Habari yako Ankali Michuzi
Embu tuangalie hii taswira kidogo halafu tujiulize 
Je, ubebaji huu wa wanyama ni sahihi kweli? hata kama ni kitoweo atachinjwa lakini je hata si mateso na kutokuheshimu haki za wanyama kwa ubebaji huu??

By Mdau

  { ankal usibanie hii hata kama taswira hii ilitoka kwenye blog yako]

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. this is not right kabisaaaaa!!...moyo umeniuma sana kwa kuona hii

    ReplyDelete
  2. Kwakweli hii si sawa kabisa, yaani mbuzi maskini kashikwa sikio huku mwingine mguu mmoja, kweli? hata mtoa zawadi ya idd angeona asingefuraia. Ivi haki za wanyama tz ni zipo kweli?Kama azipo je iweje?

    ReplyDelete
  3. This is violation of animal rights kwa kweli hata mimi imenitouch. Daah hata kama anaelekea kwenye kisu lakini sio hivi jamani

    ReplyDelete
  4. Ishi maisha yako ya nje, popote ulipo na vyovyote ulivyo, kama ambavyo ungeishi endapo ungekuwa katika nyumba ya ibada. Heshimu viumbe vya Mungu na uvipende kama Yeye alivyovipenda na hata kuviumba.Mungu ametuteua sisi binadamu kuwa juu ya viumbe vingine, lakini hakusema tuvidharau, tuvitese, ama tuvidhalilishe. Ni vyake.

    Kwa mfano, ukiona nyoka anavuka barabara porini nawe unaendesha gari usimkanyage kwani huko ni kwake na wewe ni mpitaji tu. Ya nini kumpiga mbwa au paka mawe umuonapo mtaani wakati unajua ni mnyama wa kufugwa (domestic animal)?

    Siku hizi wazungu (wake kwa waume) wanafanya mapenzi na wanyama (mbwa, ng'ombe, farasi, n.k.), nabaki najiuliza tunakoelekea na namna gani wanyama wanavyodhalilishwa (japo hawajui).

    Baada ya kushurutishwa tuukubali ushoga kitakachofuatia ni kulazimishwa kuoa ama kuolewa na wanyama. Si ajabu ndege bado wanafanyiwa utafiti.

    Siamini binadamu, hasa nisiyemjua. Si ni sisi hawa hawa tunaobaka kinamama wajawazito na hata kuwasababishia vifo vyao na vya vichanga vyao tumboni?! Tunawaua wenzetu wenye ulemavu wa ngozi, tunaroga wenzetu ili tupandishwe vyeo au wafukuzwe kazi, na chungu tele! Huyu binadamu leo hii atamtunza mnyama kwa maana njema?! Tuishi maisha yetu kana kwamba tupo ndani ya nyumba za ibada.

    ReplyDelete
  5. nyie mnachekesha sana eti haki za wanyama. Naomba muangalie kwanza haki za binadamu. Mmeshaona vibaka wanavyokamatwa na kuvishwa matairi ya gari shingoni halafu moto unawashwa? Watoto wadogo wanavyofanyikishwa kazi?

    ReplyDelete
  6. hata mtume Muhahammad pbuh kasema kuwa tunapotaka kuchinja mnyama basi tumuheshimu na tuwe wapole kwa mnyama ataechinjwa.
    lakini hii imezoeleka Tanzania kwani hakuna haki za binaadamu kutakuwa na haki za wanyama?
    tizama wamachinga wanavyopigwa na kudundwa na ma mgambo au askari njiwa na hiyo ndo serikali sasa yuko wapi mtetezi wa haki za binaadamu na wanyama??????????
    Kaeni mnasherehekea uhuru sijui huo uhuru uko wapi na nakujua wewe mchuzi hutatoa hii comment lakini jua siku yako itafika tu kama utakuwa unabania bania ukweli.

    ReplyDelete
  7. it is not fair at all

    ReplyDelete
  8. Huyo binadamu tu hathaminiwi na anazalilishwa ndio huyo mnyama?!!!!

    ReplyDelete
  9. halafu huyu aliyebeba huku kavalia kinadhifu ni kiongozi kabisa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa ( labda kama kahama hivi karibuni) sasa kiongozi mkubwa kama yeye anatufundusha nini kuhusu haki za wanyama>?!

    ReplyDelete
  10. je kuchinjwa mnyama, ni haki yake? nisije acha kumchinja kumbe namnyima haki yake.

    ReplyDelete
  11. CRAP!!! Nendeni porini mkutane na SIMBA/CHUI/MBOGO etc...afu muone kama na nyie mtafanyiwa HAKI...damn!

    ReplyDelete
  12. KAMA SIKUKUU YA KUCHINJA NDIO HIVI MMMMMHH!!

    ReplyDelete
  13. mambo ya eid hayo hebu tuacheni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...