Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba,Mhe. Pindi Chana akijadili katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala mjini Dodoma leo. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Angelah Kairuki.Kamati imeendelea kuboresha Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2011.
Wajumbe wa kamati pamoja na wataalamu waalikwa wakifatilia kikao hicho leo mjini Dodoma.Picha na Minja -Bunge
Ankal, kimoja ninachotaka, nikiwa ni raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, ni kuona katiba mpya inatambua haki yangu ya kushiriki kikamilifu katika siasa, ikiwemo kugombea nafasi yoyote ya uongozi, kama mgombea binafsi.
ReplyDeleteMfumo tulio nao ni wa kibaguzi, sawa na ule mfumo wa kikaburu uliokuwepo Afrika Kusini, ambamo baadhi ya watu wanazuiwa haki zao kwa kutumia sheria ya kikaburu. Sheria ya Tanzania inayotuzuia sisi tusio na vyama kugombea uongozi ni ya kikaburu, na sherti ibadilishwe.
Umeandika vizuri sana Bwana Mbele.Nimependa ujumbe wako.
ReplyDeleteDavid V
wasiwasi wangu ni wajumbe wa hii kamati sidhani kama wapo makini sanaa na ni professional wa masuala ya shera na katiba!kazi tunayo watanzania!
ReplyDeleteukifungua uturn commenter wa kwanza karibu wa post zote ni Koku,kwa ankali ni David V.Nyie mnaonyesha mapenzi ya kweli Mungu awazidishie
ReplyDeleteWajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Mabadiliko ya KATIBA, msipoteze muda, katiba yetu ni mbovu kabisa lazima ipigwe nyundo na tupate mpya itakayo kidhi mahitaji yetu na inayoenda na wakati.
ReplyDeleteMFANO: katiba tuliyonayo Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo Raisi wake ana madaraka karibia kumfikia MWENYEZI MUNGU sasa hii sio ishara nzuri!