Ndugu Maina Owino (M/Kiti CCM UK) akiwahutubia wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua sherehe hizo. Kushoto ni Suleiman Nyerere (M/Kiti Jumuiya ya Watanzania Northampton na katikati ni Mhe. Martha Mlata (Mbunge viti maalum CCM).
mgeni rasmi Mhe. Martha Mlata akiwahutubia wageni waalikwa.
mgeni rasmi Mheshimiwa Martha Mlata (Mbunge viti maalum CCM) akisikiliza hotuba ikitolewa na ndugu Katega (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM UK), wengine kutoka kushoto ni Leybab Mdegela (Katibu CCM Northampton) Kasongo Mohamed (Kassmoddy) Mjumbe Northampton, Suleiman Nyerere (Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Northampton) Mgeni rasmi na anayefuata ni Ndugu Maina Owino (M/Kiti CCM UK).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. nyie waongo mbona mmekimbia rumba nyumbani kuomba ukimbizi

    ReplyDelete
  2. HII NDIO GET TOGETHER TUNAYOTAKA, CCM ANDAENI NYINGINE YA KRISMASS. MTANGAZE TUTAJITOLEA MCHANGO BILA SHIDA ILIMRADI MISOSI IWE KAMA HII. KULA NA KUSAZA NA MZIKI MPAKA BYEEEE.

    KIBONA

    ReplyDelete
  3. ngugu yangu anony wa 05:18PM,
    kwanza salaam na pili pole. unanena kitu usichokijua na inaonekana dunia ya leo imekuacha majalala.

    Dunia yote imeendelea kwa kuhamisha teknahama toka inapotumika kwenda inapotakiwa zaidi ili kurahisisha shughuli.

    Wazungu ambao nabashiri una waabudu walifanya na wanaendelea kujitokomeza nchi za wengine tena kwa wingi ili waibe wanachoweza kwa jina la uwekezaji.

    Hawa wana CCM wa nje wameshapendekeza mengi sana ila yanazimwa kimya na wakubwa tena wanadhani ni tishio kwao kumbe wanataka mabo yasogee kwa haraka na kwa kila mtu Tanzania. JK anafinywa data hizi zinaishia chini chini. CHADEMA wajanja wanachungulia kapu lao wanapiga kubwa ndipo sasa CCM wanabaki kuhaha. Hawa ambiliki mpaka kisanuke.

    Kuomba kwa Ukimbizi ndio dili la mwenye akili. Ndio maaana wanasomesha wanafunzi mashuleni huko huko na kila siku vifaa vya mahospitalini vinatumwa na TRA na Bandari wanaiba vingine. Ushahidi mbona mwingi tu.

    Wametuma macontainer ya msaada wa mabomu ya mbagala na ukonga vingi vinanyofolewa bandarini na kodi inapigwa ya kufa mtu.

    Kwa taarifa yako wengi wamejisomesha wao wenyewe kwa utaalaam mbali mbali tena hata kwa madeni makubwa ya mamilioni lakini Serikali yako haitaki kuwatumia ili kuendeleza kasi ya maendeleo ya kisasa badala yake wanitwa WANA UCHU WA MADARAKA WATZ WA NJE.

    Ndugu yangu usiwadharau hao. Nyerere, Karume, Kenyatta ,Obote na wapiginia UHURU ambao sasa ni 50 yrs waliishi nje ya nchi kwa muda. Spring ya mwarabu imetokana na wazawa walioishi nje ya nchi. Wewe na mimi hatuwezi kujitibu haraka kama tukiwa na gonjwa hatarisho la maisha lakini viongozi wako watawala na upinzani wanapandishwa ndege daraja la kwanza kuwafuata hao unaowatukana ili kuokoa maisha yao.

    La akili ni kuibana serikali isiwachezee na danganya TOTO bali ushirikiane nao kwa ukweli ili wanachokijua kitusaidie na sisi.

    Mwamka asubuhi hujinyoosha akiangalia kwa jirani kuna nini.

    Moje Kigongo Wewedi.
    Mnyantuzu Asili.

    ReplyDelete
  4. HIVI NI KWA NINI UBALOZI WAO NA RUZUKU ZA SERIKALI HUWA HAWAFANYI SHREHE KAMA ZA CCM UINGEREZA.?

    YAANI HATA SHEREHE ZA KITAIFA NA RUZUKU JUU BADO WANA TOZA KIINGILIO VIBAYA NDIO MAANA WATU WENGI HUWA HAWAJI.

    SIKU MOJA WAJARIBU TU KWAMBA WATZ JITOLEENI KAMA CCM HAWA ILI TUFANIKISHE SHEREHE ZA KITAIFA WAONE WATAKAVYO KIMBIA MBUZI/KONDOO HALAL, KUKU KWA MABOX,MCHELE KWA TIPA LA KUMWAGA, VITUNGUU VYA KUSHINDWA GARI KUVUKA, HATA MIE NA MME WANGU TUTAJITOLEA KUPIKA KAMA NDIO ISSUE.

    KAMA NI VINYWAJI TUJINUNULIE BASI JAPO CCM HUBAKI NA MAKRETI KIBAO AMBAYO WATU WAMESHINDWA KUOGA.

    ISSUE HAPO NI KUONYESHA UZALENDO KIDOGO NA WATU WATAJISIKIA NI SEHEMU YA TAIFA.

    BIASHARA HADI NDANI YA UBALOZINI...KANGA...HINA...NYWELE BANDIA...UKITAKA HUDUMA RASMI KILA MTU NJE YA OFISI HIVI UBALOZI UNA SERIKALI ZA MITAA MAAFISA WANAKWENDA KUKAGUA KAZI??????!!!!!!!!!

    RAIS KIKWETE WE MTU MZURI SANA ILA UBALOZI WAKO HUU SASA NI MANYWANDA......KILA KONA YA UINGEREZA SASA UKIENDA KILIO NI UBALOZI, AU NDIO VIJANA WENZETU WANAVYOONGOZA????? SAFARI HII UKIJA TUTEMBELEE COVENTRY

    SHEILA RASHID BWAMKUU

    ReplyDelete
  5. Mdau Moje Kigongo Wewedi, Mnyantuzu Asili,,,wa 3 hapo juu umenena!.

    Ukweli wa mambo ndio huo, hatusongi mbele kwa sababu ya watu wachache sana wanaohesabika miongoni mwetu.

    Nchi yetu ya watu 45 Milioni huwezi amini tunaharibiwa maisha na watu wasiozidi 100!.

    Pana sinema moja ya zamani alikuwepo mtu mmoja kijijini alikuwa anaitwa YOMBAYOMBA yeye alikuwa pamoja na wanakijiji kumbe kwa siri yeye ndio mpinga maendeleo mkubwa akihujumu kwa siri kila jitihada za jamii kujikwamua.

    Ni ukweli usiofichika kuwa hata Raisi wetu mwenye nia njema kama JK anahujumiwa na hawa watu wachache.

    Na hii ndio sababu watu wanapatwa na mfadhaiko na kuona bora waishi nje ya nchi kama hawa ndugu zetu CCM-UK!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...