![]() |
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh |
Na Mwandishi Maalum
New York
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh amependekezwa na kupitishwa kwa kauli Moja kuwa Mjumbe wa Bodi ya wakaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa.
Bw. Utouh amepitishwa na wajumbe wa Kamati ya Tano ya Utawala na Fedha ya Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, katika kikao chake kilichofanyika siku ya Ijumaa, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, Marekani.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Bw. Utouh atakuwa mjumbe wa Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka sita kuanzia Julai Mosi 2012.
Bw. Ludovick Utouh anachukua nafasi itakayoachwa wazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Afrika ya Kusini anayemaliza muda wake mwezi Juni mwakani.
Tanzania inakuwa nchi ya tatu kutoka Afrika kuingia katika Bodi hiyo tangu ilipoanzishwa. Nchi nyingine kutoka Afrika ambazo zimewahi kuwa wajumbe wa bodi ni Ghana na Afrika ya Kusini.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Seriakali atafanya kazi na wajumbe wengine wawili ambao pia ni wadhibiti na wakaguzi wa hesabu kutoka Serikali za China na Uingereza.
Baadhi ya majukumu ya Bodi ya wakaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa, ni pamoja na kukagua Vitabu vya hesabu za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Mashirika na asasi zote zilizochini ya Umoja wa Mataifa , Misheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, miradi mbalimbali inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa, hesabu za Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai zikiwamo za mauaji ya kimbari ( Rwanda na Yugoslavia)
Bodi hiyo hukutana mara mbili kwa mwaka katika miezi ya Juni na Novemba. Pamoja na kwamba wajumbe wa bodi hiyo hutakiwa kukutana mara mbili kwa mwaka, lakini wanaweza kukutana wakati wowote pale wanapohitajika.
Kwa mujibu wa taratibu za kazi, wajumbe hao watatu wa bodi ya wakaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa ( Tanzania, China na Uingereza) watasaidiwa na wakurugenzi watatu kutoka katika nchi hizo.
Wakurugenzi hao ambao watatakiwa kuwapo muda wote , Ofisi zao za kudumu kwa kipindi hicho cha miaka sita zitakuwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Safi sana Meku. Hongera kwa kupata heshima hiyo.
ReplyDeleteNingependa wale waliokuwa wanabeza elimu ya Tanzania wajifunze kwa hawa wanaopata nafasi kubwa kubwa kimataifa.
safi sana. hii kazi ya utouh.timu yake.na audit industry yote ya tanzania.
ReplyDeleteelimu yetu ni mbovu saana sema kama utouh ni juhudi binafsi huyu baba ni mchapakazi saana na anapenda kusoma na kujua mambo na hata kama wanachaguliwa hivyo mbona wakiwa hapa hawana impact pamoja na yote hayo.../?
ReplyDeleteMtoa maoni wa tatu kumbe unatambua kwamba juhudi binafsi zinatakiwa. Hakuna elimu popote duniani inayompatia mtu kila kitu. Kinachowashinda wabongo sio elimu mbaya ila jinsi ya kutafsiri elimu hiyo kwa vitendo. Elimu ya bongo ni nzuri sana. Mliofeli msiite mbaya.
ReplyDeleteHata wakaibadilisha wakakuwekea hiyo unayotaka bado itakushinda tu ama unaweza kufaulu na bado ushindwe kuitafsiri kuwa vitendo ama unaweza ufeli vilevile. jitihada binafsi ni muhimu popote duniani.
Hongera sana boss kwa kutupatia heshima hii kubwa.
ReplyDelete