WATANZANIA TUISHIO JAPAN TUMESIKITISHWA SANA NA TAARIFA ZA MSIBA HUU MZITO KWA TAIFA LETU. MSIBA AMBAO UMESABABISHWA NA KUTOKEA KWA AJALI YA MELI YA MV SPICE, ILIYOTOKEA TAREHE 10/09/2011.

TUNAWASHUKURU SANA WALE WOTE WALIOONYESHA UJASIRI MKUBWA KATIKA ZOEZI LA UOKOAJI NA KUFANIKIWA KUASALIMISHA MAISHA YA WATANZANIA WENZETU KADHAA, NA PIA WALE AMBAO WAMEJITOLEA, NA WANAENDELEA KUJITOLEA KWA NAMNA MBALIMBALI ILI KUSAIDIA WALIONUSURIKA PAMOJA NA FAMILIA ZA WAFIWA.

TUNACHUKUA FURSA HII KUTOA POLE NA SALAMU ZETU ZA RAMBIRAMBI NA PIA KUWAHAKIKISHIA KUWA TUPO PAMOJA NANYI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MAOMBOLEZO.

MWENYEZI MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU WOTE MAHALI PEMA PEPONI AMEN

JUMUIYA TA WATANZANIA WAISHIO NCHINI JAPAN

NJENGA, Rashid : MWENYEKITI
SUGAI, Prosper : MAKAMU MWENYEKITI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ajari ilikuwa mbaya sana.. poleni sana ndugu za marehemu wote.

    ReplyDelete
  2. Leteni michango yenu huku nyie watu wa japan.. wateja wenu wa magari ndo waliokufa huku melini

    ReplyDelete
  3. Bima na SUMATRA wajibikeni sasa ndio tuwaone kazi yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...