Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako(Kushoto) mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho kwa ziara fupi. Katikati ni Balozi wa Japan hapa nchini Bw Masaki Okada.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (kushoto) akimsikiliza kwa makini Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako (katikati) kuhusu ubora wa betri zinazozalishwa na kiwanda cha Panasonic cha jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Patrick Marwa.
Kutoka kushoto ni Balozi wa Japan hapa nchini Bw Masaki Okada, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Patrick Marwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini TBS Bw Charles Ikelege( Kulia) akielezea ubora wa bidhaa za kampuni ya Panasonic ambayo ni miongoni mwa kampuni za mwanzo kabisa kupata nembo ya Ubora kutoka TBS.
Balozi wa Japan hapa nchini Bw Masaki Okada(Kushoto), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu(Katikati) na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako( Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda cha Panasonic.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hao jamaa siku hizi wanatengeneza tochi na betri tuu Radio wameacha siku nyingi sana.sijui kwa nini serikali haikuwasaidiaau kuongea nao kutengeneza hata television kwani wamekuwepo kwa miaka mingi toka television zinaingia wangeweza kulishaika soko na kuwapatia ajira watu wengi badala ya wachache waliowaajiri sasa. Serikali yetu haina kabisa mipango ya kuwasaidia wenye viwanda kuongeza ajira!

    ReplyDelete
  2. Tatizo wabongo mmezoea cheap fake, panasonic wanatengeza kila kitu mpaka leo lakini hawaleti bongo mnampenda mchina betri ya nusu saa imekwisha europe kuna kila kitu cha panasonic na bado wako kwenye soko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...