Wananchi wa kijiji cha Masaera, kata ya Kilema Kusini katika wilaya ya Moshi vijijini jana walidhihirisha nguvu ya umma mkoani kilimanjaro walipoamua kuingia katika jengo la ofisi yao na kutoa vifaa vya bwana Louis Mbuya aliyeipora ofisi hiyo alipokuwa madarakani kama Diwani wa CCM na kulifanya eneo la ofisi kuwa mahali pake pa biashara ya pombe na gesti bubu! Walioshuhudia uamuzi huo ni pamoja na Mtendaji wa kijiji bwana Kidaya, Ofisa Mtendaji wa Kata Bw Kimati.

Mwenyekiti wa TLP Mkoa Bw Tesha, Mwenyekiti wa Kamati ya Mbunge ya Kutatua kero Kilema Kusini, Bw Festo Moshi na Mwenyekiti wa CHADEMA kata, bw Lyimo. Watawala wa Serikali za vijiji jirani waliohudhuria no pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilototoni, Bw Mosha, Mtendaji wa Kijiji cha Kilema-Chini, Bw Shayo na Kitongoji waNeema kijiji cha Pofo. 

Baadhi ya vitu vilivyotolewa ofisini humo ni pamoja na vileo kama banana, konyagi, viroba bia na vitanda na magodoro.Awali OCS wa himo alifika kwenye eneo la tukio lakini aliondoka ilipobainika kuwa mkutano huo ulikuwawa halali na raia hawakuonyesha dalili za fujo kwani usalama ulidhibitiwa na mgambo wa kata.

Canute Temu, 
mjumbe wa serikali ya Kijiji na Katibu Mwenezi CHADEMA,
Kata ya Kilema Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Taarifa huru inahitajika hapa, just for balancing the story!

    ReplyDelete
  2. Mmefanya vizuri iwe fundisho kwa wengine ambao wanatumia madalaka yao vibaya yaani wakisha ingia kwenye uongozi wa serikali wao wanajiona kama Mungu na wanakuwa Mungu mtu wapigiwe makofi wasifiwe wapewe nafasi za mbele ndiyo maana mambo kama hayo yanajitokeza ya kujimilikisha mali za za umma na kwa asila mngevichoma mota vitu vyote na muombe fidia maana alitumia jengo la ofisi ya kijiji kama lake,

    ReplyDelete
  3. inaelekea tatizo lipo kwa mtoa mada,anaposema kuna masomo makuu matatu yanayotofautisha typist na secretary na kuyataja kuwa ni typing,short hand na hati mkato!anamaana short hand na hati mkato ni masomo tofauti? au hati mkato ni kiswahili tu cha shorthand!
    msipende kulalamika angalieni pia mlipojikwaa!

    ReplyDelete
  4. Poleni sana masecretary. Nawapongeza kwa kazi nzito mnayoifanya. Ila na nyie wakati mwingine muwe wawajibikaji. Unapolalamika ujue malalamiko haya yanasomwa na dunia nzima. Andika vitu vyenye ukweli. Walimu wa Magogoni nawapa hongera wanawajibika ipasavyo. Tena wale wa zamani ndio kabisaa maana masec wa zamani kwa kweli wanawajibika vilivyo. Huduma kwa mteja wanajitahidi. Nadhani Mama yetu Mhe. Hawa Ghasia atafanyia kazi yale ambayo yana ukweli. Pia mimi nadhani aangalie utaratibu wa kuongeza vyeo kwa masecretary si kuishia hapo vilipo sasa. Pia uthamani wa Masec ni mdogo sana kwa waajiri wakati hawa ndo kioo cha jamii. Wapo baadhi ya mabosi wanaoona umuhimu wa Secretary, lakini pia wapo wale wasiowathamini. Miongozo ikitolewa mara kwa mara malalamiko hayatakuwepo kabisa. Lkn pia Malalamiko yawe ya msingi.

    ReplyDelete
  5. ARUSHA hapakuwa na NGUVU YA UMMA bali imetokea JAZBA YA UMMA!

    ReplyDelete
  6. hiyo ni nguvu ya mtoa mada he just exagerating a story sisi wanamasaera tunamjua na tunajua analolitafuta ndo maana amekuja na style ya kutumia blogs na magazeti ya udaku kama campaign zake za 2015 rally hapati kitu masaera udiwani ataufanyia kwake heee! story gani haijabalance huyu jamaa ana bifu na Louis Mbuya ndo maana anaegemea upande wake tupate maelezo ya upande wa pili pia au wanaCCM wa masaera nao watuambie nini kinachojiri

    ReplyDelete
  7. Hakuna nguvu ya umma Kilimanjaro wala nini...ila kuna ghadhabu ya Wachagga wachache wajinga!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...