Mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza kwa takribani masaa manne bila kupumzika imeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za usafirishaji kwa njia ya anga kutokana na maji mengi kujaa katika uwanja wa ndege wa jijini humo.kama ionekanavyo pichani hapa.
Ngazi Maalum zinazotumika kapandia abiria kwenye ndege kama zinavyoonekana kutokana na mafuriko yaliyoikumba airport ya jijini Mwanza leo mara baara ya mvua kubwa kunyesha.
Hakuna Ndege yeyote iliyoondoka wala kutua leo jijini Mwanza maana hali ilikuwa ni mbaya sana.
Hapa leo hakukuwa na kazi yoyote nyingine leo.
Sehemu ya kurukia Ndege ikiwa imeharibika vibaya kutokana na Maji ya Mvua iliyonyesha siku ya leo Jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza wakiendelea kufanya taratibu ya kuweka vitu sawa katika chumba cha kupita abiria wanaosafiri.huku maji yakiwa yameingia mpaka ndani.
Ndege zilizofanikiwa kuruka katika uwanja huo wa Mwanza ni hizi tu,lakini zile za abiria hakuna hata moja iliyoweza kuondoka wala kutua.
Wafanyakazi mbalimbali wa kiwanja cha Ndege cha Jijini Mwanza wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda katika eneo hilo.
Ilikuwa ni kama bahari ndogo katika kiwanja cha Ndege cha Jijini Mwanza leo.Picha Zote na Mdau G Sengo.
Hali hii itaendelea kutokea na kutokea tena na tena hadi mageuzi yatakapofanyika.
ReplyDeleteInabidi wachimbe mitaro mipya au waiboreshe ile iliyopo kuimarisha "drainage system." Kwa sababu hii yote inatokana na "poor drainage system." Sisi wengine ndiyo airport yetu hiyo tunayoitumia mara kwa mara, kama msaada unahitajika kutoka kwa umma, tafadhali itangazwe (ili mradi asile mtu hela). Jamani tujitahidi tufanye ukarabati kabla sherehe za uhuru na krismasi hazijakaribia. La sivyo, tutaua si tu bishara, bali na sherehe na likizo kwa wananchi na wageni vile vile-huu mi muda nyeti jamani. Naomba kuwasilisha maoni.
ReplyDeleteHuu si uwanja wa denge , Watanzania adi lini tutaacha ubabaishaji , na kuweka uzalendo mbele! tujipende jamani na tupende nchi yetu.
ReplyDeletemdau kisumu kenya
miaka 50 ya uhuru
ReplyDeleteDuh: ndo tunashehereke miaka 50 ya uhuru kwa jiji kuwa na uwanja wa ndege kama huo?
ReplyDeleteKaka naona umeamua kuwa msaidizi wa kuimarisha biashara ya pombe, nakuonea huruma baraka zote zitaondoka na mwisho wake ni mbaya. yetu ni dhikri yaani ukumbusho na kufikisha ujumbe,wala usikasirike tunaomba M Mungu akuhidi.
ReplyDeleteAsante mdau kwa picha nzuri.Ilikuwa hatari hey??
ReplyDeleteDavid V
Hii inaonyesha ni jinsi gani miundo mbinu ilivyo mibovu inatakiwa wajenge sewage systems kulingana na mahitaji ya kiwanja.
ReplyDeleteMIAKA 50 YA UHURU HIYO.
ReplyDeleteUwanja wa ndege umejengwa kwenye njia ya maji - hayo ndiyo matokeo ya kujenga bila ya kufanya tathmini ya athari ya mazingira (EIA).
ReplyDeletePoleni sana Wana Mwanza, lakini Serikali lazima ihamishie huu uwanja katika eneo jengine, this time with full EIA carried out.
JAMANI HALI TUMEZOEA KUONA KWA WANAOISHI MABONDENI HII NI AIBU KUBWA SANA KAMA MPAKA MIUNDO MBINU YA VIWANJA VYA NDEGE INAKUWA KATIKA HALI HII NA TUNA WAKANDARASI WASIMAMIZI WA UJENZI WA VIWANJA VYA NDEGE WAPO TU, NINGEKUWA MHESHMIWA KWELI NINGEWAFUTA KAZI WAHUSIKA WA USIMAMIZI WA UWANJA HUU KITENGO CHA UJENZI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteKIPEPEO
Uwanja uko vile vile tu tokea enzi za mzee marehemu Machemba! hii kazi kweli
ReplyDeleteMIE NIMEIPENDA HIYO YA NDEGE WALIOFANIKIWA KURUKA. HAO NAONA WANARUKA KWA KUSHANGILIA. WENZETU KUTOKA ULE MKOA FULANI WANGEWEZA PIA KUTUSAIDIA KUSAFIRISHA ABIRIA WALIOKWAMA KWA KUTUMIA KILE KIFAA CHAO MAARUFU KWA JINA LA UNGO ILI RATIBA YA SAFARI HASA KWA WALE WANAOUNGANISHA ISIKWAME HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA SAYANSI NA TEKE LINALOKUJIA WAKATI WATANZANIA TANAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU HII INGEKUWA POA SANA.
ReplyDeleteKUHUSU TANGAZO LA POMBE, HII NI MOJAWAPO YA NJIA YA KUJIPATIA KIPATO HIVYO LABDA MCHANGIAJI ANGEKUPATIA TANGAZO LAKE LENYE MSHIKO ZAIDI YA HILO LA POMBE KWA MASHARTI YA KUFUTA HILO LA POMBE
wabongo bwana natural disaster haizuiliki kirahisi, mi naona hata ingetokea tsunami kama ya japan au tetemeko la turky bado mngechonga tu.
ReplyDeleteKwani wakati wanajenga huo uwanja , hawakuwa na wazo kuwa mafuriko yakitokea itakuwaje, hiyo ndio Tz bwanaa. Miaka 50 ya uhuru , Tumejaribu , Tunaweza na Tunasonga mbele wapi..... Miundo mbinu mibovu sijawahi ona jamani, Huku Dar mvua ikinyesha kidogo mimaji hiyo mireji imeziba kuzibuliwa hazibuliwi.
ReplyDeleteMungu wabariki watanzania leo natural Disaster mtu anadiriki kusema miaka 50 ya uhuru na tsunami ya japan ilikuwa miaka mingapi ya uhuru, sasa hapo mnacholalamika ni kitu gani? ni mvua imenyesha imeharibu miundo mbinu mlitaka miaka 50 izuie mvua na majanga mengine hivi ni kweli tumechoka kufikiri kiasi hicho???
ReplyDeleteUKANDARASI FEKI, KUPEANA MIKATABA KWA KUFAHAMIANA. HII ITAENDELEA DAIMA
ReplyDeletewe mchangiaji wa mwisho ni kweli kuna disaster nakubali ila kwa watanzania jamani uwanja wa ndege kama huo ni aibu kubwa sana yaani naogopa hata kuangalia hizo pic najisikia vibaya sana huku tuna miaka 50 ya uhuru,huku wabunge wanalalamoka kuongezwa mapesa jamani jamani kwanini hizo pesa wanazotaka kuongezwa zisifanyiwe mambo kama hayo na kusaidia jamii kwa ujumla kuliko wapewe wabunge na kutumbua na familia za ukiwaangali waneneeeeee hata kuhema wanashindwa,wakiumwa kidogo wanakimbilia india home vifaa vya hospital na machine hakuna watu wanakufa na hata hizo machine zenyewe ni bei ghali sana kulipia mpaka upimwe au unaambiwa kuwa usije leo mpaka siku fulani mtu yuko mahututi. oooh tanzania weeeeee ni nchi yangu naipenda sana ila akili za viongozoi zimelala,viongozi wanapenda sana kusafiri jamani mambo hayo mpaka lini na hata waki\safir nchi za nje hawajifunzi wenzao wanavyoishi jamani,
ReplyDeleteWewe anoni unaesema natural disaster una matatizo ya akili. Mvua ya kupita unaiita natural disaster? Tena bila aibu unafananisha na tsunami iliyotokea Japan? KWeli tanzania ina vihiyo? Bora nibaki nje nisije kuambukizwa upuuzi bure
ReplyDeleteNimefurahishwa na ndege walobahatika kuruka JAMANI NIMECHEKA SANA!
ReplyDeletejamani wadau wengine vip? unataka asiweke tangazo la pombe aweke lipi? we kama yamekushinda huku toka utupishe sie wanajamii, huu mtandao ni wa jamii na si wa dini fulani, hivyo lazima mambo yote yaende sawa, hata kama kuna sehemu nzuri ya kuchomea kiti moto tuwekeeni hapa wadau tuone, tumeambiwa kimuingiacho mtu si najisi bali najisi ni kimtokacho, Upo hapo weweeeeeeeee
ReplyDeletekikwete alishasema kilimo kwanza!!!
ReplyDeleteUKIONGOZWA NA KIPOFU NA WEWE NI KIPOFU LAZIMA WOTE MTUMBUKIE SHIMONI.KUAJIRI WATU KUNAHITAJI KUWE NJE YA MADHARA YA RUSHWA.HII SI MARA YA KWANZA KUJAA MAJI KWA UWANJA,KAMA NCHI ZINGINE KUANZIA ALIYEDESGHN NA INJIANI A ALIYEKAGUA NA KUTOA KIBALI WOTE WANGEFUKUZWA KAZI NA BAADA YA HAPO SERIKALI INAPASWA KUTOA MAELEZO-KWA NINI UWANJA ULIJENGWA MAHALI PASIPOFAA WAKATI NCHI INA ARDHI KUBWA NA YA KUTOSHA????AIBUUUUUUUUU TUPUUUU.50 HAMISNI YA UHURU SI MANENO NI VITU WAZI.
ReplyDeleteAma kweli ndege wanyama ndio pekee waliofanikiwa kuruka!
ReplyDelete1D1OTS...Ule mji wote wa Mwanza ni ZIWA...maji yalihama kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa...Maji yana-history ya kurudi sehem yake so it'z just a matter of time...hakuna cha miundo mbinu wala nn!
ReplyDeleteMiaka 50 ya uhuru hakuna kilichofanyika. Wape CDM wazee wa kazi, walete mabadiliko, CCM uwezo wenu ndo huo tumeshauona, hauwezi kutufikisha popote.
ReplyDeleteHAYO NI MAFURIKO JAMANIIII. HAKUNA MITARO HAKUNA NDEGE. ZOTE ZINALALA.
ReplyDeletekama hata ile mvua ni natural disaster,basi mie sijui maana ya natural disasters..
ReplyDeleteHii ndio GHARAMA YA KUUBEBA UFISADI...MTU MMOJA ANAHAMISHA FEDHA ZA UMMA KWENDA KTK AKAUNTI YAKE ANAKULA YEYE NA FAMILIA YAKE...HUKU MIUNDO MBINU IKIWA MIBOVU...KTK MANAGEMENT EXCELLENCE HAKUNA NATURAL DISASTER WALA SABABU ZISIZOWEZA KUZUILIKA...HIZI NI NGANO ZA SIASA ZA KIBONGO!
ReplyDeleteNatural Disaster gani hapa?....wakati miundombinu inaonekana MIBOVU KABISA,HAKUNA FLOW LINES ZA MITARO YA MAJI, ile LAMI KTK RUNNER WAY YA UWANJA WA NDEGE IMEJENGWA CHINI YA KIWANGO ,INAONEKANA KTK PICHA IMEMEGEKA thank you MDAU ALIYEPIGA PICHA AMETUSAIDIA SANA... inawezekana kabisa MKANDARASI ni wale wale SISI KWA SISI CO.LTD.
ReplyDeleteMKANDARASI WA UWANJA WA NDEGE Mwanza inawezekana ni TULE CHETU CO.LTD. au ile MWEKEZAJI TULEPAMOJA CO.LTD.
ReplyDelete