Home
Unlabelled
umwagiliaji wa dawa ya mbu majumbani jijini dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Huu ni uchafuzi wa mazingira ambao unatakiwa ukomeshwe kabisa. Huyu mtu kwanza hajui anachopulizia, hajui kinafanya vipi kazi, anaua wadudu hata wale ambao ni wa muhimu. Viuatilifu (SIO DAWA) anavyotumia vingi vimepitwa na wakati (obsolete). Walengwa (MBU) muda anaopulizia wala hawapo. Mazingira anayopulizia kuna shughuli nyingi za kibinadamu ambazo zinahatarisha maisha ya mkazi anapogusana na hicho kiuatilifu, (SIO DAWA) cha kuulia mbu. Municipal councils hazifuatilii suala hili kwa sababu ni biashara yao au ya mtu mjanja anayewatumia.
ReplyDeleteSasa mshikaji unalalamika nini? Kwani 22,000 ni kitu gani? Mbona wabongo mko hivyo? hapo ungeambiwa ukapate chupa na rafiki zako au ukaweke credit kwenye simu usingelalamika..waacheni wataalamu wafanye kazi zao.-Mdau, NYC-USA
ReplyDeleteHi, sasa kaka kama hawa jamaa dawa yao inafanya, meaning mbu wanaisha. fanya kutusaidia namba zao please.
ReplyDeleteAsant, mdau
mtoa hoja 1.safi sana.
ReplyDeletemtoa hoja wa pili pamoja na kuelimishwa na mtoa hoja wa kwanza bado tu huelewi, pamoja na kukaa new york usa akili bado tu haijafunguka. mtoa hoja wa pili na watatu nyie ndo mpompo tu duniani kama mataahira.
HIZO SUMU ZIMEMWAGILIWA TOKA ENZI YA UHURU MPAKA LEO 50 YRS, NUSU KARNE, JE MALARIA IMEISHA??
MALARIA NI UGONJWA WA NCHI ZENYE UONGOZI MBOVU ZIKICHANGIWA NA HALI YA HEWA YENYE UJOTO NA MAZINGIRA YANAYORUHUSU MAZALIO YA MBU.
MITARO ISIYO SILIBWA,MAKARO NA VYOO VYA MASHIMO YASIYOSILIBWA NA MAJI YALIYOTWAMA NA HALI YA HEWA YENYE UJOTO NA UONGOZI MBAYA/USIOJALI AU KUTUMIA AKILI HIVYO NDO MAZALIA MAZURI YA MBU.
SUMU HAZITOKOMEAI MBU/MALARIA BALI NI UCHAFUZI WAMAZINGIRA NA HUYOJAMAA ANAYEPULIZA POLE YAKE KWANI HAJUI HIYO SUMU ANAYOIPUMUA ITAMMALIZA KABLA HAJAIMALIZA MALARIA.
VYANDARUA HAVITOKOMEZI MALARIA BALI VINAKUSAIDIA ULALE USINGIZI MNONO BILA KUBUGUZIWA NA MBU.
JE HAPO ANAPOPULIZA NDO MAZALIA YA MBU? JE KWA JIRANI KUMEPULIZIWA?
UPOTEZAJI WA PESA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA. KWANI MBU ANAYEKUUMA ANAWEZA AKAWA AMETOKEA NYUMBA YA JIRANI KWA HIYO KUPULIZA HAPO NI KUPOTEZA MDA.
UKITAKA KUTOKOMEZA MALARIA INABIDI UTOKOMEZE MAZAKLIA YA MBU NCHI NZIMA.
-UONGOZO BORA UTAKAO SIMAMIA YAFUATAYO:-
MITARO, MAKARO, VYOO VYA MASHIMO VISILIBWE MBU WASIWEZE KUINGIA KUZALIANA.
KUSIWEPO NA MAJI YALIYOTWAMA.
INASIKITISHA SANA WAAFRIKA TUKO NYUMA KWA MAENDELEO ILA TUKO MBELE KWA
-WIZI
-UZEMBE
-NGONO
-USHIRIKINA
NA MBAYA ZAIDI MNAKARIBISHA WACHINA DOOH!INABIDI TUWAIGE WENZETU WARWANDA.
AU TUFANYE KAMA WAARABU WANAVYOFANYA. INAKUWA NA WASHAURI WAGENI JINSI YA KUENDESHA NCHI.
MFANO
PALESTINA LEO HII INAMTUMIA TONY BLAIR KUISHAURI NCHI YAO KIMIUNDO MBINU NA SASA WAKO MBALI SANA KIUCHUMI PAMOJA NA MATATIZO YAO KISIASA.
KUNA MARAIS WENGI WENYE AKILI TUNGEWATUMIA KAMA WASHAURI JINSI YA KUIENDESHA NCHI YETU KWANI SISI INAONEKANA HATUWEZI KITU.
Wabongo kweli tumechoka kufikiri, tunatafuta tu njia ya mkato. Ukiangalia watu wanaobughudhiwa na malaria ni walala hoi, ambao lishe yao ni duni, miili yao ni michovu, hao mbu hata mmoja tu akiwauma tayari malaria inaingia. Wenzetu wa matawi ya juu, hata nyumba zao walivyojenga kwa kuweka wavu madirishani na milangoni na hawafungui ovyo milango kwa sababu ya viyoyozi hakuna jinsi wataumwa na mbu. Mazingira yao wanayaweka safi, kuna gardener anafyeka majani na kuondoa mazalia ya mbu, mbu hawafiki huko. Kwa nini wananchi wasielimishwe wakayaweka mazingira yao safi bila kuruhusu mazalia ya mbu? Sumu inapokuingia mwilini, iwe kwa njia ya hewa au ngozi au kinywani inazidi kukudhoofisha, ushindwe kupambana na vimelea vya malaria. Tusikubali mazingira yetu yapuliziwe sumu
ReplyDeleteWrong timing, ukimwagilia hivyo viuatilifu sasa hivi na mvua inanyesha basi kemikali yote inaenda na maji itakayobaki ni ile iliyopigwa ndani na kwenye makaro ya maji machafu tu
ReplyDeleteZanzibar hii dawa imesaidia sana kupunguza malaria. Lakini dawa inayotumika na matumizi yake ni muhimu ili dawa ifanyekazi yake iliyokusudiwa.
ReplyDelete