![]() |
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wakiwa kizimbani leo jijini Arusha. |
Picha na habari Na Woinde Shizza
wa Globu ya Jamii, Arusha
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu pamoja na wafuasi wao kadhaa wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kutuhumiwa kufanya mkusanyiko wa watu kinyume na sheria.
Mbali na mashitaka hayo Dk. Slaa pia anakabiliwa na shitaka lake peke yake la kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi akiwa katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya NMC.
Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Devotha Kamuzora,Mwendesha mashitaka wa serikali Haruni Matagane aliiambia Mahakama hiyo kwamba kosa la kwanza na la pili linawakabili watuhumiwa wote 27 ambalo ni kufanya kusanyiko kinyume cha sheria na kutokutii amri ya jeshi la polisi.
Akisoma shitaka la pili Haruna aliiambia mahakama hiyo Dk. Slaa anayekabiliwa na mashitaka ya uchochezi ambalo ni kosa la tatu anadaiwa kutoa kauli zenye uchochezi akidai kuwa atahamasisha wafuasi wake waandamane hadi Magogoni Ikulu kuhakikisha wanamg'oa madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Kipengele kingine kilichotajwa na mwendesha mashiataka huyo ni Dk. Slaa kutangaza kwamba watakodisha ndege kwa ajili ya kumbeba Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Zuberi Mwobeji na kisha wampeleke Dar es Salaam kwa IGP ili kumuuliza kwanini hadi leo hajamhamisha kazi OCD huyo.
Katika kesi hiyo upande wa watuhumniwa wote 27 unawakilishwa na mawakili wawili ambao ni Method Kimomogolo na Albert Msando ambao kwa pamoja waliiambia mahakama hiyo kuwa wateja wao walikuwa na watu wa kuwawekea dhamana kama mahakama hiyo itaona kuna umuhimu huo.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Devotha Kamuzura aliwaambiwa watuhumiwa kwamba dhamana yao ipo wazi lakini kwa masharti ya kila mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili na ahadi ya dhamana ya shilingi milioni tano.
Hata hivyo hadi mahakama hiyo inaashiriwa watuhumiwa 17 ndio walikuwa wamekiwisha kupata dhamana huku watuhumniwa tisa wadhamini wao wakishindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 22, mwaka huu mahakamani hapo.
Nyerere alisema "..waacheni tu waandamane, wabebwe juu juu au waongee tu chochote kwani ndiyo demokrasia. Viongozi wakiwa wasafi wapinzani hawatakuwa na la kuongea"
ReplyDeleteNakupenda sana Tanzania!
kama ndio wataendesha serikai kwa kuvunja sheria hawa 2015 hawaoni ndani. Hata rais yuko chini ya mahakama. Viongozi wanaovunja sheria watasimamishaje sheria na uongozi bora. Wao wenyewe tangu wamechaguliwa wanapamba rumande za Arusha. Mimi si mwana CCM lakini kinachoendelea hakifurahishi kabisa.
ReplyDeleteNinahisi kiberiti kimeshawashwa Tanzania, ni suala la muda tu and we are too late to turn back. Ni kweli kuna sheria, lakini pia tukumbuke kuwa mababu zetu waliishi kwa amani sana kwa kutumia busara tu kuliko hata sisi tunotumia sheria. Lakini endapo tutachanganya sheria na busara bila ya mizengwe mizengwe tutaishi kwa amani zaidi (ceteris paribus).
ReplyDeleteHIVI NDOO MAAANA NENO LA MUNGU ALISHINDWA KULIENDESHA KAMA KAULI ZAKE NDOO HIZI HII NI YA PILI BUSARA NIN KITU CHA BUREEEE JAMAN SASA.MFADHILI MKUU WAO KASEMA USHOGA LAZIMA WAO MPAKA SASA KIMYA NDIO MAANA WANAKUBALI ILI WAPEWE MASAADA AU KUKOSOA MENGINE NI SAWA JE ILI HALINA MANTIKI KWA TAIFA JAMAANI AU BOSS NI BOSS HACHANI WOGA CHADEMA BE SMART WTZ TUKO PAMOJA KWA MASLAI YA TAIFA PAMOJA NA UTAMADUNI WETU WA KIAFRICA SI CAMAROONI.
ReplyDeletehawa chadema wanavuruga amani, wanaharibu biashara, wanakimbiza watalii arusha, wanafunzi hawana amani hivi ni kitu gani wanafanya? mbona hawatumii akili jamani???
ReplyDeleteJamani tatizo sio CHADEMA, tatizo ni dola. Mtoa maoni wa kwanza ninampongeza sana. Hivi watu wakikaa kikao chao kwa amani tena bila hata fujo...kwa nini polisi waende na mabomu na silaha za moto? Dola ndio inavuruga amani yetu. Wakumbuke hata Libya walianza hivyo....Kama dola (viongozi) ni safi wasiwasi wa nini? Kwani watu wakifanya kikao chao jangwani wakasema wanayotaka wao viongozi wanahofia nini? Wanahofia maovu yao kuwekwa hadharani. Kama sio CHADEMA nani angejua masuala ya EPA, DOWANS, MEREMETA, N.K.? Nawashukuru sana CHADEMA kwa kutusaidia kuona upande wa pili wa shilingi ya CCM...Aibu kwao. Sioni walifanya CCM, matatizo ni yale yale tangu 1961. We need changes now....
ReplyDeleteyaani CCM kweli na kuongozwa kwao na wanaUsalama wanashindwa kujua mbinu ndogo wanayoitumia Chadema. jinsi wanavyohangaika nao ndio wanavyowapa umaarufu sasa hapo wanaonekana mashujaa kweli huko Arusha na huo ndio mkoa utaongoza kwa uchumi mzuri kama wizara na Ikulu zikiamishwa Dar. sasa inabidi waachane nao tu hata kama kuwakamata wasiwape umaarufu kiasi hicho
ReplyDeleteMimi sio mwana CCM lakini tabia iliyojionyesha na wana CHADEMA hasa viongozi wao ambao ni wasomi kwakweli sitakaa nipige kura yangu kuchagua RAIS wa Tanzania toka CHADEMA watatumaliza wananchi maana watu tuna akili zetu tusingependa kuongozwa na vichaa/majinun; hasa huyo Tundu Lisu namshangaa kweli lazma atakuwa na tundu kichwani mwake ambalo linavujisha heshima na akili zake siku hadi siku - haya majina tunayopewa binadamu pia huwa yanatuathiri kwa namna moja au nyingine.
ReplyDeleteMsemaji wa kwanza nakupa BIG UP kwa kunikumbusha maneno ya baba wa taifa!Kwa kweli CCM wanahangaika kwa kuwa wanajijua hawapo sawa yaani wamechemshaaa!
ReplyDeleteUV-CCM Arusha walifanya maandamano na mkutano bila kibali hawakukamatwa wali hawana kesi, wakifanya chadema...!!!??? polisi, ccm na inteligensia nouumaah.
ReplyDeletelol!
ReplyDeleteUtawala bora ni ndoto kwa TZ. Wanachadema msivunjike moyo kwani mukizubaa mutaungana nao na kua jora moja.
ReplyDeleteHaki haidaiwi kwa kulala usingizi "Never"
polisi Arusha acheni kuwanyanyasa CHADEMA kama wanataka kufanya mikutano msiwaingilie kwani wamepigana na mtu au kuvunja mali za watu? mbona mnawaonea tu ila its gud coz mnazidi kuwapa umaaarufu CHADEMA na plan yao inakwenda kama walivyoikusudia....now how is the looser between them
ReplyDeleteNdio tunataka mabadiliko ya kisiasa, lakini itakuwa ni vigumu sana kwa chama ambacho tunaamini kwamba kingeleta mabadiliko nchini, viongozi wao kuonekana wao ndio waanzilishi wa vujo. Amani, haipatikani kwa njia hiyo (vujo vujo) au kwa njia ya Upanga! bali kwa hotuba, nzuri, amani kwenye vituo vya mikutano, wafuasi wengi tuonekana!!
ReplyDeletehahahahaha..... majina na tafsiri zake!!!!
ReplyDeleteKWELI MWANAO MTU UNAWEZA UKAMZAA UKAMWITA TUNDU - HUYU LAZIMA KAZALIWA NA KASORO. HIVI KIKWAO INA MAANA GANI. MIMI HATA KABLA HAKUINGIA CHADEMA NILIMWONA NI MKOROFI. SERIKALI HAIWEZI KUENDESHWA NA WAKOROFI. JAMANI HAWA 2015 WATAPEWA KURA NA VICHAA WENZAO LAKINI SISI WATU WAZIMA WENYE MAARIFA
ReplyDeleteIngekuwa wakati wa Mjerumani ni kuwachapa bakora (hamsa 20) na kuwaacha waende zao!
ReplyDeleteSina chama ila viongozi CHADEMA mmechemkaaa!Mnafanya mambo kwa kukurupuka! kama mlijipanga basi msingewakimbia polisi mkawaacha wafuasi wakiumizana uwanjani, Askari kuwafuata kuwakamata ndio wangezidi kuwapa umaarufu, ila kukimbia kujificha na kuwaacha wanachama wasijue cha kufanya kumewadhalilisha, Hapo ndio mtanzania ujue litakapofukuta mwafwa bure mkaacha familia zenu!!! CCM nimewachoka ila CHADEMA sitakaa niwape kura yangu.. Bado hatuna viongozi hadi baadhi ya watu fulani ninaowajua mimi watakapojiengua CCM na kuanzisha chama ama kugombea wakiwa humohumo CCM, Nitafikiria kuwapa kura yangu!!!
ReplyDeleteSina chama ila viongozi wa CHADEMA mmechemkaaaa!Inaonyesha ni jinsi gani hamkujipanga bali mlikurupuka kuitisha mkutano wa wanachama wote mkidai kutotendewa haki, Polisi kitu walichokifanya ni kuwapa umaarufu, hamkutakiwa kukimbia na kujificha mkiwaacha wanachama wenu wakiumia na kuhangaika wasijue cha kufanya,Bali mngeendelea kuwa kitu kimoja hadi kieleweke..Hapo ndipo Watanzania wenzangu mnatakiwa kujua siku mtakapoacha familia zenu zikiteseka usimuone wa kumkimbilia... CCM nawachukia SANA, Ila CHADEMA kura yangu kamwe siwapi!.. Bado sijamuona kiongozi wakuiongoza TZ mpaka sasa!! Labda baadhi ya watu kama wawili hivi kutoka ndani ya CCM,ambao ndio kidogo naowaona wana msimamo.. Either waanzishe chama ama wateuliwe na CCM kuiongoza TZ..Hapo naweza unga foleni kupiga kura yangu. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteMichuzi, you are very bias, unaweka maoni ya wana ccm, mbona yanayo kashfu hili tukio huweki?
ReplyDeleteKinachofanywa na dola ni ukiukwaji wa haki za binadamu, mtu ana uhuru wa kusema chochote kuhusu yeyote.
Silaha siku zako za kuaibika zinakaribia.Nakuhakikishia kadri siku zinavyoenda unazidi kujivunjia heshima katika nchi hii maaana matendo yako hayafanani na tulivyokufikiri hadi tukaamini unaweza ongoza nchi hii tukakupa kura zetu bahati mbaya kwetu mwaka jana kura hazikutosha ila sasa tunashukuru maana tunaona tulikuwa tumefanya makosa makubwa saaana kukuamini ungetupeka pabaya kama hii ndo hulka yako
ReplyDeletePANDE ZOTE MBILI ZINA MAKOSA:
ReplyDelete1.POLISI-ARUSHA: kutumia mabavu na kusababisha mazingira yaliyozaa suala hili.
2.CHADEMA: kuwa na jazba na kiburi ktk kuliendea suala hili.
SASA NI KUWA KUKOSA BUSARA kwa pande zote mbili kunatupelekea kuwa aibu na kichekesho ikiwa wageni wataona hili.
MGOLOLE ALIOVAA MH. TUNDU LISSU ni vazi la heshima na busara ktk makabila yetu Tanzania hivyo mvaa mgolole haikustahili awe hivyo ingebidi atumie busara zaidi na ustaarabu!
hahahaaaa....hilo shuka lilivyovaliwa na Tundu na hiyo facial expression mie hoi kwa kucheka...huwa namzimia jamaa sana, i can imagine hapo alikuwa anawaza nini!
ReplyDeleteFREEMAN MBOWE MSALITI!!!!!!!.....jamani huu ndio mshikamano ktk chama?,Tundu Lissu,Wilbroad Slaa na wengine kutiwa nguvuni na wengine 17 kubakia huko ndani kwa kukosa Dhamana, huku Mwenyekiti Mbowe akija siku ya pili asubuhi kujisalimisha POLISI ARUSHA huku aliongozana na KADA WA KIKE WA CHAMA!...hii ni siasa au ubabaishaji wengine kuwa waliwao?
ReplyDeleteNDEGE JOHN::::: NDIO MUONEKANO WA MHE. TUNDU LISSU, Jamaa anatia huruma sana na mgolole wake(shuka la kimasai) kwa vile yeye ni Mwanasheria kitaaluma msomi lakini anafanya mambo kama vile hakusoma sheria!!!.
ReplyDelete