Na John Kitime
Kuanzia album ya kwanza ya Tancut Almasi Orchestra , bendi iliendelea kutoa vibao vilivyoweza kudumu katika kumbukumbu za wote waliovizisikia kuanzia enzi hizo, album ya kwanza ilikuwa na nyimbo kama vile, Nimemkaribisha nyoka(Kasaloo Kyanga), Kashasha(Kyanga Songa), Tutasele (Kasaloo), Mtaulage(John Kitime), Big Four(Utunzi wa wimbo huu ulileta utata kwani ulianza kwa ugomvi kwa Mamado Kanjanika kudai kuwa aliutunga yeye wakati akina Kasaloo na Kyanga wakidai wameutunga wao. Lakini hatimae akina Kasaloo waliacha ugomvi huo na Mamado hutajwa kama mtunzi wa wimbo huu. Hebu angalia mambo yalivyokuwa wakati Kashasha likipigwa. Niko hapo na miwani kubwa nikiungurumisha rhythm guitar.
Kwa hii na mengine kibao BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hii bendi ilikuwa inatisha kwa muda mfupi ilifunika bendi nyingi kubwa wakati huo nakumbuka hata mashindano yaliyoandaliwa na CHAMUDATA Tuncut walikuwa wakiongozo

    ReplyDelete
  2. Ni aibu sana kwa serikali ya tanzania na wananchi wa tanzania na viongozi wenye kampuni zinazofanya promotion katika nchi yetu kusahau vyetu nakupenda vya wangeni,naomba katika wasomaji wanaosoma na kutembelea blog ya jamii mniambihe kwa ukweli muziki wa leo wa tanzania na wazamani enzi za DDC wakina bitchuka na bushoke ,chidumule,mkanyia,mulenga,na group yote ya ddc zile nyimbo clara,nawashukuru wazazi wangu,bora pazia kuliko bendera kufata upepo,OSS enzi zaa ndekule, nyimbo kama christina moshi,somboko ama, Juwata jazz band wakati wakiwa na marehemu moshi wiliam,niko zengekala ramadhani mnenge,joseph mulenga, Dr Remmy ongala nyimbo kama mama uko wapi,karora,pesa,mariamu wangu,mwanza,narudi nyumbani,kifo,Mzee makassy,Vijana jazz watoto wa nyumbani,Bima lee,Mzee king kiki na nyimbo kama nimepigwa ngwala,katoto kaanza kutembea,salza,malokele,kiongo,mama kabibi,Mwenge jazz band,Urafiki jazz band,Uda jazz band,na majemedari sita ambao ambao katika historia ya muziki wa dansi tanzania wako special Mbaraka mwinshehe,Salum abdalaha,Ndala kasheba,Chinyama chianze na ochestra maquis wanazembwela,juma kilaza,marehemu Dr marijani na Dar internationalna bila kusahau bendi kama tabora jazz ambao nyimbo zao mbili ziliingia mpaka kwenye chat ya muziki kule zaire nyimbo Dada rosa na Asha Mpaka Marehemu Franco akauliza hiyo ni bendi ghani kutoka tanzania wanamziki kama papa wemba na zaiko langa langa wakauliza, leo nata mniambihe ni bendi ghani kutoka tanzania imeisha ingia kwenye chat kule congo au kufanya wacongo wapige mziki wa dansi kutoka Tanzania kwenye radio zao leo Tanzania utasikia nyimbo za wanamuziki kutoka nje zinapigwa kila wakati je na nyimbo za bongo Flava,Tanzania hakuna bendi wala wanamuzikia au bendi?ndugu zangu na mapromota umefika wakataki wa kukomboa mziki wa kitanzania na kuwakomboa wanamziki wetu,naomba bwana kitime tuwekehe nyimbo za historia ya muziki wetu tukumbuke tulikotoka natufikirihe namna ya ya kuweza kuwasidia wazee wetu ambao walituonyesha njia ya maisha kwa njia ya muziki na maneneo matamu ambayo mpaka leo uwezi kuyatowa au kuyabadirisaha,na bila kuwashahu wanamuziki wakitanzania ambao mziki wao mpaka leo ahutweza kuasahuliwa wakina wilson kinyonga na peter kinyonga watoto wa Tanga wakati wakiwa na simba wanyika na les wanyika, nyimbo kama sina makosa,paulina,shilingi yaua,mombasa,nafikiri nitakujibu, ni nyingi tuu, bwana kitime nashukuru kwa clip hii uliyo iweka hapa nakumbumbuka hawa mapacha pale mwanza mwaka mlipo pinga pale pamba hotel muziki ulikuwa ni mziki nakumbuka wakina kawele mutwana nasikia yuko uk,yaani acha tuu asante sana naomba mr ruge na hao wanaotayarisha haya mafiesta wakati umefika wa kuanza kuhusurport muziki wetu,tuko na wanamuziki wenye vipaji, sio huu mziki wanaosema ni wakizazi kipya na wengine hajui hatakuimba na mziki wao mwingi ni wa utamu wa muda,hayo ndio maoni yangu watakaokubaliana nashukuru na watakao kataa maoni yangu sina ugomvi na mtu waladharau ila napenda ukikataa towa maoni yako kwa kirefu na wengine walete yao pia ili tuweze kuwa na mjadala wa muziki wetu .asnteni
    mzalendo harisi
    yosef

    ReplyDelete
  3. Huyu kawele yuko wapi ahhaaa kweli huu ni muziki umenikumbusha mbali bwana Kitime sikia muziki sikia gita kweli Tanzania YA MWALIMU ILIKUWA HAINA UBAGUZI HAAAA WANAMUZIKI WAKITANZANIA NA WAKICONGO WALIKUWA NI MTU NA NDUGU YAKE AU KAKA NA MDOGO WAKE KAWELE MUTIMWANA KWENYE SOLO GITA haaaaaaa Tupe usiku wazee wa bush haaa iringa iringa

    ReplyDelete
  4. Shukran Kitime kuweka kumbukumbu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...