Leo naomba niwafahamishe wadau kuhusu hili bango lililopo pale nyuma ya Ikulu karibu na soko la samaki ferry, linalosomeka’ HAIRUHUSIWI KUPITA BARARA HII’. Hili bango lipo siku nyingi kidogo na yapo mawili linguine lipo ocean road pale upande wa bahari kama unatoka agakghan hospital, zamani hili bango lilikua likisomeka hivi ‘ HAIRUHUSIWI KUPITA BARABARA HII KUANZIA SAA 12 JIONI-12 ASUBUHI” kuna watu wakaja wakafuta baadhi ya maneno na sasa linasomeka tofauti.
Tatizo linakuja kwa hawa watumiaji wa barabara na polisi, kuna askari wanajibanza kwenye hiyo barabara na kusimamisha magari wakidai barabara hairuhusiwi kutumika na baadae wanadai kitu kidogo ili wakuachie, sasa namuuliza mkurugenzi wa manispaa ya Ilala atueleze hii barabara imefungwa au tuelewe vipi?
Asante Ankal
Mdau Mbegu
Kigamboni
-----------------------
Katika kuweka mambo sawa Globu ya Jamii ilituma ripota wake sehemu zinazohusika na kugundua kuna aina fulani ya matengenezo ya barabara karibu na lango kuu la Ikulu upande wa Mashariki. Pia kuna kila dalili kwamba hatua ya kuzuia kabisa magari ni ya muda na pindi matengenezo hayo ya barabara yakikamilika itakuwa kama zamani - yaani kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Tuhuma dhidi ya askari wanaodaiwa kujibanza na kuwapiga bao wanaokiuka amri hiyo kwa bahati mbaya hazijapata jawabu ila zinafuatiliwa. Pia mdau jaribu kuwa muangalifu sana maana sehemu hiyo ni nyeti na hairuhusiwi kupiga picha.
Mhariri
Globu ya Jamii
Taarifa imeeleweka vizuri sana...sasa wa kushughulikiwa ni hao Polisi wala rushwa.
ReplyDeleteAise..Mhariri..Hairuhusiwi kupiga piga..sawa..lakini kuwepo na alama basi au tangazo linaoenyesha kutokupiga picha maeneo yale.Isije ikawa kama wale askari wa jiji wanaovizia magari yapaki na kuyafunga 'pingu" eti HAIRUHUSIWI KUPAKI HAPA wakati hakuna kibao cha kuzuia ku_"park".
ReplyDeleteDavid V
Unanicheksha sana mhariri kwanini hamuweki alama ya kuonesha kuwa HAPARUHUSIWI KUPIGA PICHA! duh! Tanzania kweli ! ikulu ya wmarekani watu wanapiga picha na kudanda kwenye kuta , backingham palace watu tunaenda kupiga picha mpaka, leo kuna nini hapo mpaka usiruhusiwe kupiga picha ?!
ReplyDeleteDu, bongo bwana, kwani mtu akipita hapo kuna nini? au akipiga picha itakuwaje? Mbona watu wanatembea kwa raha zao muda wowote White house ya marekani au Red house ya Urusi na wanapiga picha kama kawa.
ReplyDeleteNafikiri ripota wa Blogu hayuko sahii, kuna alama mpya ya barabarani iliyowekwa barabar hiyo inayoonyesha kuwa ni "no entry". Kwa hiyo naona kuna mpango wa kusimamisha upitaji moja kwa moja.
ReplyDeleteNafikiri ripota wa Blogu hayuko sahii, kuna alama mpya ya barabarani iliyowekwa barabar hiyo inayoonyesha kuwa ni "no entry". Kwa hiyo naona kuna mpango wa kusimamisha upitaji moja kwa moja.
ReplyDeleteWatu wanapiga picha WH, uki google unaiona Ikulu kama ilivyo from the sky. Hebu tuache hii dhana ya karne ya 19. Hakuna mantiki kuzuia kupiga picha sehemu yoyote iliyo open to public eyes.
ReplyDeleteKuhusu hao askari kuvizia watu na kuwachukulia vihela vyao hili si jipya. Ukianzia pale NBC/New Africa corner ya kutokea Luther house, ukipinda kulia tu unakutana nao, Ukija hapo Junction ya KCB na British Council, ukiwa unatokea kitega uchumi ukipita through wamekula kichwa.
Tatizo hapo ni alama za barabarani. Kama wanachi wataamua kukataa na kufikishwa mahakamani na kujitetea kwa kutokuwa na alama za barabarani, basi ni dhahiri victim mkuu atakuwa ni City council.
Watu hawaendeshi magari kwa kujua hii barabara inatumiwa vipi, bali wanaangalia alama zinazowaambia hii barabara inatumiwaje.
Huwezi kusema barabara imefungwa kwa maandishi, Alama za barabarani hazufundishi hivyo, maandishi ni kwa waenda kwa miguu. mtu anayeendesha atajua kuwa hakuna njia kama ataona mwanzo wa barabara kuna alama ya DUARA NYEKUNDU YENYE MSITARI MWEUPE KATI, AU PEMBE NNE YENYE MAANDISHI 'NO WAY'. Na maandishi hayo yawe reflective yanayoweza kuoneka umbali wa stoping distance kabla ya kuongia kwenye barabara.
Hapo ni kitega uchumi cha askari hukaa pale karibu na sok la samaki ukikosea kupita wanakutoa kitu kidogo.
ReplyDeleteSehemu si nyeti, ni Ikulu ya raisi aliyechagulwa na wananchi, nenda Whitehouse Washington, 10 Downing Street, London, makazi ya viongozi wa nchi yanatumika pia kama vivutio vya watalii. Acheni kutisha watu na mhariri wa blog ni kazi yako kuelimisha watu na si kutisha kama jeshi la polisi linavyofanya.
ReplyDeleteAnkal..umefanya kazi nzuri...LAKINI hilo angalizo ni la kizamani sana..eti sehemu ni nyeti na hairuhusiwi kupiga picha...Siku hizi si mtu anaweza kuangalia hiyo sehemu kwenye google earth akaona ndani ambako mpiga picha anayetembea nje hawezi kuona?
ReplyDeleteKWA MAANAINGINE USIRUDIE TENA HAO WA KITU KIDOGO WANGEKUONA INGEKUA LONGOLONGO LAZIMA WANGE KUTOA PUMZI
ReplyDeletewakati wa Nyerere haikua nyeti? ufisadi umewazidi wanaogopa wananchi
ReplyDeleteHAO POLISI INAWEZA KUWA SI POLISI SIUNAJUWA BONGO WATU WANAJIPATIA HAPOHAPO IKULU, KAMA MATEJA WALIVYOKUWA WAKIJICHOMA PALEPALE UKUTANI. ILA KWELI MANISPAA YA ILALA IWEKE MAELEZO HAPA MICHUZI TUISOME TUJUE HAKI NI ZIPI NA AMRI KAMA KWELI ZIPO NI ZIPI? SIO TUNAUMIZANA TU MJINI HAPA. MICHUZI TUNAOMBA USIBANIE COMMENT ZA KUSAIDIANA. MZ
ReplyDeleteKama hajui kusoma tutafanyaje?
ReplyDeleteWakati wa Nyerere hakukuwa na Alqaida wala AlShabab.
ReplyDeleteHivi sasa mambo moto ulinzi kwa wingi.