Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akiwa ameshika mfuko wa mbolea aina ya DAP ambao ni sehemu ya msaada kutoka Serikali ya Japan kulia ni Balozi wa Japan Bwana Hiroshi Nakagawa, Makao Makuu ya Wizara, Temeke, Jijini, Dar es Salaam.

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe leo amepokea msaada wa mbolea aina ya DAP kutoka Serikali ya Japan kiasi cha tani 5,953 chini ya utekelezaji wa msaada kutoka nchi hiyo unaofahamika kama KR 2 wa mwaka 2010/2011.

Mbolea hiyo iliyotolewa na Serikali ya Japan imegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 7.3 sawa na Yeni Milioni 400 za Japan.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mbolea hiyo hapo Wizarani, Waziri Maghembe alisema kuwa sekta ya kilimo nchini imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa mbolea.

Waziri Maghembe alisema licha ya changamoto hizo Serikali ya Tanzania imejizatiti katika kukabiliana na changamoto hizo ili Taifa liwe na uhakika wa chakula kwa kuongeza uzalishaji katika mazao ya chakula na biashara ili kupambana na umaskini wa kipato.

Akiongea wakati wa makabidhiano ya mbolea hiyo, Balozi wa Japan nchini Bwana Hiroshi Nakagawa alieleza kuwa, Serikali ya Japan kupitia mpango wa KR 2 imedhamiria kuwasaidia wakulima wa Tanzania ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula.

Waziri Maghembe aliishukuru Serikali ya Japan kwa mchango wao katika utekelezaji wa Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) na kuongeza kuwa mbolea hiyo itauzwa kwa bei nafuu ili kuiwezesha Serikali kupata fedha na kuahidi kuwa mbolea hiyo itasambazwa mapema ili iwafikie wakulima kwa wakati kupitia mpango wa Serikali wa kusambaza pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.

Waziri Maghembe alitumia fursa hiyo kumuaga Balozi huyo wa Japan Bwana Hiroshi Nakagawa ambaye atamaliza muda wake wa utumishi kama Barozi wa nchini ifikapo Septemba 30 mwaka huu. Waziri Maghemeb alimwakikishia kuwa Tanzania itatumia vyema misaada, utaalam na wataalam wake katika sekta ya kilimo na umwagiliaji ambao nchi hiyo imekuwa ikiisaidia Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kichwa cha habari "kutoka serikali ya watu wa China" kwenye picha anayekabidhi ni balozi wa Japan na habari yenyewe inelezea Japan!!!

    ReplyDelete
  2. NDUGU MWANDISHI BADILISHA KICHWA CHA HABARI BADALA YA CHINA SAHIHISHA WEKA JAPAN

    ReplyDelete
  3. Kaka Michuzi,
    Heading yako haiendani na habari yenyewe, huo msaada unatoka China au Japan?

    ReplyDelete
  4. Acheni wazimu CHINA au JAPAN?? Someni kichwa cha hii habari..

    ReplyDelete
  5. Kichwa cha habari kimenichanganya, umeandika "Serikali ya China", na chini yake mifuko ina bendera ya Japana na kuna maneno "from people of Japan" ????????????

    ReplyDelete
  6. author/owner, kindly correct your heading. If you mention mbolea is from China people will not even use it. However, its from the people of Japan, and that makes a big difference.

    ReplyDelete
  7. Ndugu wahusika,kichwa cha habari kinasema china,lakini caption ya picha,na habari zenyewe zinasema Japan,tungefurahia umakini zaidi katika upanashaji habari,ili imani yetu kwenu iongezeke.tujenge utamaduni wa kufanya vitu kwa umakini,asanteni.MWB

    ReplyDelete
  8. Swali; Serikali ya Tanzania yapokea msaada... kutoka Serikali ya Uchina au kutoka Serikali ya Ujapani? Re: "From the people of Japan".

    ReplyDelete
  9. Naona hapa Ankal hapa umechemsha,sijui kama ni wewe mwenyewe au waandishi wako,Umeandika msaada wa mbolea kutoka "China"na ukiangalia hata mifuko ina bendera ya Japani na balozi wao Nakagawa anaonekana hapo,sasa sijui ni haraka au stress haijulikani,inabii muwe mnazipitia habari kabla ya kuziposti.Hata hivyo sisi ni wapenzi wa blog hii ya jamii"Damu" hatutaiacha tuko pamoja nayo,na makosa hutokea sometimes.
    Jerome Nathaniel,Ugaibuni.

    ReplyDelete
  10. China au Japani?

    ReplyDelete
  11. mwandishi hapo kwenye kichwa naona umepata kwikwi, nadhani inatakiwa isomeke "kutoka serikali ya japani" kwani mbolea zimeandikwa "from the people ofjapan" na habari yenyewe hapo chini umeandika vizuri, japan.
    ni hayo tuu,
    Libeneke Oyee!!

    ReplyDelete
  12. Salama kaka Michuzi?

    Naomba kukosoa kidogo. Naona hapo juu umeandika msaada ni kutoka China. Taarifa hii inaweza wakwaza watu fulani hususani waliotoa msaada (yaani waJapani).

    Ni hilo tu,
    Mdau.

    ReplyDelete
  13. Please Michuzi edit kichwa cha habari msaada umetoka China au Japan!

    ReplyDelete
  14. MIchuzi, huu msaada watoka China au Japan? Mbona ina confuse hii?

    ReplyDelete
  15. Je China ipo ndani ya JAPAN ????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...