Katika Mkutano wangu wa mwisho na Waandishi wa Habari, wakati nikitoa taarifa ya Mkutano wa Baraza la Usalama na Amani la AU kuhusu Libya, nilizungumza yafuatayo kuhusu msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu Baraza la Waasi lililojulikana kama NTC:
- Tanzania kusikitishwa na hatua ya NATO na UN kutoishirikisha AU katika mgogoro wa Libya;
- Msimamo wa Tanzania wa kuunga mkono Mpango wa Amani (Road Map) wa AU kama njia pekee ya amani ya kutatua tatizo la Libya. Road Map ilisisitiza kuanzishwa kwa mazungumzo ya amani, kuundwa kwa Serikali yenye kushirikisha pande zote na kuitishwa kwa Uchaguzi mkuu wa kidemokrasia;
- Tanzania ilikemea kitendo cha ukiukwaji wa miiko na Sheria za Kimataifa kama zinavyosimamiwa na Mkataba wa Vienna wa 1961 kuhusu ubadilishaji wa alama za taifa na uteuzi wa Mabalozi kinachofanywa na NTC. Nilielezea hatua ya Serikali ya Tanzania kupinga kupeperushwa kwa bendera ya waasi na kubadilishwa kwa Balozi bila kufuata taratibu.
- Hivyo, nilimalizia kwa kusema kuwa Tanzania ilikuwa ikitambua kuwa kuna vita nchini Libya na hakuna dalili za wazi wakati huo zilizoonyesha nani ametwaa madaraka. Nilisema bayana kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa utawala wa Kiongozi Ghadafi ulikuwa unafikia ukingoni. Aidha, Tanzania ilikuwa haijawatambua Waasi kwa kuwa hatuwafahamu wao na azma yao, hawautambui Mpango wa Amani wa AU, na pia hawakuwa wakitambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa ikiwemo mabadiliko ya alama za nchi yao.
Katika kipindi cha karibuni hadi kumetokea mabadiliko kadhaa nchini Libya na katika duru za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa. Kumekuwa na maendeleo yafuatayo ya msingi:
- NTC kwa kusaidiwa na NATO wamepata ushindi kwenye eneo kubwa la Libya ikiwemo mji wa Tripoli;
- NTC imemwandikia Mwenyekiti wa AU na kumhakikishia kuwa NTC iko tayari kutekeleza Mpango wa Amani wa AU na kuendelea kuwa mwanachama wa AU na kushiriki katika shughuli za AU. Kufuatia ahadi hiyo, Mwenyekiti wa AU kwa kushauriana na High Level Panel on Libya na Baraza la Amani na Usalama la AU (PSC) akatangaza AU kuitambua NTC;
- NTC imefanikiwa kutambuliwa na Umoja wa Mataifa baada ya kushinda kwa kura 114 dhidi ya 17 zilizopinga na 15 ambazo hazikuunga mkono wala kupinga (Abstention). Nchi zilizopinga ikiwemo Tanzania ni nchi za SADC ambazo zilisisitiza juu ya umuhimu wa kujipa muda kusubiri kwanza NTC kutekeleza ahadi zake kabla ya kutambuliwa na UN. Nchi zilizounga mkono, ziliongozwa na mantiki kuwa NTC itambuliwe kwa kigezo cha ahadi (Promissory Note) waliyotoa ya kuunda Serikali shirikishi na kuanzisha mchakato kuelekea kwenye Uchaguzi wa kidemokrasia. Hivyo, NTC imetambuliwa kwa msingi wa wengi wape (absolute majority) na sio muafaka (consensus) au kwa kauli moja (unanimity/acclamation).
- NTC imefanya mawasiliano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujitambulisha, kuainisha mipango na mikakati yake na kuombwa kutambuliwa rasmi na Tanzania. Rais wa NTC alikutana na Mhe. Rais Jakaya Kikwete wakati wa Mkutano wa UN mjini New York na kufanya mazungumzo ya awali ikiwemo kuainisha azma ya NTC kuunda Serikali Shirikishi ndani ya muda mfupisambamba na matarajio ya Tanzania na AU.
- Tanzania kama mwanachama wa AU na UN inawajibika kwa maamuzi na maazimio ya vyombo hivyo. Hata hivyo, Tanzania kama mwanachama inayo fursa ya kuweka ‘reservation’ katika Utekelezaji wa maamuzi hayo hadi hapo itakapokuwa tayari kutekeleza. Tanzania inatambua mabadiliko katika hali halisi nchini Libya ikiwemo mabadiliko katika duru za AU, UN na jitihada za NTC kufikia matarajio ya AU, UN na wananchi wa Libya. Hatua iliyopigwa hadi sasa ni kuwa Tanzania ina mazungumzo na NTC. Tunafuatilia kwa karibu maendeleo ya hali ya amani nchini Libya na tutakapojiridhisha na hatua za NTC tutaitambua. Tumefanya hivyo dhidi ya Mauritania na tutafanya hivyo tukiona haja ya kufanya hivyo.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
29 Septemba, 2011
YA,NIMEFURAHISHWA NA MSIMAMO WA TANZANIA KATIKA HILI SUALA LA LIBYA,NI KWELI UTARATIBU MZIBA ULIOHUSIKA KATIKA KUIKUBALI NHC SIO WA KIDIPLOMASIA KABISA,NI JUST TU KWA SABABU WANAPATA SUPPORT YA WESTERN COUNTRIES,UN NZIMA IKALAZIMIKA KUKAA KIMYA.
ReplyDeleteNA PIA HILI SUALA LA NATO NA UN KUTOISHIRIKISHA AU KATIKA SUALA ZIMA LA MAPINDUZI,HII NI DHARAU NA NI KIGEZO TOSHA KUWA UN SIO UMOJA WA MATAIFA,BALI NI KUNDI LINALOSUKUMWA NA WATU WACHACHE NA WENGINE KUFUATA MKUMBO.
KIONGOZI WA UTURUKI AMEANZISHA HOJA YA UN IWE REFORMED AGAIN,POSSIBLY HATA ZILE KURA ZA VETO ZIONDOKE KATIKA MAAMUZI,HII HOJA IMESHAANZA KUTIZAMWA KAMA NI NEW BEGINING OF A NEW WORLD,ANYWAY TUNAOMBA KHERI.
MDAU USA
Sitaki nataka
ReplyDeleteUpuuzi mtupu, wao si walijifanya wajuaji, wajiunge na EU na sio AU, kama hawakutaka kukubali maamuzi ya AU, hiyo ni dharau, kwanini AU wanakubaliana nao?
ReplyDelete