Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda Mh. Winston Baldwin Spencer  kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf Astoria jijini New York Jumatatu usiku.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi tuzo hiyo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe baada ya kuipokea. Nyuma ya Mh. Membe ni Balozi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Mh Ombeni Sefue (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi Maajar
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa shukrani kwa kupewa tuzo hiyo. Marais Paul Kagame wa Rwanda, Abdoulaye Wade wa senegal na Mwai kibaki wa Kenya, pia walipokea tuzo kwa michango yao katika maendeleo ya nchi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kweli nabii hathaminiki kwao

    ReplyDelete
  2. Movie ya COMING TO AMERICA by Eddie Murphy was partly acted in that hotel.

    ReplyDelete
  3. tuwekee clip ya anachoongea au paka tukaipate kwa wakenya?picha tu tunamjuwa ni ni yeye wakila siku so what?(qweman)

    ReplyDelete
  4. KWA SEKTA YA AFYA IPI???????MALARIA? TU NA NGAO JUU. MATATIZO YA HUKU YANAWENYEWE. LOO!!!!!!!!! HII KALI

    ReplyDelete
  5. langu ni lilelile la kila siku kuhusu huyo bodigadi wa rais hivi ni lazima kuvaa magwanda? hawezi kuvaa nguo za kawaida kama suti n.k?

    maana kwa upeo wangu namuona kama anachafua hadhi za shughuli maana kila shughuli ikiwa ni sherehe ya vibopa au nyinginezo huyo bodigadi utamuona na magwanda yake

    sherehe nyingine zinahusisha viongozi wakuu wa nchi tofauti lakini huwezi kuona magwanda yameingia humo utaona tu walinzi wakawaida

    najisemea tu Ankali misupu ukipenda iweke usipopenda ifunike kama kawaida yako

    ReplyDelete
  6. HII BLOG HOVYO KABISA HUWA HAITOI MAONI YA WATU ILA WANAYOPENDA WAO. NAJUA HII MTAISOMA TU HATA KWA KIMYA KIMYA. HOVYO!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...