Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar
Mh. Mohammed Aboud Mohammed
NA IDARA YA HABARI MAELEZO - ZANZIBAR

Jumla ya Sh. Bilioni 1 na Millioni 100 zimekusanywa na Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar hadi kufikia leo ikiwa ni michango mbalimbali kutoka kwa Taasisi, Watu binafsi na Wadau mbalimbali wa nje na ndani ya Zanzibar kutokana na ajali ya Meli ya Mv. Spice Islanders.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed huko ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati alipokuwa akipokea Mchango wa Dola za Kimarekani 1,444 sawa na Sh. Milioni 2 laki Moja na Hamsini na Nne na Mia Nane kutoka kwa Watafiti mbalimbali kutoka nje.

Waziri Aboud amesema kuwa Serikali imefarijika sana kutokana na wanafunzi hao kuona umuhimu wa kutoa michango hiyo kwa waathirika wa ajali hiyo ya Meli ya Mv. Spice Islanders.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hadi sasa bado haijatumia fedha yoyote ile iliyotolewa kwa Michango hiyo ambapo fedha hizo zinatarajiwa kutolewa mara tu Tume ya Uchunguzi ya Ajali hiyo iliyoteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kutoa taarifa yake.

Akikabidhi mchango huo kwa niaba ya Watafiti hao Dk. Naiman Saleh Jidawi ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Baharini Zanzibar kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa wanafunzi hao wameguswa sana na ajali hiyo hivyo wameona na wao watoe mchango wao.

Aidha amesema kuwa Fedha hizo walizochangia zitasaidi katika malengo yaliyokusudiwa kutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kuwa watafiti hao kutoka nje walishtushwa sana na tukio la ajali ya Mv. Spice Islandes hivyo ikawalazimu kujikusanya pamoja na kuona kuwa wao hawatajisikia vizuri ikiwa hawatochangia chochote kuhusiana na ajali hiyo ambayo siyo ya Zanzibar tu bali ni ya Tanzania kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. sawa hela zimekusanywa na tumefahamishwa je Waliosababisha ajali pamoja na wamiliki na mawaziri wamejiuzulu?
    hebu tuweni na demokrasia kama greece na italy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...