Balozi wa Tanzania nchini  Philippines,Mheshimiwa Sisco Mtiro aliwatembelea watanzania waishio nchini humo na kupata nao dinner la jioni.Watanzania hao ambao asilimia 99 ni wanafunzi katika vyuo mbalimbali. 

Katika dinner hiyo mheshimiwa balozi aliwasisitiza kuishi kwa kufuata sheria za nchi hii na kuepukana na magendo na madawa ya kulevya ambayo yanaweza kuliletea aibu taifa letu. Pia alisisitiza kila mtu afanye juhudi katika kila kilichiomleta huku ikiwa ni pamoja na kutangaza kwa nguvu zote utalii wa Tanzania popote tunapoishi. 

alisisitiza kuishi kwa umoja na kujaliana katika matatizo na raha wakati wote.

Watanzania waishio Philippines wanapenda kumshukuru mheshimiwa balozi kwa kuwajali na kwa kuwatambulisha kwa consulate iliyopo mjini Manila.

Mungu ibariki Tanzania

Sam.
Media & comm.
Balozi wa Tanzania nchini  Philippines,Mheshimiwa Sisco Mtiro akiwa katika meza moja ya Chakula na Watanzania waishio nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini  Philippines,Mheshimiwa Sisco Mtiro akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Watanzania kila sehemu mpo, jamani kwa masomo au ndo wabeba box, maisha mazuri? au ndo waganga njaa, rudini nyumbani muwekeze jamani mnapofanikiwa aibu, huko unaishi vizuri lakini kwenu maisha magumu na ya kustaajabisha vujumba vya ajabu ajabu tu mwishowe mnakatalia huko huko.

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa balozi je uliwahi kukutana na Watanzania waliopo Malaysia ambako ndipo ofisi zako zilipo ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...