Mwenyekiti wa kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini  kuchangisha fedha kupitisha Bajeti na kubainisha endapo kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi kutoa taarifa  kwa waandishi wa habari juu ya uchunguzi wa suala la fedha zilizokuwa zimechangishwa kimeingilia na kuathiri madaraka ya Bunge, Mhe. Ramo Matala Makani (Mb) akimkabidhi ripoti ya Uchunguzi huo Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Ofisini kwake Bungeni Leo. Pembeni ni Makamu Mwenyekiti was Kamati hiyo Mhe. Martha Umbulla (Mb) akiwa amebeba viambatanisho vya ripoti hiyo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akionesha ripoti ya kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini  kuchangisha fedha kupitisha Bajeti na kubainisha endapo kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi kutoa taarifa  kwa waandishi wa habari juu ya uchunguzi wa suala la fedha zilizokuwa zimechangishwa kimeingilia na kuathiri madaraka ya Bunge. Ripoti hiyo itasomwa rasmi Bungeni katika Mkutano wa Bunge ulionza leo. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Maendeleo ya Africa ni ndoto..

    Kama kiongozi hakubali kuwajibika mwenyewe anapokosea, mpaka aundiwe tume na kupoteza muda kibao kwa ajiri ya mtu 1 au 2.. basi tusikasirike Wazungu wanapotuambia sisi ni Mashoga.

    Maana wao ni Mabwana zetu kwa pesa wanazotuhonga kila siku.

    ReplyDelete
  2. Hiyo kukataa ushoga tu sisi waafrika huko ulaya wameshaunda tume kuchunguza. Ndio demokrasia, sio kuandamana na kukataa dhamana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...