Wananchi waliofika katika ofisi za chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Ubungo kwa ajili ya kuanza maandamano ya amani ambayo yaliahirishwa kufuatia majadiliano yanayoendelea mjini Arusha baina ya jeshi la polisi na viongozi wakuu wa chama hicho, wakimueleza Mkuu wa Operesheni toka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni aliyefahamika kwa jina la Y. J. Mrefu sababu za kutaka kuandamana.
Kina Ras Makunja wakilinda doria maeneo ya Ubungo jijini Dar tayari kwa muziki
Ras Makunja na gitaa lake tayari kukwea jukwaaani
Gari la doria likihakikisha hakuna maandamano leo
Na Francis Dande
Jeshi la polisi nchini leo limeweka ulinzi mkali katika maeneo Kimara pamoja na maeneo waliyodhania kuwa wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wangekusanyika kwa lengo la kufanya maandamano ambayo yamepigwa marufuku katika taarifa iliyotolewa na Kamishina wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja.
Wakiwa kwenye Magari yenye namba PT 1412,PT 2118, PT1848 na PT1447 askari wa jeshi hilo kikosi cha kutuliza ghasia walionekana wakiwa wanaenda mbele na kurudi nyuma katika eneo hilo la kimara kona kabla ya kuelekezwa na viongozi wao kusogelea ofisi za chama hicho ambapo wanachama wake waliweka uzio wa kamba kuzuia watu kuingia katika ofisi hizo bila ya ruhusu maalumu.
Katika eneo hilo la ofisi watu waliokuwa wamekusanyika katika ofisi hizo walisikika wakiimba nyimbo za kuhamasishana kabla ya Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche kuwaambia kuwa maandamano yameahirishwa kupisha majadiliano yanayoendelea baina ya jeshi hilo na uongozi wa Chadema Taifa.
Baada ya maelezo hayo toka kwa Heche wanachadema waliokuwa katika eneo hilo walianza kutawanyika kurudi katika shughuli zao za kawaida, kabla ya askari wa jeshi hilo waliokuwa katika gari namba PT 1447 Kuwakamata vijana watatu waliokuwa wameshika bendera ya chama hicho pamoja na kitabu cha muongozo wa katiba kwa raia wa Tanzania kilichotolewa na taasisi ya Policy Forum.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova alisema kuwa kwa sasa hana taarifa zozote za kukamatwa kwa wafuasi wa CHADEMA na kutoa maelekezo kwa mwandishi wa habari hizi afike katika kituo cha polisi cha Urafiki kwa taarifa zaidi.
Shughuli zao za kawaida zipi? Hivi unaona kuna mwenye shuguli ya kawaida hapo? mmewanyima bure kazi akina Ras! Hivi hawajawahi kutumbiza sehemu hizo eee!
ReplyDeleteUhuni huu wa polisi utakoma tu siku moja.
ReplyDeleteNaona Ras makunja yupo soup soup,na gitaa jipya si mchezo, sasa hapo watu wangoje muziki...mwe mwe mwe..patakua hapatoshi
ReplyDeleteeh eh akina Ras Makunja ndani ya mtaa ? sasa muziki utachezeka tena naona magitaa yamesafishwa
ReplyDeleteMi nadhani polisi ndo wanataka fujo, kwani mkiwapa uhuru wao itakuweje? au mtajuaje kuwa ni haki yao kuandamana? Wakianza kurusha mawe itakuweje. Hakuna uhuru pamoja na kusherekea miaka 50
ReplyDeleteRas Makunja gitaa nimefika bei niuzie kaka namie nikapigie muziki mbele ya safari? tena limekupendeza sana sana kaka
ReplyDeleteras makunja naona sebene la leo hapo lingekua kali,sasa mkubwa naona umepiga pamba mpya za bongo tambarare au?
ReplyDeletembona chadema wana behave kama vile ni chama cha vibaka. hawa watu kweli hawafai kuongoza nchi. tabia zao za maandamano na fujo kila siku zita waogopesha wapiga kura. watanzania tusi wakubali watu wa aina hii. mapigano ya wao kwa wao yanayoendelea kwenye nchi nyingi huanzishwa na watu kama hawa. tafadhali chadema tumieni kura badala ya fujo kuingia ikulu. winning the elections is the way to go.
ReplyDeleteHivi Polisi wa Tanzania wana matatizo gani jamani? Haki zinazodaiwa na wananchi hata wao zinawahusu na kama zikipatikana hata wao watazifurahia....mimi nafikiri bado hatujawa na Polisi waelewa kama wenzetu wa nchi zilizoendelea kwani polisi wao wanasaidia wananchi kufikisha ujumbe wao kwa amani tofauti na hapa kwetu ambapo Polisi wanatumika kuwaumiza na kuwaua raia kwa kufuata matakwa ya wanasiasa...Mungu isaidie Tanzania. Polisi wanatumia pesa za wananchi kuwaumiza wananchi wenyewe na kwa sasa hali ya uchumi wa nchi ni mbaya na wahusika hawataki kuwajibika...mbona Waziri Mkuu wa Italia amejiuzulu? Mtu kama hawezi aachie ngazi...
ReplyDeletekwa nini maandamano yaanzie kimara? au ndi ule ule ukabila wa chama cha chadema,wanawafata kabila la viongozi wakuu...
ReplyDeletehivi me nauliza kinachowakera nini hasaaaaa simuwaache waandamane???? kama hawafanyi fujo nyie kinawakera nini??? hata mkiwazuia hatupati misaada nchi za nje wameshajua hii nchi ya TZ tunachakachuliwa ufisadi umejaaaaaaaaa wananchi hatuna haki yakuongea wanafaidika wao wenyewe viongozi sisi kila siku maisha yanapanda mara sukari hakuna mara imepanda bei tabu tupuuuuuu umaskin ndio wazidi kushamiri TANZANIA,kila kitu kimebinafsishwa bado sisi sasa inaudhi sanaaaaaaaa
ReplyDeletekweli haki ya Tanzania ni ngumu sana kuipata wanawaonea sana Chadema kwakweli watanzania haki haitafutwi kwa kubembeleza inabidi muda mwingine utumie nguvu policy wao wanapewa order japo wangetakiwa waungane na wananchi maana hao ndo wana hali mbaya hata pengine kuliko raia serikali yetu itumie akili kidogo kwani wakiwaacha waandamane itawacost nini??tena wangewaacha ingekuwa pouwa maana tungekuwa tunaongelea story tu sasa hii kuwapiga au kuwazuia ndo inawapandisha chati kwa maana nilijua serikali haioni kumbe inaona?wangewaacha wafanye wanachofanya ilimradi tu amani isivunjike hii policy wanawapiga ndo inavunja amani
ReplyDeleteTatizo kubwa la kina ras makunja ni kutosikiliza wanancho wanachokijua wao ni kila penye mkusanyiko wa watu panahitajika muziki ,na magitaa yao yapo mkao wa kushambulia
ReplyDeleteHuo ni uonevu mkubwa na unyanyasaji kwa wananchi,maana wananyimwa haki zao,Wananchi hawana uhuru wa kujieleza!Sasa hiyo nchi ni ya kikomonisti au ni ya kidemokrasia?Kuna siku watu watakujachoka watataka uhuru wao wa kupata haki ya kujieleza na damu itamwagika,kama ilivyotokea kaskazini mwa Afrika!
ReplyDelete