Anko Michuzi salama,
Tunakupongeza sana kwa kazi yako nzuri unayoifanya na ni imani ya kwamba wewe ni mic yetu tunasema kwa sauti ya chini na wewe una ongeza sauti tafadhali sisi ni MASECRETARY WA TANZANIA.
1. KWANZA nataka kukufahamisha kitu ambacho unaweza kushangaa. leo ni miaka 50 ya uhuru, ikiwa chuo cha Uhaziri/Magogoni hawatambui ni vyeti gani wanatoa kwani ukiingia kukagua vyeti katika ofisi za serikali kwanza hadi ikulu ni kwamba kila secretary ana cheti cha aina yake ana ngazi ya aina yake, mpaka imefikia haijulikani cheti kipi ndio kinaonyesha ubora kwa maana kuna vyeti vya miezi 9 kuna vya miezi mitano kuna vya mwaka mmoja na kuna vya miaka miwili kuna vya mwaka mmoja na nusu kuna vya miezi mitatu.
Hivyo vyote ni vyeti vyetu masecretary. cha kushangaza utaona mwenye cha miezi mitatu anamshahara mkubwa zaidi wa miaka miwili, au mwenye cha miezi mitano anamzidi wa miezi kumi na tano haya ndiyo maajabu ya vyeti.
2. PILI utoaji wa mafunzo utashangaa sana kuona ndani ya miaka 50 ya uhuru wanachuo wa magogoni ni wale wale wanaosoma maana kila siku hawamalizi ukiingia januari mtaala ni mwingine ikifika mwezi juni mtaala ni mwingine hii ni hatari sana sana.
Mfano utakuta kuna masomo yale makuu matatu muhimu sana yanayototofautisha kati ya typist na secretary yaani typing, hatimkato, shorthand yanatolewa pale ni masomo magumu sana. kuna hatua tatu kwa kila somo ukifanikiwa ukapata hatua zote unakuwa secretari. unajua nini inashangaza sana ikiwa hivi mfano:- mwaka 2005 ulipewa cheti cha kukufahamisha kuwa umetunukiwa kuwa secretary wa kiwango cha juu yaani typing III, shorthand 100, hati mkato 100 na sherehe kubwa na joho ukaripia HAPA SASA unapotaka kuendelea na masomo mengine mfano DIPLOMA unajua nini hapa kinatokea cheti chako kinafutwa unaambiwa unanza upya masomo ya secretari ambayo walikupatia cheti na taarifa hii unapewa ukiwa umeshakaa pale darasani miezi minee ukizani unaendelea na yale yaliyoandikwa katika fomu ya kujiunga, MSHANGAO NI MKUBWA SANA NA AIBU NA FEDHEA.
tunaomba kwanza kabisa watambue kuwa hii sio haki kabisa kwani hakuna secretari mwenye cheti Tanzania nzima anae stahili kuitwa secretary. Hii inamadhara makubwa sana ambayo yanapelekea masecretary kunyanyasika mpaka sehemu zetu za kazi kwa kiasi kikubwa kwani taasisi ambayo tunakimbilia ili kujikomboa na kuwa na sura ya usomi ndio hii ambayo haitufahamu sisi ni kina nani BASI sasa unapokuwa na wewe hufahamu wewe ni nani pale kwenye taasisi mtu/watu wanadhani kuwa labda umepelekwa pale kuwafariji waliochanganyikiwa KULALA NAO, maana hueleweki.
3. TATU hapa katika chuo hiki kuna kutoelewana kwa uongozi wao wenyewe. walimu wanaoonekana wazee (tangu uhuru) na wale wa sasa (wasomi/masharobalo) utakuta migongano yao inaingilia wazi kwa wanafunzi na kusema tutaona kama mtafaulu, mfano vijana wanasema wamechoka kuona sura za hao wazee wanawabania wanawaletea mambo ya kizamani wao wasomi wanataka nafasi zao.
Inafikia mwalimu wa sasa anawadharau wanafunzi walio maliza kidato cha nne hata kama una div one kisa yeye alimaliza fomu six anatumia muda wa kipindi chote akijisifia elimu yake na kutueleza mikakati yao ya kupata madaraka hii sisi haituhusu wanatuchelewesha.
Pia hao walimu wa zamani wametusaidia sana tunawashukuru ila kuna wale ambao kwa sasa wameshachoka kabisa kabisa hawana nguvu, ila wamefanya kazi kubwa katika taifa kwa kufundisha hao masecretary wa taifa hili sasa miaka 50 na kuona matokea haya mazuri ya kila secretary na cheti chake. HONGERENI. TAASISI NZURI NI ILE INAYOKUTANA NA KUTOA MAAMUZI KATIKA VIKAO VYAO. HATUTAKI KUHUSISHWA NA AJIRA ZAO SISI TUNATAKA ELIMU TU.
4. NNE mabadiliko kwa binadamu ni ya lazima kabisa kabisa na tunayakubali kabisa ila mabadiliko yanamwanzo na yanendelea. huwezi kusema kwa sababu sasa mnaingia katika mfumo huu wote unahusika kwa maana ya kwamba kwa sasa hakuna cheti cha secretary hapa tanzania kinachofahamika VYOTE VIMEFUTWA NA NECTA.
yote haya yanatokana na mgomo wa wanachuo kwani haileweki
MSHANGAO MKUBWA:
1. Mkuu wa chuo anatoa mabadiliko ya mitaala bila kutoa maandishi/matanganzo kwa wanachuo wanapewa kwa sauti, chuo kina website imesinzis kwa hili, kuna nini kinaogopwa tangaza mabadiliko wanachuo wasome tena na tena waelewe.
2. Je Idara kuu ya utumishi hapo nyuma wana taarifa hizi, wanajua kila kitu kwani hao masecretary wenye vyeti kumi na mbili wanawashughulikia wao Je waziri (mwanamama)mwenzetu anajua hayo
OMBI:
Kutokana na heshima yetu tuliyonayo masecretary hata wao wanafahamu, tunaomba sana kusaidiwa haraka sana katika hili kwani hatutajikomboa kabisa kwa maana ya kwamba secretary ni uti wa mgogo wa ofisi ukiukata ofisi itapata kiharusi, je itakuaje msaada wa mama Hawa Ghasia ni wa muhumi sana.
NINA MENGI SANA LAKINI KWA LEO NAISHIA HAPA
SECRETARY MWENYE MACHUNGU NA KAZI YAKE

Ulichozungumza mtoa mada ni UKWELI MTUPU USIOPINGIKA katika hiki chuo chetu kinachoitwa Chuo cha Watumishi wa Umma. Mimi ni wale tuliovaa majoho kwa mara ya kwanza yaani graduation yetu ilikuwa ya kwanza Mei 2006 lakini jiulize ukitaka kwenda kusoma masomo kama ya Administration iwe chuo chochote kama CBE, Open University na kwingine hiko cheti chako cha Magogoni hakitambuliwi kabisa na mbaya kabisa hata katika ofisi zetu hakuna kutambuliwa pamoja na kuwa umesugua muda mwingi katika Shorthand na Hati Mkato lakini ukija ofisini unawekwa kwenye kundi la kina nani ikiwa wengine kiofisi wakitoka kwenye vyuo vyao wanapewa ngazi mbalimbali mpaka wanaitwa PROFESSIONAL sasa sisi tuwekwe wapi? NAOMBA SANA CHUO HICHO KITOE HATA MWONGOZO WA GRADE ZA MASECRETARY NA VYETI KUTAMBULIWA.
ReplyDeleteNikisikia mtu anakwenda Magogoni naanza kumuuliza unaenda fanya nini kwa sababu ya kero za pale!
Secretary Mkereketwa!
ukaripia= ulitaka kusema ukalipia(fedha) au kukaripiwa (kufokewa)?
ReplyDeletefedhea= unaamaanisha fedheha= (kuumbuka au kuumbuliwa) au fedha umekosea ukaandia fedhea?
huenda hiyo nd'o sababu inyowafanya waliosoma miezi mitatu wakalipwa fedha nyingi kuliko wewe labda kutokana na uelewa na ufahamu wako wa lugha mama(swahili). sijui kama kimombo kinapanda kwani secretary au katibu mukhtasi si lazima usome miaka kumi ukadhani mshahara wako utakuwa sawa na alosoma wiki kumi.
walimu= elimu haina umri. kwa asomae au asomeshae. kama mwalimu anajisifia kwa kutoa changamoto kafika kidato cha sita au chuo kikuu, jitahidi nawe usome elimu ya kidato hicho au zaidi. hiyo ni changamoto.
naenda kubeba box ntarudi tena baadaye.
Nimeiona.
ReplyDeleteNi vizuri umekaa chini na kutoa duku duku la mabadiliko ya kimaendeleo. Wahusika fanyieni kazi hili na mtoe feedback
(signed)
9/11/2011
MIAKA 50 YA UHURU, TUMETHUBUTU, TUMEDIRIKI NA TUNASONGA MBELE!!!.
ReplyDelete-----------------------------------
Haya ni mapungufu inabidi yashughulikiwe kwa kuwa kama ilivyoandikwa yana tu sasambua na kuonekana kutokwenda na wakati na mpangilio kamili.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa wigo wa eneo letu unapanuka kwa ujio wa SERIKALI ZA ENEO LA AFRIKA MASHARIKI, Kenya,Rwanda,Uganda, na Burundi pia nchi kama South Sudan inafikiriwa kuwa mwana chama karibuni.
Hivyo isifike wakati huo tukawa kichekesho ktk shirikisho la EAC na kutoa nafasi MASEKRETARI wetu wakarudi nyumbani kuchoma maandazi na vitumbua kutokana na ushindani wa wenzetu.
wEWE KWELI SECRETARY....DUH HUNA KAZI YA KUFANYA KUTUJAZIA NOTES HUMU NDANI?
ReplyDeleteHiyo taaluma ya usekretari ni endangered, labda ingeitwa kwa jina jengine.
ReplyDeleteMumejitahidi sana kujitetea lakini kwa kweli huko maofisini performance yenu ni subzero. Ni wachache sana wenye qualifications za kuwa secretaries kiuhakika.
Jitahidini muende na wakati kwa kujifunza computer skilss, english language (hapo ndiyo tatizo kubwa), na mengine mengi yatayopendezesha ofisi. Leo munaringa sana lakini output kidogo sana.
POLENI SANA LAKINI LEO IMEBIDI NITOE DUKUDUKU LANGU KIDOGO.
Ni kweli kabisa hili ni tatizo ambalo Secretary analipata kutokana na vyeti vya Magogoni kutokuwa na Categorise za kuonesha huyu ni Secretary daraja gani na anastahili kupanda hadi wapi na huyu ni vp utaona leo mtu anaondoka anenda kupita 40 w.p.m. anakuwa Executive Secretary na yule ambaye ana 50 w.p.m. wa miaka mingi baro anaitwa typist kwa kuwa hana mtu wa kumuombea kupanda. Kwa kweli hili ni tatizo linatakiwa kuangaliwa kwa undani zaidi ama sivyo tutayumba kila siku.
ReplyDeleteSecretary ni mtumishi katika ofisi ambaye anatakiwa kuheshimiwa na kujiheshimu sio kwa ajili ya kuandaa chai kwa bosi peke yake. Ana kazi nyingi za kufanya.
ReplyDeletekama sikosei mlizindua chama cha masecretari mwanzoni mwa mwaka huu Arusha. hii ndio kazi yao.
ReplyDeletewewe anonymous wa tarehe 9/11 saa 02:38 hovyo kabisa, yaani laiti ungejua hata wewe katika kazi zako ni hovyo, na unakosea sana, ungetoa kwanza boriti kwenye jicho lako ndio utoe kwa mwenzako. je unauhakika wewe huna kasoro katika kazi zako? mimi ni secretary mara nyingi boss ananipa kazi nichape akiwa amekosea sana kiingereza na mimi humsahisha sana, na ninaandika kiingereza kizuri. wewe mwenyewe hapo kizungu chako hovyo kabisa. TAFAKARI NA UCHUKUE HATUA.
ReplyDeletehapa sasa tunakaribia kufika kwani tumeanza hata kama tutatukanwa na wachangiaji wakiwa ndio wahusika. tatizo lipo tena lipo haswa kwani hivi vyeti ni tatizo kubwa na utayarishaji wa masomo ndio haswa. Kwa kweli bila chuo hiki kukaa na kuwaza kutuwekea misingi iliyo thabiti hatutafika, tunaonewa kuanzia chuo mpaka ofisibi. Ila tangu uhuru sijaona ujumbe kama huu kutoka kwa masecretary nazani sasa tunakaribiwa kufika mungu ibariki taaluma hii na wateja wake mungu wabariki wasimamizi wao, Mungu mfungue macho Mama Hawa Ghasia aweze kusima ukurasa huu wa michuzi atuone sisi wanawake wenzake. Mungu teketeza ujinga wa hao walimu wasiojua nini wanafanya
ReplyDeleteNina uchungu sana
jamani jamani nimekubali kuwa hata asiye kuwa na macho ipo siku atapapasa, nimeshangaa sana kuona masecretary wameyaona haya. kwanza kuna mchangia hapo juu kanifurahisha sana amesema ni kweli tumesasambua huyu mchangiaji anaonyesha ni mdau tena wa cheo kikubwa sana katika hili tunakuomba baada ya kuchangia endelea, hapo magogoni ni sehemu ya kutukomboa sisi msitupe elimu kama vyuo vya mtu asiyefahamu. unaweza kuendesha ofisi bila kada hata nne but siyo kumkosa secretary haitawezekana tusaidiesni sana.
ReplyDeleteasante
mimi nimeshangazwa na matangazo yanayotolewa hapa chuoni eti chuo kimejiunga na NECTA sasa inakuwa hivi
ReplyDelete1. fomu ya kuingia hapo chuo inasema mfano diploma ni miaka miwili na maelezo mengine.
2. baada ya kuingia darasani baada ya miezi sita haya ndiyo yaliyofuata yakipingana na na. 1
3. diploma ni mwaka mmoja unapewa cheti cha (technician) secretary anapewa cheti cha technician ya nini na diploma gani ya mwaka mmoja
4. matokeo ukipata vipindi vyote kwa grade ya c umefeli unaenda nyumbani uruhusiwi kusoma tena katika vyuo hivyo mpaka umekaa nyumbani mwaka mzima.
5. kwa hiyo tunachoshangaa ni hiki kuna diploma ya mwaka mmoja hatufahamu.
6. Nilichogundua mimi ni kwamba chuo hiki kinafanya biashara sana hivyo kwa mtazamo wangu NECTA ina idadi ya wanafunzi wanaopashwa kupewa vyeti kwa mwaka yaani idadi, lakini kutokana na hawa wa utumishi wanachukua idadi kubwa sana hawatapewa vyeti hivyo wameamua kutumia ujanja ujanja kuwakatisha watu masomo baada ya mwaka mmoja na kuwarudisha nyumbani eti wewe ni technician wa nini jamani mimi nachoka
Naamini wanasoma blog hii ni wadau msaada utapatikana. Pia kama uongozi hauilewi wawasaidie sana ili nasisi tuondokeana na kutoelewa kwao
HATIMKATO
Ahsante ankal kwa kutoa hii habari za masecretari.
ReplyDeleteHakika ankal, sisi masecretari tunanyanyasika sana tena sana. Manyanyaso yetu yanaanzia pale Magogoni. Chuo hiki cha Magogoni ukisoma pale utaapa sitaenda nisome tena magogoni! Unasoma na mtu hawezi Hatimkato hata spidi ya 40, shorthand ndio hata shorform ile ya kuanzia hawezi, Kiingereza ndio basi, wewe unajipinda hulali usingizi. Lakini mwisho wa siku mtu huyu asiyejiweza anatoka na Hatimkato 100 na shorthand 100! Jamani! kuna haja gani kuwa na chuo kama hiki? Je unategemea mtu wa namna hii utendaji wake kazini utakuwa vipi kama siyo kila kitu kwake ni njia za panya tu! Sasa kwa jinsi hii aliye Sekretari anategemea kupata haki kutoka wapi na wakati manyanyaso yanaanzia chuoni? Hiki chuo cha Magogoni kimejaa rushwa kushinda idara za mahakama, hospitali, n.k. tena chenyewe hakichagui aina ya rushwa! yenye pesa twende, ngono ndiyo mwake!
Ukija kwenye mshahara. Sekretari analipwa chini ya mhudumu tena kupanda kwa mshahara wa sekretari unaambiwa uwe na Shorthand 100 na Hatimkato 80, lakini wahudumu wao kila baada ya miaka miwili wanapandishwa mshahara tena bila hata cheti cha semina! Na ukiangalia siku hizi ktk ofisi za serikali hakuna mhudumu anayefanya kazi ya usafi, sana kazi zao ni kuchemsha chai na kupeleka majalada kwa mabosi tena ukimtuma sekretari anakwambia huwezi kunituma wakati nakuzidi mshahara. Jamani wakuu wetu wa kazi sekretari ni mtu muhimu sana katika ofisi yoyote. sekretari ni kiungo katika ofisi, sekretari ndiyo kioo cha ofisi, bila sekretari hakuna mawasiliano/mahusiano kati ya bosi na watendaji wake, Wizara/idara kwa ujumla. Wewe bosi unayemdharau sekretari wako elewa sekretari ni mtu muhimu sana kwako na ktk ofisi yako. sekretari mpende, mheshimu kama familia yako. Jua ukiweka dharau/uadui naye naye akaamua kuwa adui yako ni dakika moja tu anakuangamiza, kwa kukuharibia kazi hata kutoa roho yako! Tuwaheshimu sana hawa watu.
Narudi kwetu sisi Masekretari.
(i) Tujiheshimu. unajua ili mtu akuheshimu anza mwenyewe kujiheshimu ndipo mtu/watu wengine watakuheshimu. Kuna baadhi yetu ambao vyeti vyao ni "ngono" aliipata kwa ngono na anaitendea kazi kwa ngono! Heshima ianzie ndani mwako. Bosi anakutongoza kutegemea wewe mwenyewe utakavyojiweka.
(ii) Tupendane. Sisi wenyewe hatupendani sasa haki tutaipataje? Haya yote yanatukuta kwa sababu hatupendani kwa kuwa hatupendani hatuna umoja. Hili ndilo linalofanya tushindwe kutetea haki zetu. Mimi nikiwa sehemu nzuri au nimemdhibiti bosi napata maslahi basi wenzangu wasio na nafasi hiyo wakidai haki zao nawaona kama wakorofi tena ndiye ninayebeba majungu kupeleka kwa hao mabosi. Kwa hali hii tutabaki kulalamika maisha yetu yote hakuna haki tutakayopata.
(iii)Tuna chama chetu lakini ni bora ijulikane moja kuwa hatuna chama. Sijawahi kusikia tamko lolote la chama kuhusiana na haki za Masekretari wala utetezi wowote, wala utekelezaji wa maazimio tunayokubaliana wakati wa mikutano yetu ya kila mwaka. Yote haya ni kwa sababu hao viongozi wa chama ndio hao ambao wako kwenye neema wewe haki yako inamhusu nini? Masekretari tupendane ili tuungane tuwe na umoja kama waalimu, wanavyuo na kada zingine ili tuweze kujitetea na kupata haki zetu.
Tuna chama chetu lakini ni bora ijulikane moja kuwa hatuna chama. Sijawahi kusikia tamko lolote la chama kuhusiana na haki za Masekretari wala utetezi wowote, wala utekelezaji wa maazimio tunayokubaliana wakati wa mikutano yetu ya kila mwaka. Yote haya ni kwa sababu hao viongozi wa chama ndio hao ambao wako kwenye neema wewe haki yako inamhusu nini?
ReplyDeletehahahahaaaa!!!!!!!!! unamjua mwenyekiti (rais) wa chama hiki
haya sawa tunamuomba mungu
MIAKA 50 YA UHURU
ReplyDeletechuo kimezalisha sana tunakubali wajirekebishe tu! watafute maoni kwa wadau, waangalie hayo masomo yanaendana na wakati huu tutakuwa sawa tu, ila mimi nadhani typing, hatimkato, shorthand ni masomo yanayochukua muda sana ningeshauri yatolewe kwenye certificate ili unapo kuwa diploma upate nafasi ya kusoma na kuelewa.
hali ya chuo sio nzuri sana ila ni katika mawasiliano tu wanachuo wako tayari kwa mabadiliko ila hakuna wa kuwapa taarifa sahihi hapa kwangu naona ndilo tatizo
secretary:
ni yule aliyesomea na kuelewa mafunzo na yule anayenda na wakati (kitaaluma) na kijamii.
ni kiungo kikubwa sana katika ofisi kwa kazi, lugha na kila kitu, nawaomba wachangiaji kama ni secretary usitumie lugha isiyokubalika ili tueleweke.
Mic ya ankal, imetupazia sauti asante sana
TUMEDHUBUTU, AMEN TUTAWEZA
SPEAKING OF THE DEVIL!!!!
ReplyDeletekihi chama tapsea kwakweli nadhani kazi yake kubwa ni makusanyo na kutupora wakati wa makongamano. yaani utafikiri nyuma yao kuna tapeli fulani anawapa mikakati.
MWENYE AKILI NA AFAHAMU
SPEAKING OF THE DEVIL!!!
ReplyDeletewajinga dio waliwao, chuo mmhh, mwajiri mmh, chama cao mmmhh, haya mimi nitaona tu necta mshara mikubwa sana chuo kinafuata hilo bila kujali maslahi ya wajiri wao wanachuo
NTASEMA TU IPO SIKU UTASIKIA
Duh!! Post imenishtua... ndo nipo certificate nataman kufika diploma... bado magogoni kunasumbua???
ReplyDeleteNaombeni ushauri jinsi ya kuelewa na kufaul HATIMKATO na SHORTHAND
asanten