Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuagwa rasmi kwa timu ya Taifa ya Mchezo wa Pool iliyoondoka leo kuelekea nchini Malawi kushiriki mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011.wengine pichani kutoka kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT).Dionis Malinzi,Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga pamoja na Kocha Mkuu wa Timu ya Pool ya Taifa,Dennis Lungu.
Mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT),Dionis Malinzi (kushoto) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Pool,Charles Venance wakati wa kuagwa rasmi kwa timu hiyo iliyoondoka leo kuelekea nchini Malawi kushiriki mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kuondoka kwa timu ya Taifa ya Mchezo wa Pool nchini kuelekea Mjini Blantyre nchini kushiriki mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011 yanayotarajiwa kuanza tarehe 22.11.2011 mpaka 26.11.2011.
Akitangaza safari hiyo jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo alisema “Bia ya Safari lager imekamilisha yale mahitaji yote muhimu ya Timu ya Taifa kwa ajili ya safari hiyo, pia ikumbukwe kwamba Safari Lager ndiyo mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imekuwa ikiidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa pool table tangu mwaka 2008 kwenye mashindano ya Africa na Dunia.
Timu itapita katika mikoa ifuatayo na kucheza mechi za kirafiki na timu za mikoa. Mikoa hiyo ni Morogoro, Iringa, Mbeya, Kyela- Mbeya na Kasumulo boarder- Mbeya kwahiyo ni muda mwafaka kwa wananchi kuangalia timu yenu na kuona jinsi ilivyojiandaa.
Naye kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa,Denis Lungu alitangaza majina ya wachezaji wa timu ya Taifa iliyoondoka leo kuwa ni:-
1 OMARY AKIDA - KINONDONI
2 FELIX ATANAS- DODOMA
3 GODFREY MHANDO- KINONDONI
4 MOHAMED IDDY- KINONDONI
5 CHARLES VENANCE- TEMEKE- CAPTAIN
6 ANTONY THOMAS- ILALA
7 SHAMIS NASSORO- ILALA
8 ABDALLAH HUSEIN- KINONDONI
Akiongelea kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa Bw. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu ya ALL AFRICA CUP yanatajiwa kushirikisha nchi 14 wanachama wa ALL AFRICA POOL ASSOCIATION (AAPA) na nchi hizo ni Africa kusini, Tanzania, Malawi, Zimbabwe, Cameroon, Zambia, Uganda, Swazland, Reunion FFB, Reunion Arabas, Nigeria , Msumbiji, Morocco na Lesotho.
Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Isaac Togocho alisema “ Mchezo wa pool table sasa umekuwa si mchezo tena wa kupoteza muda bali ni mchezo kama michezo mingine na unaelekea kuwa ajira rasmi kwa vijana wa Tanzania.
"Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa kuweza kuiweka Tanzania katika ramani ya michezo kimataifa kupitia SAFARI LAGER BEER ni fahari kubwa kwa mchezo wa pool table Tanzania. TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”
Bwana Misupu,naomba kuuliza,huo mchezo unaitwa
ReplyDelete"pool table" au "table pool"
kwa ufahamu wangu "pool table" ni meza ya pool.
Nawakilisha.