Na Sunday Shomari.
Bondia wa Tanzania Rodgers Mtagwa Alhamisi hii alijikuta tena akishindwa kupata nafasi ya kuitwa bingwa wa dunia baada ya refa kusimamisha pambano katika raundi ya pili dhidi ya bondia wa Mexico na bingwa wa WBC wa uzito wa unyoya Jhonny Gonzalez aliyetetea vyema mkanda wake.
Hii ni mara ya tatu mfululizo ambapo Rodgers Mtagwa anashindwa katika mapambano ya ubingwa ambayo ni nafasi nyeti sana kupata katika ndondi hapa Marekani hasa ukiwa umepoteza pambano lilikutangulia.
Kama nilivyoeleza katika andiko lililopita lazima Mtagwa atakuwa na Meneja mzuri na inabidi atumie nafasi hiyo vyema kwani amempa kila nafasi ya kuweza kuchukua mkanda wa dunia na ameshindwa mwenyewe.
Lakini pia nilieleza Mtagwa aliporwa ushindi New York Madison Square Garden dhidi ya Juan Manuel Lopez nafasi ambayo ingempatia ubingwa wa WBO na hilo liliwakasirisha wengi New York waliojaa kwenye uwanja ule.
Kwa hiyo pengine ingekuwa bora kwa meneja kuomba marudiano badala ya kupambana na bondia hatari wa Cuba Gamboa, sasa kwa wakati huu nafasi ya Mtagwa kuendelea kufikia hapa huenda ikawa mashakani lakini hatujui tutafanya juhudi ya kumpata yeye na meneja wake tusikie yapi waliyonayo.
Mtagwa alifikiri hapo bongo?
ReplyDeleteHUYU JAMAA KILA SIKU ANADUNDWA, NASIKA WAZUNGU WANAMTUKIA TU, HATA AKI ZAKE AZIJUHI , AJUHI HATA ENGLISH. WAZUNGU WATU WABAYA SANA WANAMFANYA MTAJI.NA WATU WA UBALOZI WETU WA TANZANIA MBONA AWAMSAIIDI HUYU KIJANA?
ReplyDeleteASIJE KUFA ULINGONI. MUNGU AMSAIDIE HUYU JAMAA. NDIO KUISHI MAMTONI ZAFI HILA KAKA UKIONA UMESHINDWA KUVUMILIA TOROKA KAMBI. USIJE WAKAKUFANYA KAMA MUHAMEDI ALI. MUNGU AKUSAIDIE SANA NDUNGU , MTANZANIA WENZANGU . NAJUA NI SHIDA TU NDO ZINAKUFANYA UKAPIGANE HAYO MAKONDE. NAZANI SASA UNA MIAKA ZAIDI YA 32 UKO . KI BOXING WEWE NI MZEE!PEACE BRO
MDAU PARIS
Mtagwa alizidiwa kwa kila kitu,nafikiri inabidi aongeze juhudi zaidi na zaidi!
ReplyDeletetanzania ni kichwa cha mwendawazimu thats all.
ReplyDeletemichuzi kwa nini una bana comment , zenye ukweli. jamaa kazeeka kwani ni huongo
ReplyDeletemdau china
Hamna cha juhudi zaidi ni kwamba tu hawezi kupigana. Umri pia sasa unaanza kwenda time to consider retirement kabla kichwa hakijaanza kuharibika.
ReplyDeletewamexico sio mchezo wasikie hivyo hivyo sugu kila siku wanawakandamiza wamarecan kizenji
ReplyDeleteWewe anonymous wa kwanza acha ubaguzi kusema wazungu watu wabaya sana huo ni ubaguzi. Mzungu hapa akisema waafrika wabaya mtaanza kulia lia acheni ubaguzi. Kuna wanasheria chungu mzima walio weusi kama unafikiri naonewa si kuna wanasheria hao wamsaidie? Msichafue lugha. Hii blog hata watanzania wazungu wanasoma!
ReplyDelete