Ankal mithupu pole na majukumu,naomba usiniweke kapuni, turushie hii wadau waione.

Leo naomba niwafahamishe wadau kuhusu hili bango lililopo pale nyuma ya Ikulu karibu na soko la samaki ferry, linalosomeka’ HAIRUHUSIWI KUPITA BARARA HII’. Hili bango lipo siku nyingi kidogo na yapo mawili linguine lipo ocean road pale upande wa bahari kama unatoka agakghan hospital, zamani hili bango lilikua likisomeka hivi ‘ HAIRUHUSIWI KUPITA BARABARA HII KUANZIA SAA 12 JIONI-12 ASUBUHI”  kuna watu wakaja wakafuta baadhi ya maneno na sasa linasomeka tofauti.

Tatizo linakuja kwa hawa watumiaji wa barabara na polisi, kuna askari wanajibanza kwenye hiyo barabara na kusimamisha magari wakidai barabara hairuhusiwi kutumika na baadae wanadai kitu kidogo ili wakuachie, sasa namuuliza mkurugenzi wa  manispaa ya Ilala atueleze hii barabara imefungwa au tuelewe vipi?
Asante Ankal
Mdau Mbegu
Kigamboni
-----------------------
Katika kuweka mambo sawa Globu ya Jamii ilituma ripota wake sehemu zinazohusika na kugundua kuna aina fulani ya matengenezo ya barabara karibu na lango kuu la Ikulu upande wa Mashariki. Pia kuna kila dalili kwamba hatua ya kuzuia kabisa magari ni ya muda na pindi matengenezo hayo ya barabara yakikamilika itakuwa kama zamani - yaani kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Tuhuma dhidi ya askari wanaodaiwa kujibanza na kuwapiga bao  wanaokiuka amri hiyo kwa bahati mbaya hazijapata jawabu ila zinafuatiliwa. Pia mdau jaribu kuwa muangalifu sana maana sehemu hiyo ni nyeti na hairuhusiwi kupiga picha.

Mhariri
Globu ya Jamii



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Taarifa imeeleweka vizuri sana...sasa wa kushughulikiwa ni hao Polisi wala rushwa.

    ReplyDelete
  2. Aise..Mhariri..Hairuhusiwi kupiga piga..sawa..lakini kuwepo na alama basi au tangazo linaoenyesha kutokupiga picha maeneo yale.Isije ikawa kama wale askari wa jiji wanaovizia magari yapaki na kuyafunga 'pingu" eti HAIRUHUSIWI KUPAKI HAPA wakati hakuna kibao cha kuzuia ku_"park".


    David V

    ReplyDelete
  3. Unanicheksha sana mhariri kwanini hamuweki alama ya kuonesha kuwa HAPARUHUSIWI KUPIGA PICHA! duh! Tanzania kweli ! ikulu ya wmarekani watu wanapiga picha na kudanda kwenye kuta , backingham palace watu tunaenda kupiga picha mpaka, leo kuna nini hapo mpaka usiruhusiwe kupiga picha ?!

    ReplyDelete
  4. Du, bongo bwana, kwani mtu akipita hapo kuna nini? au akipiga picha itakuwaje? Mbona watu wanatembea kwa raha zao muda wowote White house ya marekani au Red house ya Urusi na wanapiga picha kama kawa.

    ReplyDelete
  5. Nafikiri ripota wa Blogu hayuko sahii, kuna alama mpya ya barabarani iliyowekwa barabar hiyo inayoonyesha kuwa ni "no entry". Kwa hiyo naona kuna mpango wa kusimamisha upitaji moja kwa moja.

    ReplyDelete
  6. Nafikiri ripota wa Blogu hayuko sahii, kuna alama mpya ya barabarani iliyowekwa barabar hiyo inayoonyesha kuwa ni "no entry". Kwa hiyo naona kuna mpango wa kusimamisha upitaji moja kwa moja.

    ReplyDelete
  7. Watu wanapiga picha WH, uki google unaiona Ikulu kama ilivyo from the sky. Hebu tuache hii dhana ya karne ya 19. Hakuna mantiki kuzuia kupiga picha sehemu yoyote iliyo open to public eyes.

    Kuhusu hao askari kuvizia watu na kuwachukulia vihela vyao hili si jipya. Ukianzia pale NBC/New Africa corner ya kutokea Luther house, ukipinda kulia tu unakutana nao, Ukija hapo Junction ya KCB na British Council, ukiwa unatokea kitega uchumi ukipita through wamekula kichwa.

    Tatizo hapo ni alama za barabarani. Kama wanachi wataamua kukataa na kufikishwa mahakamani na kujitetea kwa kutokuwa na alama za barabarani, basi ni dhahiri victim mkuu atakuwa ni City council.

    Watu hawaendeshi magari kwa kujua hii barabara inatumiwa vipi, bali wanaangalia alama zinazowaambia hii barabara inatumiwaje.

    Huwezi kusema barabara imefungwa kwa maandishi, Alama za barabarani hazufundishi hivyo, maandishi ni kwa waenda kwa miguu. mtu anayeendesha atajua kuwa hakuna njia kama ataona mwanzo wa barabara kuna alama ya DUARA NYEKUNDU YENYE MSITARI MWEUPE KATI, AU PEMBE NNE YENYE MAANDISHI 'NO WAY'. Na maandishi hayo yawe reflective yanayoweza kuoneka umbali wa stoping distance kabla ya kuongia kwenye barabara.

    ReplyDelete
  8. Hapo ni kitega uchumi cha askari hukaa pale karibu na sok la samaki ukikosea kupita wanakutoa kitu kidogo.

    ReplyDelete
  9. Sehemu si nyeti, ni Ikulu ya raisi aliyechagulwa na wananchi, nenda Whitehouse Washington, 10 Downing Street, London, makazi ya viongozi wa nchi yanatumika pia kama vivutio vya watalii. Acheni kutisha watu na mhariri wa blog ni kazi yako kuelimisha watu na si kutisha kama jeshi la polisi linavyofanya.

    ReplyDelete
  10. Ankal..umefanya kazi nzuri...LAKINI hilo angalizo ni la kizamani sana..eti sehemu ni nyeti na hairuhusiwi kupiga picha...Siku hizi si mtu anaweza kuangalia hiyo sehemu kwenye google earth akaona ndani ambako mpiga picha anayetembea nje hawezi kuona?

    ReplyDelete
  11. KWA MAANAINGINE USIRUDIE TENA HAO WA KITU KIDOGO WANGEKUONA INGEKUA LONGOLONGO LAZIMA WANGE KUTOA PUMZI

    ReplyDelete
  12. wakati wa Nyerere haikua nyeti? ufisadi umewazidi wanaogopa wananchi

    ReplyDelete
  13. HAO POLISI INAWEZA KUWA SI POLISI SIUNAJUWA BONGO WATU WANAJIPATIA HAPOHAPO IKULU, KAMA MATEJA WALIVYOKUWA WAKIJICHOMA PALEPALE UKUTANI. ILA KWELI MANISPAA YA ILALA IWEKE MAELEZO HAPA MICHUZI TUISOME TUJUE HAKI NI ZIPI NA AMRI KAMA KWELI ZIPO NI ZIPI? SIO TUNAUMIZANA TU MJINI HAPA. MICHUZI TUNAOMBA USIBANIE COMMENT ZA KUSAIDIANA. MZ

    ReplyDelete
  14. Kama hajui kusoma tutafanyaje?

    ReplyDelete
  15. Wakati wa Nyerere hakukuwa na Alqaida wala AlShabab.

    Hivi sasa mambo moto ulinzi kwa wingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...