Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu,Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa Kenya,Mh. Raila Odinga wakati alipokuwa akimsindikiza mara baada ya mazungumzo yao jana jioni jijini Dar.Kushoto ni Mke wa Waziri mkuu huyo, Mama Odinga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la maofisa wanafunzi aliowatunuku kamisheni jana katika Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na baadhi ya maofisa wanafunzi aliowatunuku kamisheni jana katika Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumamosi, Novemba 26, 2011, ametunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Katika sherehe iliyofanyika kwenye Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha, Rais Kikwete alitoa kamisheni kwa maofisa wanafunzi 506 waliofanikiwa kumaliza mafunzo mafupi ya 27.
Kati ya maofisa hao wanafunzi, 69 ni maofisa wa kike na 437 ni maofisa wa kiume na maofisa wote ni wanataaluma wakawa ni pamoja na walimu 101, maofisa mawasiliano ya umma 54, wataalamu wa utawala 48 na wahasibu 167.
Maofisa wengine walitunukiwa kamisheni katika sherehe za leo ni wataalam wa kilimo 14, wahandisi tisa, wanasheria 52, wanahistoria na utamaduni 12, waandishi wa habari 43, wataalam wa ugavi watatu na waataalam wa sayansi ya mazingira watatu.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Kenya, Mheshimiwa Raila Odinga.
Viongozi hao wawili wamekutana kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar Es salaam wakati Rais Kikwete akirejea Dar Es Salaam jioni ya jana.
Viongozi hao wamezungumzia masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Kenya na yale ya kikanda.
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 26, 2011
mbona madaktari mafamasia manesi na fani nyingine za tiba hawapo?inamaana ndio taaluma zenye maketi kubwa uraiani?minavyojua mtaalam mpaka kwenda jeshini ujue duniani kugumu sana sana watu wa tiba inaonekana ni muhimu sana duniani ndiomaana hawapo hapo na sababu kubwa hawapendi kubanwa banwa wanataka wawe huru
ReplyDeleteTunashukuru kwa Jeshi letu kuanza kugundua umhimu wa kuwa na wataalamu wa fani zote.Tunaendela kuwaasa kuwa hata fani tusizokuwa nazo tanzania watu wasomeshwe ili kwamba jeshi liwe full nondo.Bila wataalmu wa aina zote Jeshini nchi itakufa.Bado tunahitaji madktari wazuri,manesi wenye digrii na maters au hata PhD na watalaamu wa michezo,watalaamu wa Saikologia,watalaamu wa kupima ardhi,wataalmu wa wanyama nk Bravo TPDF
ReplyDeleteJWTZ lilishajua kuwa na umuhimu wa kuwa na wataalam ambao ni maofisa tangu zamani. Nilikuwa operesheni Okoa ktk JKT na nilipata chance ya kwenda Bulgaria kusoma MSc ya Ujenzi. Condition moja tu ilikuwa niende kama employed (private) na nirudipo na MSc yangu basi niende Munduli ili niwe Commissioned. Otherwise utabakia NCO na degree zako. Kama sikosei kuna madaktari pia JWTZ.
ReplyDeleteBlackmpingo
Nimeipenda hiyo picha ya kwanza juu kwa sababu zile sare zsa kutisha zilizokuwa zinakaa nyuma ya rais hazipo..wako 'simpo'sana..vijana wa kazi wamevaa tai zao..sai sana
ReplyDeletewadau daktari alikuwapo MD degree holder alihitimu Hubert Kairuki Memorial University na kufanya Internship Muhimbili Hospital, pia walikuwapo wenye advanced diploma of medicine. Mdau
ReplyDeletena hata mwaka jana alikuwapo PhD holder bingwa daktari wa mifupa na sio kweli jeshi letu lina bana wataalam wake
ReplyDeleteNi jitihada zinazoleta matuamini kwa sekta ya Wapiganaji kuchangia kitaaluma kulisukuma gurudumu letu la maendeleo, kwa vile inatambulika ni wachapa kazi na waadilifu...ila ni muhimu kwenda na Maeneo Kitaaluma yaliyo na uhitaji mkubwa na vipaumbele kulingana na mahitaji yaliyopo.
ReplyDeleteInaonesha kuwa Watanzania wengi hususani wauguzi si wazarendo wa nchi ndomana hawakujiunga na jeshi kwa lengo la manufaa ya umma .
ReplyDelete