Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ua kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa was Abeid Amani Karume Air Port,akitokea nchi za UAE,katika ziara za kuimarisha uhusiano wa kihistoria na nchi hizo. Picha na Othman Maulid Habari naMaelezo Zanzibar 

Rais wa zanzibar Dk Ali Mohamed shein akisalimiana na makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif hamadi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar,akitokea ziarani UAE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na watoto baada ya kumvalisha shada la Mauwa jkana akitokea safarini katika nchi za UAE
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kufukia eneo la Bahari kwa lengo la kuongeza Ardhi kwa ajili ya makaazi ili kupunguza ujenzi katika maeneo ya kilimo.
 
Hayo yameelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein wakatia akizungumza na Waandishi wa Habari hapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar mara baada ya kurejea ziara yake katika nchi za Falme za kiarabu
Amesema Sharjah imeshafanya kazi hiyo kwa ufanisi na kufanikiwa kujenga nyumba za makaazi katika maeneo ambayo yalikuwa ya bahari hapo awali.
Aidha amesema Nchi kama Uholanzi na nyigi nyenginezo zimeshafukia bahari na kujengwa miji ya kisasa kabisa bila ya tatizo lolote.
Hivyo alisema Zanzibar inayo maeneo ambayo yakifukiwa yataweza kujengwa nyumba nyingi za maendeleo kwani miaka ya nyuma kazi hiyo ilifanywa katika maeneo ya Funguni hadi Makumbusho ambalo eneo lote hilo lilikuwa Bahari.
Akizungumzia suala Uwekezaji Dk Shein alisema wakati umefika kwa Zanzibar kupata maendeleo ya haraka kwa kukaribisha wawekezaji wa uhakika katika Nyanja mbali mbali ili kuweza kuongeza pato la taifa.
Amesema kuwa katika mazungumzo yake na viongozi wa Sharjah na Ras Al khaima wameonyesh hamu ya kuendeleza maeneo hayo ili yaweze kuchangia katika uchumi wa Zanzibar.
Kuhusu suala la Maji safi na salama amesema Serikali ya Sharjah italeta wataalaam wa kuangalia vianzio vipya vya maji kwani utafiti uliofanywa umeonyesha kwamba maji katika visiwa vya Zanzibar yamepungua hivyo ipo haja ya kutafuta vianzio vipya kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
Akizungumzia juu ya mafunzo kwa vijana wa Zanzibar Dk. Shein amesema kuwa Sharjah na Ras Al khaima wamekubali kuwapokea vijana wa zanzibar katika Vyuo vyao mbalimbali ikiwemo masomo ya Udaktari.
Amewaomba Viongozi wa Chuo kikuu cha Sharjah kuja Zanzibar kutembelea Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuona nyanja gani za mafunzo ambazo wataweza kushirikiana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. watoto hao mbona wamevaa hivyoo jamaniii , ukikutwa umevaa hivi zenji watakuona hufai weye, ila kupokea rais pooaaaaaaaaaaa.
    Uzungu huuuuu mmeona hawatapendeza wakivaa juba hahahhhahahahahahah
    kazi ikooooo tena haswaaaaaaaaaaaa
    Allah tunusuru

    ReplyDelete
  2. tangu lini watoto wa kizanzibar wanavaa hivyo. Mnatutusi jamani.

    ReplyDelete
  3. HAO NI FREE MASON WESHAINGIA HADI Z'BAR.WATOTO WANAFUNDISHWA KUANZA KUONESHA KWAPA NA MABEGA YAO HADHARANI. WAKISHAKUWA WAKUBWA HAWATAONA AIBU TENA MBELE YA WATU.kWELI ALLAH ATUNUSURU NA UZUNGU HUU

    ReplyDelete
  4. Mhhh jamani, John akiwazuia watoto wa kiislamu kuvaa hijabu, waislaam watakuja juu ile mbaya, lakini mzazi yu radhi kumvisha kama hawa watoto simply because anaenda mpokea Mheshimiwa Rais. Mungu hebu turehemu kwa hili

    ReplyDelete
  5. kuiga kwing matokeo yake mnashindwa kuwastiri watoto wetu,wangevaa hijab isingependeza???

    ReplyDelete
  6. Watoto wa Zanzibar dotcom hao Msiumize vichwa jamni.

    ReplyDelete
  7. Inatia moyo kwa kila tusikiapo, lamuhimu positive impact kama tutarajiavyo. lakini hapa hatukupata ni nyanja zipi hao wawekezaji wa Sharja na Ras al khaima wamekusudia kuwekeza ili kuchangia uchumi.
    Nakama ni ufukiaji wa bahari basi nilazima tujezingati environmental impact yake kwa maeneo hayo kwamfano:( losses to ecosystems and threatening the thriving existence of fish stocks) na sio kigezo tu eti Zanzibar iliwahi kufukia bahari kutoka funguni hadi makumbusho mnazimmoja ambayo ilikua ni mto tu unaogawa stontown na n'gambo ambao haukua natija sana.

    kwa maoni yangu zanzibar bado haijawa na uhaba wa kupelekea kufukia bahari, ila alternative ways zipo kwa mfano kuweka sheria na mipango madhubuti yenye kutekelezeka ili kuondosha ujenzi katika ardhi za kilimo na kuanzisha miradi ya ujenzi itakayotekelezwa na hao wawekezaji na serikali kwa pamoja na sio kuwapa watu viwanja eti wajenge wenyewe ambayo si njia muafaka. ukiangalia viwanja vyengine vipo semu za kilimao ambazo serikali yenyewe imetoa.

    ReplyDelete
  8. Hivi haya mambo yakupokea kiongozi akirudi kutoka ziarani yataisha lini? hawa watu wote waliokuja hapo airport wametumia magari ambayo yanalipiwa na kodi za wananchi, na huko makazini walikotoka si wangebaki tu waendelee na kazi kuliko kuenda kumpokea kiongozi? Hizi siasa inabidi ziishe na viongozi wataongea na simu au video conference kama kuna lolote la kuambiana.

    ReplyDelete
  9. Ni vibaya sana kuona mavazi ni kila kitu, ni wangapi wanavaa hijabu sana ila wako na waume za wenzao chumba kimoja na halafu ukija mfungo wa ramadhani nao wanafunga? Tunao huku tena waswali sala 5 au 7 kama zipo, msitudanganye uislamu ni roho na si mavazi ndo maana nchi za kiislamu wanapigana kila kukicha wakiamini physical than spiritual. Ankal usibibabie please niachia hii tu

    ReplyDelete
  10. Wadau naombeni kuuliza,hivi ndege anayotumia Mhe .Shein ndiyo anayotumia Mhe Kikwete?au Rais Zamzibara ana ndege yake na Rais Tanzania ana ndege yake pia?naombeni kujuzwa.

    ReplyDelete
  11. hali halisi ya tanzania ni kujikwamua kutoka kwenye umaskini kupitia wawekezaji, dah watanzania hatuwezi kufikiria njia nyingine zaidi ya hiyo, anyway haiwezekani labda miaka 2000 ijayo.sasa bahari ikishafukiwa tumaini la masikini kunufakia hipo ama ndo sera za wawekezaji lazma twende kwa njia ya "win win situation"; ila kwa Tanzania mara nyingi huwa ni "win lose situation"..

    ReplyDelete
  12. Mdau wa 4:15, kosa moja halimaanishi kwamba umeruhusiwa kufanya na la pili.

    Kuvaa wavae vizuri hiyo ndiyo hatua ya mwanzo, ya pili ndiyo wajirekebishe na hayo mengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...