Mwanariadha mkongwe aliyewahi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa, Gidamis Shahanga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa kwa Taasisi ya Michezo ya Gidamis Shahanga (SSI) yenye lengo la kuinua michezo, hususani riadha, jana kwenye hoteli ya Courtyard Protea, Upanga jijini Dar es Salaam. Kulia ni mwanariadha wa zamani, John Haygahimo.
Gidamis Shahanga (katikati), mmoja wa wanariadha waliowahi kuiletea Tanzania medali katika michuano ya kimataifa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa kwa Taasisi ya Michezo ya Gidamis Shahanga (SSI) yenye lengo la kuinua michezo, hususani riadha, jana kwenye hoteli ya Courtyard Protea, Upanga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mmoja wa Wakurugenzi wa taasisi hiyo, Deusdedith Mayomba Duncana na kulia ni mwanariadha wa zamani, John Haygahimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi, mbona wanariadha wa Tz huwa wana majina ya kiaina aina sana??? Mmeshtukia??? Kama kuna mtu ana orodha ya majina atuwekee hapa muone.

    Endapo wewe una jina la kiaina aina na huna jobu cheki na riadha, au mwanao kama vipi muelekezee kwenye fani.

    ReplyDelete
  2. Mhe. Shahanga asante sana kwa habari ya kuazisha hii shughuli, labda utaiokoa Tanzania tupande juu kama majirani zetu Wakenya.

    Ukweli ni kwamba TAAA na TOC wameshindwa kufanya kitu, la maana pia kama wanaohusika wanasoma itabidi waachie ngazi uongozi.

    Bado siku 250 hamsini tuu kabla ya ufunguzi wa michezo ya OLIMPIKI huko London lakini ukweli ni kwamba bado tumelala maana timu hatuna tunasubiri tujenge timu wakati zitakapobakia wiki mbili kabla ya michezo!!

    ReplyDelete
  3. Majina wa wanariadha waliopita ambao nawakumbuka ni kama hawa;

    Filbert Sanka Bayi
    Suleiman Mjaya Nyambui
    Gidamis Shahanga
    Alfredo Shahanga
    John Haygaimo
    Peter Mwita
    Juma Ikangaa
    Boay Akonay
    Mossy Ali
    Mwinga Mwanjala
    Banuelia Mrashani
    Simon Mrashani
    John Bayo
    Chris Malundi (marehemu)
    Ali Nyonyi
    Maxmillian Iranghe
    Zakaria Gwandu
    Zakaria Maleko
    Simon Naali
    Simon Robert,,,,,,,,,,,,,

    Mwingine aendelee na orodha hii

    ReplyDelete
  4. Orodha ya wanariadha ...umewasahau wawili:

    1.Agapius Massong
    2.Afande mmoja jina lake la mwanzo silikumbuki ila la mwisho la ukoo ni Isegwe.

    ReplyDelete
  5. Gidamus Shahanga,,,ahsante umefanya jitihada nzuri sana ni kuwa kwa sasa kimichezo inabidi tuangalie maeneo mengine kama hii Riadha, pia Ndondi kwa vile imejidhihirisha wazi kuwa ktk suala la ''soka'' gharama kubwa inatumika, mipango yetu haipo sawa na bado tunakanyaga tope!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...