Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Kepteni Mstaafu , Seif Mpembenwe, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Luteni Mstaafu Chiku Galawa, Novemba 24, mwaka huu mpakani mwa Mikoa hiyo eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , akizundua jengo la mradi wa Benki Mazao katika Kijiji cha Dihinda, Wilaya ya Mvomero , Mkoani Morogoro, Novemba 24, mwaka huu wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani hapa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , ( wapili kutoka kushoto) akiuliza Mkulima, Hamida Mrisho wa Kilimo cha Umwagiliaji wa zao la Mpunga katika Kijiji cha Mkindo, Wilayani Mvomero, Novemba 24, mwaka huu juu ya uzalishaji wa zao hilo kwa ekari ,wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani hapa,( watatu kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Halima aDendego , ambaye ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mvomero na Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akisoma hotuba ya Mkoa wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Tanga, eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero, Novemba 24, mwaka huu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , akikaaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, kutoka Mkoa wa Tanga, eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero, Novemba 24, mwaka huu.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , akiagana na viongozi wa Mkoa wa Tanga na kukaribishwa na viongozi wa Morogoro, wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero, Novemba 24, mwaka huu.
Ukosaji wa kazi kweli ni tatizo kubwa !!!
ReplyDeletetutumie nguvu zetu kuondoa matatizo halisi yanayowakumba wananchi,tusijihusishe na mambo ambayo practically hayatatui matatizo tulionayo.Mwenge umekuja mara ngapi?wanaoukimbiza wanapewa allowance kubwa,watoto wanajipamnga barabarani ukiondoka matatizo yao yapo pale pale.
ReplyDeletehuo ndio uchawi wa kizanaki yaani huo ni muzimu wa mwenge wazaramo wanaita kibwengo,wahaya wanaita kimuri yaani mzimu wa moto hapo hakuna kitu kama mdau alivyosema ni uzembe tu vitu visivyo kuwa na maendereo
ReplyDeleteMwenge uwekwe jumba la makumbusho! matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi. Maaraba ngapi za shule zingejingwa kwa fedha zinazotumika kuuzungusha mwenge nchi nzima. Hakuna mantiki ya Mwenge wa Uhuru katika karne hii, huu ni ukweli usiopingika.
ReplyDeleteNi wakati m uafaka wa kuuweka mwenge kwenye makumbusho ya taifa na kutumia muda tunaopoteza kwa kukimbiza mwenge kutatua matatizo ya nchi.
ReplyDeleteMWENGE BADO NI MUHIMU SANA::::::::
ReplyDeleteItafaa tukiutumia mwenge kwa njia hizi mbili:
1.Mafisadi wakamatwe na waumbuliwe hadharani ktk sherehe za kumaliza mbio zake mbele ya wananchi na Raisi,,, huku Mafisadi wakikumbushwa kuwa mfano ktk picha ya Viongozi hapo juu Waasisi wa nchi walijitahidi uadilifu.
(((Itafaa wajifunze kuwa waadilifu)))
2.Moto wa mwenge utumike kwa kuwaamuru Mafisadi kuweka viganja vyao na kuchomwa na moto huo ili iwe adhabu kabla mwenge haujazimwa.