Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu akisalimiana na Viongozi wa Kampuni ya SS BAKHRESSA mara baada ya kuwasili kwa ziara fupi ya kutembelea viwanda vya kampuni hiyo na kujionea uzalishaji wa chakula unaofanywa na kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu(Kushoto) akisikiliza maelezo ya utendaji wa kampuni ya SS BAKHRESSA kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw Hussein Sufian (Kulia)

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu( Kulia) na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Eng Marwa(Kushoto), wakionja kinywaji kipya cha Azam Cola kinachozalishwa na kampuni ya SS BAKHRESSA
Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji wa Kampuni ya SS BAKHRESSA Bw Patrick Muriuki ( Mwenye Kofia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu(Mwenye suti) kuhusu aina mbali mbali za unga wa ngano zinazozalishwa na kampuni hiyo.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, ameipongeza kampuni ya SS BAHKRESA kwa uamuzi wake wa kuwekeza kwa dhati katika uzalishaji wa bidhaa za chakula za aina mbali mbali.

Mh Nyalandu ametoa pongezi hizo Jijini Dar es salaam mara baada ya ziara yake ya  kutembelea viwanda vya kampuni hiyo ili kujionea hali halisi ya uzalishaji wa bidhaa za chakula unaofanywa na kampuni hiyo.

“Ndugu zangu ninawapongeza sana kwa kazi iliyotukuka ambayo mnaifanya kwa miongo kadhaa sasa, juhudi zenu zipo dhahiri, mnagusa maisha ya Watanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Vyakula na Vinywaji mnavyozalisha sio tu vinalinda afya zetu, bali pia ni chanzo kikubwa cha ajira hasa kwa vijana, serikali itaendelea kuwaunga mkono kwa kila linalowezekana” amesema Nyalandu.

Mh Nyalandu ameiomba kampuni hiyo kuwa tayari kuwafundisha na kuwaonesha njia wajasiriamali wadogo ili nao washiriki kikamilifu katika kuzalisha bidhaa za chakula kwa ubora unaokubalika huku akisisitiza umuhimu wa vyakula hivyo kuuzwa kwa bei nafuu ambayo watu wote watamudu.

Pamoja na kushiriki katika kilimo cha mazao mbali mbali ambayo ni malighafi kwa viwanda vyake, SS Bahkressa ni wanunuzi wakubwa wa mazao mbali mbali na matunda yanayozalishwa kwa wingi kote nchini na pia ni miongoni mwa kampuni zilizoajiri idadi kubwa ya Vijana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. MBONA SIONI MAGABACHORI HAPA?KAMPUNI HII NI YA WAZAWA KWELI AU KUNA KAMCHEZO WANAKAFANYA?AU MPAKA AWE JK NDO WATATOKEA MAANA LADA MHESHIMIWA WAZIRI HATISHII UWEPO WAO HAPA NCHINI!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. ANON WA 08:28:00 PM, INASIKITISHA SANA KUWA TANZANIA BADO KUNA WATU WABAGUZI WA RANGI KAMA WEWE. HAMNA KAMCHEZO KOKOTE HAPA AZAM. 99.9% YA WAAJIRIWA NA VIONGOZI NI WAZAWA. ZAMANI AFRIKA KUSINI WALIKUWA WANA SIASA YA "APARTHEID" YA UBAGUZI WA RANGI. TZ TUKAWASAIDIA KUKOMESHA SIASA HIYO. SASA SISI TUNATAKA KURITHI SIASA HIYO YA UOZO WA KIBAGUZI!!!!!! NENDA MFUATE MTIKILIA NA UOZO WENU WA KIBAGUZI DP!!!!!!! MARTIN LUTHER KING ALISEMA "RACISM IS NOT PATRIOTIM" NA MZEE MANDELA AMESEMA "WE WILL NOT REPLACE WHITE RACISM WITH BLACK RACISM". TAFAKARI.

    ReplyDelete
  3. Mtoa maoni wa kwanza ana mawazo hatari ya kikaburu.

    ReplyDelete
  4. mdau wa hapo juu kwani Mzee bakhresa ni gabacholi? yaani hilo tu ndio umeona linafaa kuchangia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...