SALAMU za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Spice Islander na kuua watu 202 zimezidi kumiminika nchini kutoka Jumuia ya Kimataifa.
Salamu hizo za rambirambi pia zimetumwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein.
Hadi leo, Jumatano, Septemba 14, 2011, Mheshimiwa Rais Kikwete alikuwa ametumiwa salamu za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali 22, zikiwemo zile kutoka kwa Mfalme wa Sweden Mfalme Carl Gustaf R, Gavana Mkuu wa Canada Mheshimiwa David Johnston, Waziri Mkuu wa Mauritius Mheshimiwa Dkt. Navinchandra Ramgoolam na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Salamu nyingine zimepokelewa kutoka nchi za Benin, Philippines, Ukraine, Poland, Belarus, Misri, na Khazkistan.
Aidha, salamu nyingine zimetumwa kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama Asha Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Mohammed Babu, Balozi wa Tanzania katika Ufaransa Mama Begum Karim Taj, na Balozi wa Tanzania katika nchi za Misri Mheshimiwa Ali Shauri Haji ambaye pia anaiwakilisha Tanzania katika Israel, Jordan, Libya, Lebanon, Syria na Palestine.
Mheshimiwa Rais Kikwete pia amepokea salamu za rambirambi kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania katika Oman Mheshimiwa Abdallah Abasi Kilima, Balozi wa Tanzania katika India Mhandisi John H. Kijazi, Balozi wa Tanzania katika Canada Mheshimiwa Alexander C. Masinda na Balozi wa Tanzania katika Brazil Mheshimiwa Francis Malambugi.
Salamu pia zimepolekewa kutoka kwa Katibu Mtendaji wa International Conference on the Great Lakes Region Balozi Liberata Mulamula na kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mazao (Common Fund for Commodities), Mheshimiwa Ali Mchumo.
Meli ya Spice Islander ilizama kwenye pwani ya Zanzibar katika eneo la Nungwi usiku wa kuamkia Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu, 2011 na mpaka sasa watu 202 wamethibitishwa kuwa walipoteza maisha katika ajali hiyo na wengine 619 waliokolewa katika ajali hiyo.
Hadi sasa meli hiyo iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Pemba kupitia Zanzibar haijaweza kuopolewa kutoka baharini hata kama wazamiaji wa ndani na kutoka Afrika Kusini wanaendelea na kazi ya kuitafuta meli hiyo.

Brother Michuzi.
ReplyDeleteNaomba nichukue fulsa hii kukupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya katika kuendeleza libeneke. Ni ukweli usiopingika kwamba blog yako bro Michuzi inaongoza katika kupasha habari, kuelimisha na kuonya pale inapobidi;na kwa sababu hiyo watu wengi hususani watanzania walio nje ya nchi wanaipenda na kuiheshimu blog yako. Hata hivyo, naomba nichukue nafasi hii kukukumbusha jambo ambalo ninaamini unalijua kutokana na uzoefu wa taaluma yako, UHARIRI.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikikerwa sana na habari/ matangazo yanayotolewa katika blog yako pasipo kuhaririwa. Baadhi ya matangazo hayo yamekuwa yakiandikwa kienyeji mno kiasi kwamba yanapoteza maana na kuwa kichekesho. Mimi binafsi inanisikitisha mno ninapoona waraka wa serikali,idara, au kampuni inayoheshimika inapotoa tangazo au tamko katika blog likiwa limeandikwa hovyo hovyo. Mfano halisi ni tangazo lililotolewa na hospitali ya Taifa Muhimbili kuhusu mgonjwa anaetafuta ndugu zake. Tangazo hilo lilitoa maelezo mengi yasiyo ya msingi lakini halikutaja kabisa taarifa za muhimu kama JINSIA ya mgonjwa, makisio ya UMRI wake, MAUMBILE (Mrefu, mfupi; Mnene, Mwembamba)Rangi ya ngozi, NYWELE, na MAVAZI.Nashindwa kuelewa ndugu wa mgonjwa huyo wangemtambuaje bila taarifa hizo muhimu.
Brother Michuzi, huu ni mfano mmoja tu kati ya makumi ya makosa ambayo nimekuwa nikiyaona kila siku katika blog yako. Naomba unielewe kwamba nimetumia mfano huo si kwa lengo la kuishambulia hospitali ya Muhimbili bali kwa ajili ya kuonesha udhaifu wa wahariri wa blog yako. Katika taarifa nyingine muandishi wa taarifa muhimu alitaja visiwa vya Zanzibar kuwa ni "Pemba na Zanzibar" badala ya "Unguja na Pemba" na habari yake ikachapishwa bila kuhaririwa.
Bro Michuzi naomba unielewe kwamba lengo langu ni kukupa ushauri tu ili ukipenda ufanye marekebisho ya kuboresha blog yako. Taarifa za serikali, mashirika na makampuni zinapoandikwa hovyo hovyo zinaonesha wahusika wa idara hizo ni wazembe kama sio wajinga. Tatizo ni kwamba lawama nyingi zinaelekezwa kwa wewe mwenye blog maana wasomaji wanaamini unazipitia taarifa/matangazo hayo kabla ya kupost. Tafadhari Brother Michuzi LINDA heshima yako.
Naamini wapo wasomaji wengi sana ambao wanafurahia kusoma blog yako lakini pia wanakerwa na makosa mengi yanayokuwemo.Naamini utaufanyia kazi ushauri wangu kwa manufaa ya watazamaji na manufaa yako pia.
Nakushukuru sana.
NIMESEMA.
Mwana Dikala