halima alizaliwa akiwa ni mlemavu wa miguu yote miwili na hakuweza kutembea (Kiwete). Wazazi wake walijaribu kumpeleka katika hospitali mbalimbali bila mafanikio. Mwisho wakiwa katika kukata tamaa wakaambiwa kuwa mtoto huyu anaweza kupona kama atapelekwa KCMC au CCBRT.
uvimbe kiunoni ambalo linamfanya asiweze kuhisi chochote kuanzia kiunoni hadi miguuni kiasi ambacho hata haja kubwa na ndogo zinatoka bila mwenyewe kujitambua. Alipofikisha miaka mitatu alitoka vidonda miguuni na havikupona mpaka alipofika miaka kumi na moja (2010) mwaka huu tena vimeanza kumtokea vidonda miguuni.
Tunaomba contact details
ReplyDeletePOLE SANA HALIMA NA MWENYEZI MUNGU ATAKUAFU INSHALLAH.SASA MICHU MBONA HUJAWEKA HATA A/C AU NUMBER ZA SIMU ILI WASAMARIA WEMA WATAKAOJITOLEA KUMSAIDIA?NA PENGINE WENGINE WATAPENDA KWENDA KUMUONA NA KUJITOLEA MSAADA WOWOTE.
ReplyDeleteNi kweli huyu mtoto anahitaji msaada.
ReplyDeleteIla mbona umeelezea shida na mateso yake tu? Tungependa kufahamu gharama ya matibabu au aina ya msaada, na sehemu ya kupeleka hiyo misaada.
Mdau
Amsterdam
hakuna simu ya kuwasiliana nao?
ReplyDeletesasa msada gani unatakikana mbona hukutueleza na wapi upelekwe bebu tufafanuwa tukufahamu
ReplyDeleteAbdullrasull
Zanzibar
Mmmmh wanaume Mungu awasamehe kumuachia mama mzigo na kukimbilia nyumba ndogo ni dhambi kubwa na huyu mtoto mzuri hivyo ukaondoka na huko uliko ukipata mwenye matatizo zaidi utaondoka tena? Ok pole mdogo wangu, naamini Mungu wa mbinguni anakila sababu ya kukuumba hivyo na anawezo wa kukufanyia njia iwe kwa madaktari(hospitalini) au kwa kuombewa na kusaidiwa kama hivi. Nimesikia uchungu sana wa huyu bb kumwacha mke anayekusaidia kulea mtoto mwenye matatizo hadi kufikia umri huu. Sijui kwa kuwa mi ni pacha kama yeye? Anyway hili tangazo ni bubu maana yake hatujaambiwa tumsaidieje, hasa kama atakuja moshi wengine tungeweza kumsaidia hata vitu vidogo, vidogo kama nguo, chakula hela za matumizi. Please michuzi usikae kimya toa taarifa zote
ReplyDelete