Ankal, habari yako pamoja na wana blogu duniani kote.
Kumbuka, juzi nilikutumia maoni ama malalamiko yangu ya ukweli kuhusu uozo wa nchi yetu watu wengi wameyapokea kwa hasira na kusema vingi vya ajabu.
Binafsi, mi si mtu wa bongo fleva (kuvaa suruali makalioni na kujifanya black american ama kuongea kiingereza na mtanzania mwenzangu wakati niko tanzania). Mi ni mtu mzima na nimesoma na dharau ni kitu ambacho sina na sijawahi kuwa nayo maishani mwangu.
Nimekuja TZ knowing kwamba nyumbani ni nyumbani hata kukiwa kubaya ila ni nyumbani na ndiyo maana mpaka kijijini niliwapeleka wakwe zangu na mshemeji waone mazingira ya nyumbani. Kuoa mzungu is not an issue anybody anaweza kuoa anayemtaka, kwanii si ni mapenzi tu? Nilichokiona ni kwamba sie huko nyumbani tuna dharau za kijinga.
Naenda benki to change my money na siyo to beg anybody na nikawa mcheshi kama kawaida yangu ili nipate huduma bora lakini ikaonekana kwamba I am too excited to be at the bank ku exchange pesa.
Kuna baadhi ya watu wanasema pale JKN Airport hakuna hao watu wanaosaidia watu kujaza visa, nawauliza mara ya mwisho walienda lini huko uwanjani? mbona hawa watu wapo tu pale wamezagaa na hawana uniforms? Sikutaka nijaziwe forms kwani nilijaza zangu mwenyewe na familia yangu when I turned around nikamwona baba mkwe amezungukwa na watu ndipo nikaenda kumwona kutaka kujua kuna nini. Bahati mbaya nilikuta tayari wameshamjazia sehemu ambazo wao wanaita short cut ya kupata visa kumbe jamaa tayari walishamchukulia mikoba yake iliyokuwa na laptop pamoja na camera.
Sasa kama hawa jamaa si wezi na kula na watu wa immigration kwa nini hawachukuliwi hatua? Watanzia tuache upuuzi, mimi ni mtanzania pure and sometimes I am proud of my country but not government kwani ni wao ndio wanaofanya nchi izorote maana hakuna hatua inayochukuliwa na serikali. Mbona it's very simple.
Pale ni kutuma mashushushu na kuona hali halisi then manager ama mkuuu wa immigration anachukuliwa hatua na ndipo huu upuuzi utakwisha ila hivi hivi, nothing will happen. Yes, I did get some nice customer service TZ especially Kunduchi beach pale hapana mfano na kama services zote zingekuwa vile mbona TZ tungeringa.
Kumbukeni, malalamiko yangu mengi yalikuwa ni juu ya sehemu nyeti za nchi yetu na ndizo nilizoenda mimi na kukutana na haya matatizo. Uwanja wa ndege ni sehemu ambayo watalii wengi hushuka. Benki ni sehemu ambazo watalii uenda ku exchange pesa. Mbugani, ndipo watalii uenda kushuhudia wanyama wetu. Hizi sehemu zote nilizozitaja customer service is extremely poor and we are not even ashamed of it, na hii yote inaonyesha kwamba TZ we dont have what we call customer service.
We umeona wapi tajiri/mteja ndiyo anamnyenyekea muuzaji/mwenye duka wakati pesa ni za tajiri/mteja? Watanzania wenzangu tuache kuongea upuuzi, I know some of you mnaandika tu ili mradi maybe you don't know kwamba hivi vitu vina exist in TZ au la mnajuwa ila hamtaki kukubali ukweli. Nendeni mbugani sikilizeni watalii wanavyolalamikia na services zetu as compared to Kenya na South Africa wakati sisi we beat them handly kwa mbuga zetu.
Yaani hatutilii maanani kabisa suala la customer service. Kuna hili pia inabidi niliwasilishe kwako Ankal. Siku tunaondoka pale uwanjani wale jamaa wanaokagua mizigo walinushapalia mimi nifungue mizigo yangu ili waone ndani nina nini. Sikukataa ila nilisikitika kwani wazungu kama 7 hivi walikuwa mbele yetu na kupita bila kukaguliwa including wakwe zangu ila ilipokuwa zamu yangu kupita jamaa akanishupalia na kuniambia nifungue mizigo yangu. Nami bila tatizo nikafanya hivyo, sasa najiuliza ni nini kilichomshinda yeye kuwaambia wazungu wafungue masanduku yao? nalo pia watanzania wenzangu mtapinga? Jamani tukubali ukweli.
Yes, kuna watanzania (hawa huku tunawaita wabongo fleva, yaani wanaopenda kuiga vitu bila kujuwa) wakitoka nje ya tanzania wakirudi wanakuja na nyodo kibao wakati mtu amekaa mwezi tu ama miaka kadhaa, mimi nina miaka karibia 25 nje ya tanzania na kiswahili naongea tena kwa kujivunia siyo nionekane feki ama mtu fulani wa nje kwani huo ni utumwa na modern ujinga. I am old enough so I am NOT a bongo fleva type.
Msipinge vitu wakati ukweli na mifano iliyo hai inaonekana nje nje. I love y'all.
MDAU UNANISHANGAZA SANA KWA SABABU HUELEWEKI, WEWE KAMA UMEONA CUSTOMER SERVICE NI MBOVU, YOU SHOULD STICK TO THE POINT ACHA KU APOLOGIZE MARA WE SIO BONGO FLEVA, EDUCATED UNAONGEA KISWAHILI FASAHA, THATS ALL BS. KWA MAANA INGINE WATU WENYE VIGEZO TOFAUTI WANA STAHILI HUDUMA MBOVU ? KWANI WEWE HUJUI MAANA YA JOB DESCRIPTION ? KAMA MTU HAJA KU VIOLATE IN ANY FORM OR FASHION WALA KUINGILIA UTENDAJI WAKO WA KAZI; MUONEKANO WAKE,UONGEAJI WAKE,ELIMU YAKE AU HATA UVAAJI WAKE SHOULDN'T BE OF ANY SIGNIFICANT WHEN IT COMES TO OBLIGATION TO FULFILL YOUR RESPONSIBILITY. KWA MAONI YANGU UMEJARIBU KU APEASE IRRENSPONSIBILITIES, INFERIORITY AND PREJUDICE.
ReplyDeleteNB: BONGO KUNA WATU HAWAJAWAHI KUTOKA NJE YA TZ NA WANAONGEA SWANGLISH, WANAVAA MILEGEZO, WANA NYODO NA MENGINE YOTE UNAYO YAJUA.
MDAU, Dirty Dirt South.
Mdau hata mimi nakuunga mkono kabisa. Mimi ni Mtanzania, msomi na nimesoma na kufanya kazi Tanzania, Ulaya na Marekani. Na kazi nilizofanya ni professional na sio za kubeba box. Nina fedha yangu nzuri, investments zangu nzuri nje ya TZ na nimeoa mtasha sio kwa ajili ya makaratasi ila kwa ajili ya mapenzi ya kweli. Nina familia yangu ya maana na mke wangu ni msomi nae ana kazi yake ya maana na sio box huku ughaibuni.
ReplyDeleteHayo yaliyokupata hata mimi yamewahi kunipata. Mimi naipenda sana nchi yangu na hupenda kuzungumza kiswahili fasaha bila kuweka Kiingereza ndani yake. Cha ajabu ni kwamba baadhi ya Watanzania wenzetu wanatuaibisha na wanaharibu nchi yetu. Kabla ya kutoka Tanzania, nilijaribu kuomba Scholarship pale Dar es Salaam, wizara ikaninyima licha ya matokeo yangu mazuri. Mtoto wa naniii aliipata ile scholarship licha ya F zake alizopata Fomu six. TNikaangaika sana na Wazungu wakatambua uwezo wangu na kunipata Scholarship. Nikamaliza Digrii ya kwanza Ulaya. Kwenda kwenye Masters Chuo kikaomba nipigiwe muhuri kutoka ubalozini kwenye Makaratasi yangu ili kuthibitisha kuwa Serikali yangu inanitambua kwa vile scholarship zile zilikuwa ni za nchi zinazoendelea. Afisa balozi yule ambaye juzi juzi alipandishwa kuwa balozi na JK alininyima msaada ule. Director wa ile Masters program hakuamini. Tukashika gari na kuelekea ubalozini na akamuelewesha yule Afisa tunachoitaji. Yule Afisa ambaye sasa ni Mheshimiwa Balozi akawa mbogo na hakuwa na msaada wowote. Tukaenda wizara ya mambo ya nje ya nchi husika (ushahidi tunao) na kuelezea kesi yetu. Wale walituelewa na wakanitafutia aina nyingine ya scholarship based on my academic records ingawa mimi sikuwa raia wao. Nikafanikiwa na kupata Scholarship na kupata Digrii ya pili. Baada ya hapo nikapata scholarship nyingine na kupata Ph.D. Marekani na sasa napeta kwa raha zangu.
Pale chuoni walinipenda sana na wakataka nianzishe miradi kwenye vyuo vikuu vya Tanzania kwa fedha zao. Nikavicontact vyuo vikuu vya Tanzania. Nikawa nasumbuliwa tu hakukuwa na kitu cha maana kuliko burokrazia zisizo na maana. Nikapeleka proposal katika nchi nyingine ya Afrika na kule tukafanikiwa. Sasa tunafanya nao research mbalimbali kwa hela kutoka huku na mwaka kesho tutakuwa Asia vile vile. Mimi upuuzi huu wa Watanzania wenzangu uliniuma. Lakini ilinibidi nipeleke miradi ya maendeleo nchi nyingine.
Ninachosema ni kuwa Watanzania tubadilike. Hivi kama mtu yuko serikalini au kwenye bodi tangu 1961 mpaka leo, tutabadilika vipi? Watoto na vijana wetu wanasoma ili wafanye kazi gani? Ni nini tija ya elimu? Halafu tukitoa maoni yetu kama wataalamu, kinachofuata ni matusi kutoka kwa watanzania wenzetu, tukitoa utaalamu kwa wazungu tunakubalika na vitu vinasonga mbele. Kweli nabii hukataliwa nyumbani kwake. Mimi naipenda nchi yangu ile nimeshagive up na nimeachana nayo kwa sababu ukuritimba, ufisadi na nipotism vinatawala.
Atakayetaka kunitukana na atakane. Kama alivyo kuwa akisema baba wa Taifa, hilo nimesema na mdomo nafunga hata mimi nasema vile vile. Sasa kwa Watanzania wenzangu wasio na akili nakaribisha matusi yao. Nitukaneni mpaka mchoke ila ukweli nitasema. Uozo hupo sana Tanzania. Asanteni.
Mdau hata mimi nakuunga mkono kabisa. Mimi ni Mtanzania, msomi na nimesoma na kufanya kazi Tanzania, Ulaya na Marekani. Na kazi nilizofanya ni professional na sio za kubeba box. Nina fedha yangu nzuri, investments zangu nzuri nje ya TZ na nimeoa mtasha sio kwa ajili ya makaratasi ila kwa ajili ya mapenzi ya kweli. Nina familia yangu ya maana na mke wangu ni msomi nae ana kazi yake ya maana na sio box huku ughaibuni.
ReplyDeleteHayo yaliyokupata hata mimi yamewahi kunipata. Mimi naipenda sana nchi yangu na hupenda kuzungumza kiswahili fasaha bila kuweka Kiingereza ndani yake. Cha ajabu ni kwamba baadhi ya Watanzania wenzetu wanatuaibisha na wanaharibu nchi yetu. Kabla ya kutoka Tanzania, nilijaribu kuomba Scholarship pale Dar es Salaam, wizara ikaninyima licha ya matokeo yangu mazuri. Mtoto wa naniii aliipata ile scholarship licha ya F zake alizopata Fomu six. TNikaangaika sana na Wazungu wakatambua uwezo wangu na kunipata Scholarship. Nikamaliza Digrii ya kwanza Ulaya. Kwenda kwenye Masters Chuo kikaomba nipigiwe muhuri kutoka ubalozini kwenye Makaratasi yangu ili kuthibitisha kuwa Serikali yangu inanitambua kwa vile scholarship zile zilikuwa ni za nchi zinazoendelea. Afisa balozi yule ambaye juzi juzi alipandishwa kuwa balozi na JK alininyima msaada ule. Director wa ile Masters program hakuamini. Tukashika gari na kuelekea ubalozini na akamuelewesha yule Afisa tunachoitaji. Yule Afisa ambaye sasa ni Mheshimiwa Balozi akawa mbogo na hakuwa na msaada wowote. Tukaenda wizara ya mambo ya nje ya nchi husika (ushahidi tunao) na kuelezea kesi yetu. Wale walituelewa na wakanitafutia aina nyingine ya scholarship based on my academic records ingawa mimi sikuwa raia wao. Nikafanikiwa na kupata Scholarship na kupata Digrii ya pili. Baada ya hapo nikapata scholarship nyingine na kupata Ph.D. Marekani na sasa napeta kwa raha zangu.
Pale chuoni walinipenda sana na wakataka nianzishe miradi kwenye vyuo vikuu vya Tanzania kwa fedha zao. Nikavicontact vyuo vikuu vya Tanzania. Nikawa nasumbuliwa tu hakukuwa na kitu cha maana kuliko burokrazia zisizo na maana. Nikapeleka proposal katika nchi nyingine ya Afrika na kule tukafanikiwa. Sasa tunafanya nao research mbalimbali kwa hela kutoka huku na mwaka kesho tutakuwa Asia vile vile. Mimi upuuzi huu wa Watanzania wenzangu uliniuma. Lakini ilinibidi nipeleke miradi ya maendeleo nchi nyingine.
Ninachosema ni kuwa Watanzania tubadilike. Hivi kama mtu yuko serikalini au kwenye bodi tangu 1961 mpaka leo, tutabadilika vipi? Watoto na vijana wetu wanasoma ili wafanye kazi gani? Ni nini tija ya elimu? Halafu tukitoa maoni yetu kama wataalamu, kinachofuata ni matusi kutoka kwa watanzania wenzetu, tukitoa utaalamu kwa wazungu tunakubalika na vitu vinasonga mbele. Kweli nabii hukataliwa nyumbani kwake. Mimi naipenda nchi yangu ile nimeshagive up na nimeachana nayo kwa sababu ukuritimba, ufisadi na nipotism vinatawala.
Atakayetaka kunitukana na atakane. Kama alivyo kuwa akisema baba wa Taifa, hilo nimesema na mdomo nafunga hata mimi nasema vile vile. Sasa kwa Watanzania wenzangu wasio na akili nakaribisha matusi yao. Nitukaneni mpaka mchoke ila ukweli nitasema. Uozo hupo sana Tanzania. Asanteni.
ndugu mdau, kwanza pole sana na yaliokukuta. hiyo ndio BONGO, ULIYOYASEMA MIMI NAYAAMINI KABISA kwa kuwa yananipata na jamaa zangu wakija au kutoka yanawapata. in daily basis.kwa bahati mbaya wabongo wamechoka na serikali wanafanya vitu bilakujali. HAKUNA KITU KINAITWA CUSTOMER SERVICES KUTOKA KWA WABONGO. ila ukiajiri wakenya au waganda YES. hata hiyo hotel uliyosema naweza kukuapia kuwa viongozi sio wabongo. Serikali ni ya hongo right from top to bottom. jana nimerudi toka safarini, askari njiani baada ya kunicheki na hakuwa na tatizo ..she was very nice and asked for chai.. niliamua kumpa out of goodfaith, lakini aliniambia kuwa nimpe wazi wazi ionekane kwa kuwa boss wake anazihesabu na lazima akabidhi mahesabu..zote za hongo na za zawadi..THAT IS BONGO. Now you can understand why JKN airport no action will ever be taken. so pole sana. mimi nilisikitika sana sasa nimecurve to the system. ndio maana wengine hawawezi kukuelewa.jambo moja ningependa nikusawazishe ni kuwa pamoja na hasira na frustrations ulizopata kutokana na uzalendo uliokuwa nao, lakini sio kweli kuwa kazi ya bank cleck ni ya kipuuzi, kazi zote ni kazi muhimu sana na nivizuri kama tungeziheshimu. hakuna kazi ya kipuuzi kwani ndio maana uliihitaji. take care.
ReplyDeleteMimi ni MTZ ninaishi hapa hapa Dar, lakini MUNGU amenijalia nimetembea nchi kadhaa za Ulaya, Marekani na Mashariki ya mbali. Seriously speaking wabongo tunatia aibu- Customer Care ni ZERO! Mhudumuu ni Mfalme badala yake!
ReplyDeletePole ndugu yangu wa Ughaibuni kwa adha zote ulizopata pamoja na wakwe zako. Kinachisikitisha zaidi ni kuwa kuna watu hawataki kuambiwa ukweli. KULIJUA NA KULIKUBALI TATIZO NI SEHEMU YA KULITATUA JAMANI...TUBADILIKE!
Pole mdau wa ughaibuni,
ReplyDeleteVipi matukio hayo ya wizi hapo Uwanja wa Ndege, uliyatolea taarifa polisi. Na hao polisi walisema nini?
Nafikiri kuna mambo mengi ya kufanya kuboresha huduma zetu sehemu mbalimbali. Tunaweza kwa kiasi kikubwa kufanikiwa hivyo kwa msaada kiasi fulani wa serikali. Hebu tujaribu kupendekeza njia na gharama nafuu na ambazo hazina utegemezi wa serikali ili kuweza kuondosha matatizo haya,
Mdau wa New York,
ReplyDeleteMara zote ktk maoni yangu tokea mwanzo tumekuwa pamoja mimi na wewe kwa kukuunga mkono.
UKWELI UMETOA NA MARA ZOTE UKWELI UNAUMA''HUDUMA KWA WATEJA KTK TANZANIA IMEOZA KABISA'' there is no country in the world where by ''CUSTOMER SERVICES IS IN COMPLETE DEATH THAN IN TANZANIA''
HOJA ZA MSINGI NI MBILI HAPA CHINI:
1.Huwezi iweka Tanzania ktk ulinganishi wacha na huko kuliko endelea, sema hapa na majirani zetu ZAMBIA,MALAWI,MSUMBIJI,CONGO DRC ukiwa bosi na pesa (MAKUTA, AU DOLARI WANAVYOITA)ndio kabisaa unakaribia kuabudiwa labda mwenyewe ukatae,KENYA,UGANDA,BURUNDI na RWANDA.
2.Tunataka UFANISI/ We need EXCELLENCE!(KWA VILE TUPO KTK USHINDANI NA ULINGANISHI NA MAENEO MENGINE)
HIVYO ILI KUFIKIA LENGO NI LAZIMA TUSHUGHULIKIE MALALAMIKO YOYOTE YALE KWA FAIDA YETU, YEYE ALIKUJA NA MSAFARA WA WAGENI HIVYO TUMEAIBIKA NA KUUMBUKA SAAANA,,, KAMA MDAU WA NEW YORK ANAVYOTUSHUKIA KWA MARA YA PILI SASA!
Mdau wa New york madai yake Mnyamwezi huyu yasipuuzwe!.
ReplyDeleteTunaweza kuja umbuka zaidi, kwa vile mficha MARADHI MAUTI HUMUUMBUA!
Hatuwezi kuendesha mambo kwa kusaidiana saidiana na kuteteana ili kuficha UBOVU!
Mdau wa newyork,baada ya kusoma maoni ya watu nilitegemea ungerudi na the least you could do was kututajia ni benki gani na mbuga ipi ulipopata huduma mbovu...do not generalise please.kama ulivyotaja kunduchi na huduma nzuri,i think its fair we know pia waliotoa bad customer service.
ReplyDeletesomething else,i expected an apology kwa kusema kazi ya bank teller ni ya kipuuzi yet you contradict yourself again na kuiweka katika list ya sekta muhimu za nchi...what a hypocrite.
Mkuu pole sana kwa yaliyokupata,huo ndio ukweli kabisa nilikuwa hapo TZ ktk likizo yangu mwaka jana dec niliyaona hayo bila ubishi,na wakati naondoka niliombwa pesa toka mlangoni mpaka nakaribia kuvuka geti la mwisho, niaibu lazima tukubali haya mambo yapo na ni vema yakaangaliwa kwa maslahi ya nchi.Nakupa pongezi kwa kueleza ukweli kwa urefu.
ReplyDeleteMdau wa DC
NDUGU YANGU POLE SANA! ULIPOANDIKA MALALAMIKO YAKO NILIJUA KABISA NINI KITAFUATA KWA WAOSHA VINYWA WA BONGO! TUNA TATIZO KUBWA SANA SISI WANANCHI WA KAWAIDA NA NAKWAMBIA HII ITATUGHARIMU SANA SOON, HII HADITHI YA AMANI, UTULIVU INA MUDA MFUPI. SISI WENYEWE BADALA YA KULALAMIKA KWA WATAWALA KUMSUPPORT JAMAA ALIYEONA MATATIZO KAZI YETU NI KUMSHAMBULIA. WE ARE SO POOR IN THINKING! TUNAKURUPUKA, TUNAWEKA SIASA NA KUSIFIA MAFISADI. WATU WANAACHA MAMBO YA MSINGI KUHUSU FUTURE YETU WANAKIMBILIA KUSHAMBULIA OOH! UNAONGEA KIINGEREZA, OOH UNA NYODO! WHAT IS THIS? hIVI MNADHANI MTU MZIMA AKAE CHINI KUSINGIZIA MAAFISA UHAMIAJI, WAHUDUMU WA HOTELI ILE IWEJE? KWAMBA KAAMUA TU KUSEMA WAKATI ALIKUTA SERVICES NI ZURI?! CANT WE REASON? KWANI KUNA ALILOSEMA LA UONGO? HATUJUI HUDUMA ZILIVYO MBOVU KILA SEHEMU TANZANIA? HUJAENDA BAA UKAACHA KUHUDUMIWA KISA UMEKUJA NA MWANAMKE? HUJAENDA HOTEL KUBWA UKADHARAULIWA KISA RANGI YAKO? HOW ABOUT OFISI ZA SERIKALI? HAMJUI MATUSI YA NGUONI KWENDE DALADALA? HIVI TUNAJARIBU KUSEMA KWAMBA; HUDUMA NI BORA, WENZETU HUDUMA NI MBAYA KAMA ZETU? SIO KWELI ETI WATZ NI WAKARIMU. SIO KWELI. WE ARE EXTEREMELY POOR-EXTREMELY LOW IN CUSTOMER CARE, KNOWLEDGE, UWEZO WA KUCHAMBUA ISSUES ILA NI MABINGWA WA KULALAMIKA, KUWEKA SIASA MBELE, PERSONALISING ISSUES ETC. BEHOLD WATZ, HII AMANI UCHWARA TUNAICHEZEA KWA UJINGA WETU. CHONGENI MIDOMO LAKINI HUO NDIO UKWELI. KAZI YETU KULALAMIKA WAKENYA WANACHUKUA KAZI ZETU! OF COURSE LAZIMA WACHUKUE! HATA MIMI LEO SIENDI NIKIONA KUNA MKENYA ANATOA HUDUMA VIZURI NI AFADHALI NIONGEZZE HELA NIPATE HUDUMA KWAKE KULIKO MTZ AMBAYE HACHELEWI KUKUZUNGUSHA CHENJI YAKO, KUKUTUKANA, KUKUDHARAU! CHEAP POLITICS IS DESTROYING US!
ReplyDeleteWatz wanasikitisha! na Serikali inaangalia. we fikiria hata hii migomo ya kuuza mafuta ni nini? good customer care and business ethics?! Watz acheni ushabiki simamieni issues na haki
ReplyDeleteNashangaa unapo sema mtu mzima alafu ukatoa malalamiko kwa kebehi na kudharau kazi za watu hapo hapo unataka uhurumiwe aaah wewe inaonyesha ni jeuri sana ndo maana watu walikuwa wanakupotezea na wazungu wako tunawaona sana mnavyo nata mkiwa na wazungu mnajifanya miungu watu.
ReplyDeletePotezea tu.
ACHANA NAOOOOOOOOOOOOOO. BORA UMESHAWAPA UKWELI WAO WAMEZE WATEME WATAJIJUUUUUUUUUUUUU.
ReplyDeleteMimi ninaswali na nipo hapa USA vile vile.
ReplyDeleteMara ngapi umeshakwenda bongo for last 5 years?
Labda ulionekana wa kuibiwa.Bongo ndio tunamatatizo ya customer service,lakini hata inchi hizi za ulaya na Amerika zilipitia matatizo kama haya mpaka soko la ushindani likakshinda.
Mimi pia Nafikiri kuwa jinsi ulivyo wasilisha mada ndio tatizo kubwa kuliko mada yenyewe.
Tanzania tunatatizo la leadership na viongozi wanajua matatizo haya.Ni safarindefu na tutafika tu.Tunashukuru sana kuweza kutoa dukuduku lako kwani viongozi wanasoma hi blog na wamepata haya malalamiko.
Mwisho napenda kusema kuwa,angalia unavyo wasilisha mada yako kwani mara hii ya pili inaeleweka vizuri na kuwa you are frastruated.
Brother unachoongea ni kweli...tatizo ni kwamba Tanzania kuna side money nyingi sana kiasi kwamba hakuna anaejali ajira ile aliyonayo katika taratibu na maadili yake. Nilienda Tanga Hotelini nikaagiza soda ...ikapita kama robo saa...nikamuuliza yule mhudumu...sista vipi mbona nimekuagiza soda muda mrefu..? akanijibu we huoni kama nahudumia watu wengine. kwa kweli sikujiskia vizuri..na imekuawa kama tabia kwa baadhi ya Bars in town kwa sasa ukienda na msichana utapata huduma mbaya vibaya but ukiwa mwenyewe wanakunyenyekea ili kutengeneza mazingira ya kuondoka nae....hii sio sawa...embu kila mmoja pale alipo na nafasi aliyonayo kikazi ajaribu au afanye kama taratibu na maadili ya kazi hiyo then utaona mambo yanavyooka kwa nchi yetu...tunalalamikia serikali hali ni ngumu ila ukichunguza kiundani utagundua pia na sisi tunachangia kwa kiasi fulani... Mtalii akikwazika hapa Tanzania hawezi kumrecomend rafiki yake au ndugu yake aje holiday Tanzania....obviously atamwambia ajaribu nchi ingine ....Mi naongea kwa uzoefu wa hapa hapa ndani ...sikai nje na sijawah enda nje...EMBU TUBADILIKE JAMANI.....KATIKA KUBADILI HII NCHI MAZURI YAKE TWAWEZA TUSIYAONE ILA WATOTO AU WAJUKUU ZETU WAWEZA KUJA KUJIVUNIA MAAMUZI YETU......
ReplyDeleteMengine niliyoyabashiri katika mada yako nayaweka kando, kwani si ya muhimu sana.
ReplyDeleteIla nakubaliana na wewe kuwa sekta ya huduma Tanzania ni choo cha mwendawazimu.
Nilipata wageni kutoka Ulaya mbona nilijuta. Na bahati mbaya jamaa wana mihela kibao ila hawataki sehemu za kifahari sana, hivyo tukitulia kidogo sehemu najihisi nimevuliwa nguo kabisa kwa jinsi huduma zinavyotolewa. Yaani siku walipoondoka nilishukuru sana. Iliniuma sana maana mwaka uliotangulia walinikaribisha nchini kwao na nilliburudika sana. Kibaya zaidi wakawa wanaisifia sana Tanzania kwa yale wanayoyasikia na kuyasoma, ila walikumbana na picha lenyewe ilikuwa ni mshike mshike.
Mdau wa ughaibuni! Kwanza pole sana kwa songombingo uliyoipata hapo kwenye kinachoitwa JKN Airport (Sina hakika kama ina hadhi ya kuitwa international Airport. Ndugu yangu Mdau wa ughaibuni, kwa hali ilivyo, wote wanao kubishia ndiyo hao hao wanaosumbua watu hapo Dar Airport.Ni wepesi wa kuingia humu kwenye blogu na kupinga vikali wakisaidiwa na wakuu wa idara zao hapo uwanjani. Ki ukweli ni wezi na waombaji kiasi cha kutia aibu kama sio kukera. Mimi mwenyewe yalishanikuta mara mbili nikiwa natokea ughaibuni. Kuna watu wengi wanao zurura ndani ya majengo ya airport lengo likiwa ni kusumbua wageni wanao ingia Tz. Kila mmoja anakulazimisha akufanyi hiki au kile, lakini lengo ni kukuibia.
ReplyDeleteMimi mara zote mbili nilizoibiwa, nilipeleka malalamiko yangu kwenye ofisi zinazo husika. Cha kusikitisha mhusika badala ya kukushughulikia kutatua tatizo anakuambia mbona huelekei kuwa na hivyo vitu vilivyo ibiwa! Na hakuna anaye kujali kabisa.
Ukweli ni kwamba hapo uwanjani upo mtandao mahususi kwa ajili ya kuwaibia wageni, na kisha mali zinazoibiwa hugawana na wakubwa zao.
Tunachoomba ni kwamba, tuombe mungu waKenya wajenge uwanja wao ndege pale Taveta/Voi,ukizingatia kwamba tiketi za ndege kwa upande wa Kenya ni rahisi. Halafu tuone kama huo wa Dar si utabaki kupokea ndege za viongozi pekee.
Nawasilisha.
Mdau Ughaibuni.
Unajua unapoona wananchi wa kawaida kwa wingi wao wanafanya makosa kila kona ujue hata kule juu ni tatizo kubwa. Usidanganyike na suti na magari yanayotukana hali ya nchi na wananchi wake.
ReplyDeleteKwa mfano unaposema mashushushu wapelekwe JKN Airport kuchunguza, huwezi amini kuwa hao walioko huko ni mashushushu ila wameacha kufanya kilichowapeleka na wamepageuza dili.
Kaka umenena, tz kuna uzembe maeneo mengi sana. Ninachokuomba usikatishwe tamaa na watoa maoni maana kwa walio wengi hapa Bongo kusafiri kwa ndege hata zile za kwenda mikoani ni issue, ndo maana kuna mtu anaweza kaa Bongo hata miaka mitano hajawahi kwenda Airport, ikitokea bahati nzuri anakwenda huko ni pale anapomsindikiza ndugu au jamaa anyekuja majuu, na kumbuka huwezi ingia ndani, kwa hiyo unaweza kujikuta unabishana na mtu ambaye tangu kazaliwa hayajui mazingira ya ndani ya eaport ya Bongo. Kaka usikate tamaa kama kuna tatizo uwe unalitoa itasaidia sana, maana hapa Bongo watu wanafanya kazi kwa mazoea.
ReplyDeletekaterero73@gmail.com
uliyoyasema kaka ni swadakta bila ubishi abishae na abishe airport ni wizi mtupu wanakuzuga na kukufungulia kibegi kisailence ukifika uendako ndani ya kibegi kuna mapungufu wakati uliweka ulichoweka kiuhakika. habari ndio ndio hiyo ndugu zangu waTZ. tukubaliane na ukweli,yapooooo.
ReplyDeleteI agree with you Brother, Kuna uzembe mwingi sana sana kwenye Airport zetu, ni Aibu sana. Tusifumbie macho mambo kama haya we need to change
ReplyDeleteMdau umesomeka,Tatizo sio kwamba hakuna hayo uliyoyasema ni kweli yapo sehemu kwa sehemu.Our concern hapa ni kwamba unawezaje kuita kazi za watanzania wenzio ni za kijinga?Hivi kazi ya kijinga ikoje labda utufafanulie ili tuelewe.Maana sisi hata kazi yako ya kuzibua vyoo huko ulipo tunaithamini na kuipenda na wala hatuoni ya kijinga.Issue hapa ni kwamba umeleta dharau kwa wabongo,Kwa taarifa yako mtanzania ni bora afe na njaa kuliko kumlamba miguu mwenye vijisenti kama wewe.
ReplyDeleteKama unajivunia utanzania na kiswahili mbona umechanganya na lugha ya kikoloni?akili ya ukoloni haijakutoka wewe, endelea kubeba boksi.
ReplyDeleteCustomer care ilikufa tulikumbatia sera za ujamaa, unajua chini ya hii sera hakuna alie juu wala chini "KINADHARIA"... sasa in late 60's and 70's Watanzania walikolea hii sera... Mbona sasaiv kuna afadhali... in those days watalii walikua wanalala chini, eti.. "nani amtandikie godoro mkoloni" ... Sasaivi hali ni mbaya kwavile for the past one generation Customer care was not OUR CULTURE.... sasa kama kizazi kilichotutangulia hakiku-Practice customer care... sisi watoto wa 80's tuta-practice vipi??? mimi hili neno customer care nimelisikia wakati Mobile Phone companies zilipoanza hapa Tanzania... Well na Yote haya Mabaya hapa Tanzania hayataisha iwapo Culture Mbovu Mbovu zilizoletwa na sera Hovyo Hovyo za huko nyuma hazitakanwa HADHARANI na WATANZANIA kuombwa msamaha kwa kupotoshwa na HAO walioleta na kuzi-propagate hizo sera...
ReplyDeleteTRA "Tafuta Rushwa Asubuhi" inafanya kazi zake katika misingi SAHIHI ya "MFANYABIASHARA NI KUPE" Huu ndio wimbo sisi CHIPIKIZI tulikua tunauimba kila siku shuleni... U-communist... Hapa kwetu CHUKI dhidi ya WAFANYABIASHARA ilianza at STATE level... so as long as its' the same STATE's men who were against "Businessmen -hood, No Good to Business can happen...
Kaka yangu pole. Achana na wabongo kaka, we ujiulizi kwanini vigogo wengi wanajifanyia mambo yao wanavyotaka kwasababu wanajua watanzania wengi ni mbumbumbu mzungu wa leli hawaelezeki kabisa na wala hawashauriki, watakalia hivyo hivyo tu kazi ni kulalamikia serikali wakati wenyewe hawataki kukosolewa. Na ukiangalia wale wote waliochangia negative ndio hao wanaovalia masuluari matakoni (bongo fleva, sisi tuko hapa bongo tunawajua mtu mwenye busara zake hawezi kubisha kuhusu hilo ulilolileta hapa. Huduma kwa ujumla tanzania ni poor.
ReplyDeleteSikia mtanzania mwenzangu, mtu anapokuambia jambo juu ya mahali popote jua ni mwenyeji wa hapo na mara kwa mara hutembelea eneo hilo. Usidhani mara yangu ya mwisho kusafiri nje ya Tanzania ni Januari mwaka huu, hapana. Mimi ni msafiri mzuri tu nje ya Tanzania na hilo eneo la uhamiaji airport Dar nalifahamu. Uzembe ni wako, kwanza ulikuwa na wageni ambao ni mara ya kwanza kuingia Bongo kwa nini hukukaa nao eneo moja, pili baada ya mkwe wako kuibiwa ulitoa taarifa kwa wahusika ama umeishia kuja toa lawama huku kwenye michuzi blog? Hii ya Benki bado nakataa, hakuna watumishi wa namna hiyo tena Tanzania. Na kama kweli ulitendewa hivyo ungeripoti mara moja kwa branch manager uone kama muhusika hakuchukuliwa hatua za nidhamu.
ReplyDeleteKuambiwa kufungua mizigo yako na wengine kuachwa ni utaratibu wa kawaida tu wa usalama. Si wote ambao hufunguliwa mizigo ila wanafanya kushitukizia, labda baada ya kupita watu kama 10 hivi wa 11 anachekiwa mizigo. Pili yawezekana scanner iliona kitu ambacho hakikueleweka vizuri ndiyo wakataka wakione na macho kuhakikisha ni nini na kama ni kitu salama kuingia kwenye ndege. Yaelekea umekuja Tz na mawazo hasi kwa hiyo jambo dogo tu ukifanyiwa ambalo ukilifikiria kwa kina utaona linaleta maana unaanza ona TZ haifai. TUBADILISHE UELEWA WETU JUU YA NCHI YETU
Preach!
ReplyDeleteMhh, wewe umongea vya maana vitupu. Yako madudu mengi nchini kwetu wengi tunaona uvivu tu kuviandika. Unaenda polisi unasema umegongwa na gari wanaandika report na kuchukua namba ya gari ukimaliza unaambiwa ukiliona hilo gari utoe taarifa polisi. Sasa kama huyu polisi ya mapokezi ndiyo anakwambia hivyo wakuu wao wako wapi? Serikali itoe namba za simu ambazo zitatumika kutoa taarifa kuhusu madudu yanayotokea sehemu mbalimbali na wawepo watendaji, hii nayo si ni ajira na niajira inayosaidia kuendelea kwa nchi?Degelavita.
ReplyDeleteHAWA WANAMTANDAO WA UZEMBE WANAOBISHA DHIDI YA MADAI YA MDAU WA NEW YORK ''MNYAMWEZI'' ALIYEKUJA NA MSAFARA WAKE WA WAGENI WAKIWA NA DOLLA ZAO KULA SIKUKUU,
ReplyDeleteANAYEBISHA AJARIBU KUAKISI AKILI NA FIKRA ZAKE KTK MADIRISHA YA HUDUMA ZA TAASISI ZETU KAMA HIZI:
-TRA( NDIO KWANZA IMEANIKWA HUMU LEO)
-MABENKI
-HUDUMA ZA KISERIKALI
-HUDUMA MBALIMBALI ZA WATEJA
NA KWINGINEKO!
-RUSHWA ,KIBURI, DHARAU NYODO NA UZEMBE HADI MOCHWARI JAMANI?
HIVI HATUMA AIBU TUNASHUPAA NA KUTOKWA NA MISHIPA YA SHINGO KUTETEA UCHAFU?
UNAWEZA KUMKUTA MTU AMELEWA CHAKARI UKAMWAMBIA NDUGU YANGU UMELEWA UMEZIDIWA NA POMBE NIKUSAIDIE NIKUPELEKE NYUMBANI UKAPUMZIKE,,,YEYE MLEVI AKAKATAA AKASEMA SIJALEWA KABISAAA!!!
HIVI WA TANZANIA TUNA AKILI KWELI?
Nakuunga mkono kwa yote uliyoyaandika, hayi ya nyuma sikuyaona. Ila nina swali moja kwako kaka: Kwa nini umechanganya lugha? Wakati mwingine tumia kiswahili fasaha bila kuchanganya itaongeza uzito katika madai yako ya kuwa Mtanzania ambaye hujazuzuliwa na kukaa nje ya nchi. Ubarikiwe!
ReplyDeleteUBOVU WA HUDUMA KWA WATEJA TANZANIA:
ReplyDeleteKinacho tukwamisha ni mambo haya:
1.TANZANIA NDIO NCHI YA PEKEE DUNIANI AMBAYO KIGEZO CHA KAZI HIYO NI KUWA MWANAMKE MWENYE UZURI WA SURA NA UMBILE, KAMA MAKALIO MAKUBWA HIVI! (Vigezo vingine havizingatiwi na havina umuhimu kabisa!)
2.WENGI ELIMU YAO NI MGOGORO,KIINGEREZA CHA KUBABAISHA!,,,NA WENGI WANAINGIA KTK NAFASI HIZO KWA KUGHUSHI VYETI!
3.WANAPATA WENGINE KWA KUPITIA RUSHWA ZA FEDHA NA NGONO,,,KUFIKIA KULAWITIWA!
4.WENGINE WANAPATA NAFASI KWA NJIA ZA USHIRIKINA (HAWA MADADA NI WACHAWI SANA ,NDIO MAANA WAKUBWA WAO WANAJUA HAYA LAKINI WAMEWAFUNGA KWA UCHAWI HAWASEMI)!
SASA WANDUGU, UNAMKUTA MTU ELIMU YAKE YA WASIWASI HANA UJUZI NA KAZI HIYO HALAFU YUPO HAPO SEHEMU NZITO KABISA, AMEFIKA VIPI?
KWA KUWA AMEPATA KWA NJIA ZA AJABU AJABU NAFASI BILA SIFA HUSIKA LAZIMA ATAKUWA ANA BABAIKA NA ANAKUWA LIMBUKENI NA NDIO MWANZO WA YOTE HAYA!!!!!!
Ndugu nakupongeza kwa kueleza ukweli wa uliyoyaona.Mimi nafikiri wahusika wachukue hatua maana inaonekana wapo wtalii wengi wanaofanyiwa hivyo lakini kwa kuwa hakuna sehemu ya kueleza dukuduku zao hakuna anejua kinachoendelea.
ReplyDeleteKama tuna uzalendo na nchi yetu kweli lazima tuwe wakweli pasipo kuficha, taasisi nyingi hasa za serikali hawajui kumjali mteja!!
1.siku nyingine punguza jazba ndio utoe maoni yako,
ReplyDelete2.wewe umeandika lugha ngapi?
3.Hao watu unao watetea kwenda kwao ni mbinde,nahata ukifanikiwa utanyanyaswa zaidi ya mbwa.
sikiliza babu,kama unaona bongo hauiwezi,tuachie wenyewe sio unaropoka tu,kiswahili chenyewe hujui,ny@ng´afu!.
Du umejieleza vema, umenigusa sana kwani ni ukweli mtupu uloongea, tulikurupuka kukushambulia bure.
ReplyDeleteMbona unajishitukia. Unakaa unaongea mambo ya Bongo Fleva tuuuu, hayo yanakuhusu nini? Kama una malalamiko yako sema, lakini hauhitaji kujilinganisha na tabia ya mtu mwingine. Unaongekama uko insecure sana.
ReplyDeleteHayo malalamiko yako watu wengi wameyasema na kuyaandika sana hata humu kwa michuzi, suala ni watanzania kama wewe unayejua kipi bora, unafanya nini kubadilisha hali? Najua inauma sana kudhalilishwa na kunyanyaswa ndani ya nchi yako, hasa ukiona wageni wanapeta tu, lakini malalamiko hayawezi kubadilisha kitu. Kila la heri.
Huyu mheshimiwa ameeleza aliyoyaona akiwa Tanzania na ni kweli kuna lugha mbaya aliyotumia. Yeye siyo Mungu , inawezekana ni hasira ya kutohudumiwa ambayo inaweza kumpata mtu yeyote. Ni kweli ndugu zangu Watanzania nchi yetu imeoza, mtu anaajiriwa na analipwa mshahara lakini hathamini kazi yake. Ukitaka huduma mpaka upenyeze bakshish (rushwa). Tabia hii imejengeka karibu kila sehemu inayotoa huduma. Ni kweli kabisa pale uwanja wa ndege mtanzania anapekuliwa isivyo kawaida lakini akija mtu ambaye siyo mweusi haulizwi chochote anapita tu. Nilishangaa siku moja anakwenda China na hati ya kusafiria ya kibalozi anazuiwa kucheck-in eti hana viza. Tanzania na China zimeondoleana viza kwa passport za kibalozi(diplomatic passport) na za watumishi wa serikali (service passport). Sasa kama mtu anafanya kazi hapo uwanja wa ndege na hajui taratibu inamaanisha nini? Hili ni tatizo ambalo tunatakiwa kulikubali na ukikubali tatizo basi unakuwa umeelekea kwenye ufumbuzi wa tatizo. Ikumbukwe kuwa hapo uwanja wa ndege kuna abiria mmoja aliwahi kukamatwa na pembe za ndovu kwenye mzigo uliopitishwa kwenye hizo "scanner" za Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere. Kama watu wangekuwa waaminifu hizo scanner zisingetambua kilichomo katika mzigo huo? Hiyo ni picha tosha kuwa Tanzania imeoza kwa rushwa. Na huyo aliyeufichua inawezekana hakuwa ameshirikishwa kwenye mchakato mzima. Watanzania wengi bado hatuthamini kazi na ndiyo maana inashindikana kuendelea kama nchi. Tunachothamini ni ujanja wa kupata fedha za haraka haraka hata kama ni kwa njia haramu. Mfano mdogo una daladala mpe dereva. Hata kama gari lina matatizo yeye anachojali ni kupata fedha; likiharibika atakwenda sehemu nyingine kutafuta kazi. Hana shida leseni anayo. Ni vyema tukaelewa kuwa kuna tatizo nchini na hapo ufumbuzi wa tatizo unaweza kupatikana. Baadhi tunageuza sehemu ya kazi kama kijiwe cha kupigia story. Huyu bwana alichosema ni ukweli aliouona yeye. Baadhi walisema kuwa kama meneja ni Mkenya ni dhahiri ataajiri Wakenya wenzake. Sawa hebu tujiulize kama hiyo nafasi ya meneja ilistahili Mtanzania ni kwa nini hakuajiriwa na serikali imechukua hatua gani? Kwani mwekezaji anapokuja kuwekeza nchini kuna taratibu zake katika nafasi za ajira na masharti ya uwekezaji. Katika utandawazi ni dhahiri Tanzania itaachwa nyuma kwa sababu kwanza mfumo wa elimu umedumaa. Elimu inayotolewa in walakini. Tumeshuhudia mwaka huu wanafunzi wa shule za msingi zaidi ya 9,000 wakifutiwa matokeo na waliohusika na matokeo mabovu wakiachwa waendelee kutesa wakati wanafunzi wanateseka. Kwa elimu ya kupeana majibu ya mitihani hatutafika kamwe. Tanzania wapo watu waliokuja kama watalii lakini walipomaliza kutalii wamefungua maduka Kariakoo wanauza maua, karanga, vitasa n.k. Je serikali haiwaoni? Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka ya mtu kufanya atakalo na asiulizwe? Je ni nani anawapa kibali cha kuendelea kuishi nchini kama siyo Idara ya Uhamiaji? Au ndiyo shamba la bibi? Ugonjwa huu ndiyo unapelekea kila sehemu ya huduma kuoza. Tubadilike tuache jazba au la sivyo katika hiyo EAC tutabaki kulalamika kuwa Wakenya wanachukua nafasi zetu. Huyu bwana wa Marekani ameeleza matatizo aliyokumbana nayo, pamoja na lugha aliyotumia kutowafurahisha wengi lakini tukubali kuwa Tanzania kuna matatizo.Tusiwe kama yule mfalme aliyepita mbele ya watu wake akiwa uchi na watu wakawa wanamshangilia tu wanaogopa kumwambia mfalme yupo utupu mpaka mtoto mmoja alipopiga kelele na kusema mfalme hakuvaa nguo. Tubadilike tuwe wakweli na tuukubali ukweli.
ReplyDeletemtoa maoni BARAKA nimefurahi umeweza kutoa maana halisi ya TRA, kinadharia na kimatendo.
ReplyDeleteni kweli kwao kila mwenye kipato ni kupe na mwizi mkubwa kwa hiyo wao lazima wamkamue hata ikibidi kuuwa chanzo halali cha mapato yake bila kujali kuwa hata wao watakosa mapato (ushuru) kutoka chanzo hicho
Kwa kifupi ndugu zangu kweli TANGANYIKA ni nchi yetu nzuri tuna kila sababu ya kujidai ila serikali ndio ndio imeifanya nchi iwe hivyo kwa hiyo sisi tutalaumiana tu muhimu viongozi tuliowachagua waamke ili wawe ktk ubora wa kiserikali kama nchi nyengine DUNIANI hakuna kingine zaidi ya hicho mungu ibariki TANGANYIKA 50 YA UHURU waache porojo viongozi wawenwachapakazi.
ReplyDeleteWadau msiwe kama vile mmekuja TZ leo, benki zote za biashara Bongo hazimilikiwi na serikali na ushindani katika sekta hii ni mkubwa sana. Uzembe na utovu wa maandili hakuna hata benki moja inayoruhusu kwa kuwa kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi lake enyewe. Nakataa na nitaendelea kukataa aliyosema juu ya benki. Kama ana ukweli aitaje hyo benki. Huenda ikawa alishindwa timiza masharti/wasilisha makaratasi yaliyotakiwa ali dolari zake zinunuliwe. Tumezoea fanya mambo kwa njia za mkato inapofika unaambiwa fuata njia iliyonyooka unaona unatendewa sivyo. Acheni hizo
ReplyDeleteFri Dec 30, 10:26:00 AM 2011
ReplyDeleteKIPENGELE NAMBA 4 USHIRIKINA SIKUBALIANI NA WEWE ACHANA NA IMANI POTOFU.
We bwana wacha kuchanganya watu , bongo kila baada ya miezi miwili watu tunakwenda kuenjoy japo for a weekend unakamata BA alhamisi tunaingia pale ijumaa asubuhi watu tunakula bata jumapili asubuhi tunakamata pipa jioni tuko makwetu LONDON na jumatatu kazinini kama kawaida. Jilaumu wewe wa kutokwenda marakwamara. Alafu kama kweli ungekuwa msomi wewe ungemtafuta meneja wa airport au mkuu wa polisi palepale airport mara ulipogundua umeibiwa wangeangalia CCTV mbona wangewakamata tu hao wezi BABAA,Wewe bwana hukuibiwa mule ndani mimi nafikiri hivyo vitu umesahau sehemu. Fanya juu chini watu wakaangalie CCTV siku uliyofika jibu litapatikana. Sikatai pale pana problem ipo tena kubwa haswa OMBAOMBA WAPO SANA,tena wale security watakuganda weee kaka niachie chochote. Kuhusu wale potters mjomba mbona wapo na uniform wanazo pale ndani mi nahissi wale ndio wamekuchapa mzigo wako tena sio ndani ni nje maana wako very sharp. ILA KIUKWELI PALE PANA MATATIZO NA HAYO MATATIZO HUYAKUTI KENYA WALA UGANDA. Kama mtualiweza kuingia na BASTOLA KWENY NDEGE YA EMIRATES BILA KUSTUKIWA INAONESHA NI JINSSI GANI UTAWALA ULIVOMBOVU. POLE SANA JOMBAA.
ReplyDeleteTanzania nafikri ndio tunaanza kupata uhuru sasa maana matatizo yote yanayosemwa nimeyapata na ni kweli tupu kwanza watu hawana utaratibu wa kusheshimu kazi na badala yake wanaleta dharau kazini,mimi nilipokuwa dar nilitumiwa pesa kupitia western union na nilipokwenda bank ya posta mle ndani muhusumu alikuwa busy kuzungumza na rafiki yake kuhusu kuku anaofuga na kuacha wateja tumesimama nilipotaka kuongea na menager kwa bahati nzuri alikuja then hakuna kitu alisema ,uhamuzi niliochukua ni kuchukua ID yangu na kisha kuondoka,baada ya majengo matatu kulikuwa na bank binafsi na wanatoa huduma kama zile nilihudumiwa within 5 min.Utakuta polisi traffic yuko katikati ya barabara kisha anapokea simu?kwel kuna Ethic ya kazi hapo?nilifika duka mooja dar liko katika ya mji nikakuta wana kibali fake cha biashara na kina mihuri na sign zote za TRA sishangai kuona hayo yote ila hatuwezi kufika mbali kama kweli tunahitaji maendeleo na wahusika wanayajua ila wanafumba macho.Kwa fact polisi wa dar (traffic)wana sindicate ya kila sku na RTO anapokea 10m per day toka kila traffic aliyeko kazini kisha anapewa mmoja,ndio maana siku hizi wako barabarani na magari yao.Sio kwamba mwema hajui bali ni utaratibu wao ukigoma kuchangia upati hiyo pesa then unapelekwa ngara huko kuwa mlinzi,kwa njaa zako utachangia tu.Usalama wa taifa umejaa watoto wa wakubwa sijui wapi hii nchi inakwenda.Nina mengi ila hayo machache kwa leo na tusipobadilika we are done n dust.
ReplyDeleteHuyu Bwana vipi???? kwa taarifa yako Tanzania ni mojawapo za kiafrika zinazoenda kwa kasi sana kimaendeleo ikiwemo cuostomer services, na ndio maana watu dunia nzima wanakimbilia TZ siku hizi hata Airport kuna msongamano wa ndege, uwanja hautoshi. Wewe umeng'ang'ana huko N/york umechelewa sana. Mbona huku Ulaya na wao wanatudharau sana na wakati mwingine wanatuibia????? Mfano sasa hivi Uingereza inabidi irudishe change ya rada ambayo wao walijua kabisa wanatuibia.
ReplyDeleteNdugu zanguni mlioko ughaibuni lazima muwe makini sana. Babu zetu zamani waliuza utu wao na nchi kwa pelemende (pipi), shnga n.k. Leo hii wazungu wanakuja na gear mpya, unapewa penzi kama entry point ya kuja bongo kufanya research. Hiyo research yako itamsaidia nani??? Mzungu au Mtanzania??? Hata kama umesomeshwa na mzungu ndio mikakati yao ili baadae uje uize TZ. Usifikiri walichokufanyia ni ukarimu, ni yale yale ya kupewa pipi na shanga na wazungu.
ReplyDeletewatanzania kizazi kilichopo ni cha mkulima,mfanyakazi choka mbaya sana,na hao wengi wao wapo maofisi nyeti.kwa kifupi itachukua karne moja kwa waTanzania kuwa pamoja na dunia ya sasa.Tanzania bado nchi changa sana na watu wake ni wachanga kimawazo hilo halina ubishi.cha muhimu ni kusaidia siyo kuwa na hasira na nchi hii.Miradi iwe ya kusaidia utaeleweka.
ReplyDeleteTatizo la waTz. ni kujifanya wajuaji! Sio siri Tz tuna matatizo tena makubwa tu, tunatia aibu kwenye customer services na huduma zingine zote. Nyie mnaopiga midomo hamjawahi hata kutoka nje ya Tz mnasikia story za nchi za nje tu na mnazibeba kama zilivyo. Ukweli ni kuwa nchi za wenzetu custumer care ipo juu sana, wala hutajutia kama kwetu. Tubadilike waTz jamani, Kenya, Botswana, SA, Angola, Namibia etc zinatushinda. Imagine Rwanda juzi tu tuliwasaidia wakati wa vita, ebu angalie walivyotuacha kwa mbali kwenye kila kitu! Tubadilike tuache majungu na kusema hovyo, ni lini na sisi tutakuwa mfano bora?
ReplyDeleteKwa kiasi kikubwa ni Serikali yetu mbovu ndiyo inayopelekea yote haya. Serikali legelege na ya wizi ndiyo inayotupelekea hapa tulipo. Serikali isiyokemea maovu ndiyo hii inayotutesa. Tunahitaji Serikali iliyo bora, imara, yenye maamuzi na siyo hii tuliyonayo! Mungu atusaidie tuje kuipata serikali ambayo siku moja itatuondoa kwenye hii hali ya sasa na kutuonyesha njia iliyo njema na tukubalike kimataifa. Tunatia aibu sana, sana. Sisi tulio huku s'times unaona hata aibu kusema kuwa tunatokea nchi ya Tanzania!
waosha vinywa hoyeeeeeee mtu katoa lalamiko lake wengine mnampinga waone sura zao tz imeoza kila idara hamtaki sasa,nilijua tuu lazma kuna watu watapinga migitu mingine ndio maana mnaonewa nchi imejaa mafisadi tele kisa amani utulivu nyokoooooooo
ReplyDeletebongo sucks mim nakubaliana na wewe..last summer nilikuja bongo,likanikuta hilo hilo,fungua mzigo,nikawaambia unadhani hii ndo first airport mim kudrop by,fungu then mtafunga km mlivyoukuta maana sijafika jk hapa sio kwetu,walinywea na hawakufungua mzigo wa box wa bag,airport haina hata camera mpaka mfungue mizigo ya watu tena watz na wazungu no,ujinga mkubwa
ReplyDeleteJamani achane kelele hasa nyinyi watu wa ughaibuni. Kama kweli ni wasomi mngelikuwa na uwelewa zaidi. Kuna kitu kinaitwa "Utamaduni". "Utamaduni" wa TZ ni tafauti na tamaduni za "Ughaibuni". Huwezi kuamini lakini nipo hapa UK nimekwenda supermarket inaitwa "Tesco" wameniibia chenji yangu. Nilitoa pesa noti ya £20 niliporudishiwa chenji sikuhesabu nilipofika nyumbani naangalia £1 moja imepungua. Mara nyengine nilipokwenda nikahesabu chenji nikagundua jamaa amenifanyia tena £1 kasoro nikamuonyesha kwamba pesa alizoniriudishia zimepungua. Ninachotaka kusema wizi kila pahala upo. Utamaduni wa mTZ akichekewa na mfanyakazi hufikiri yule mfanyakazi anamtaka kwa ngono. Ughaibuni kuchekewa ni moja ya kazi ya mhudumu. Mzungu yeyote aliyesoma hashangai hayo mambo ya bongo maana anajua utamaduni ni tafauti.
ReplyDeleteMwenzangu aliibiwa laptop hapo JKNIA wakati anapita kuelekea kwengineko. Lisemwalo lipo ubushi wa nini wa bongo mabungo?
ReplyDeleteMdau Anonymous Fri Dec 30, 09:43:00 AM 2011, wewe ni mfanyakazi wa airport ndio maana unatetea ujinga. Kubalini ukweli watanazania, itatusaidia kubadili inchi. na anonymous Fri Dec 30, 02:00:00 PM 2011, airport kuna msomangamano wa ndege!!, ungekuwa sahihi kusema airport yetu ni ndogo. Hebu toa takwimu ya tanzania kuendelea kwa kasi kimaendeleo hasa customer service, usipayuke tuuu!!
ReplyDeleteMnapoteza muda tu hapa binafsi yangu tatitizo si yale aliyolalamika kilichokera ni kudharau kazi za benki kuwa makarani hawana lolote. hivi umewahi kujiuliza kama duniani watu wote mgekuwa waliimu nani angefanya kazi nyinmgine! au wote mgekuwa wahandisi nani angekuwa mfanyakazi wa sector nyingine! hatukatai kuwa matatizo hayapo bali yapo sana na mengine ya kuudhi ila kila mahali yapo. hata huku nje tunapoishi kusoma ama kufanya kazi kuna mauozo mengi tu ila kwa kiwango chao na si sahihi kulinganisha yale unayoyaona huku ughaibuni basi ukishuka tu mwalimu nyerere utegemee kuyaona ni kosa kubwa. mambo haya yanaenda na hatua ya maendeleo pamoja na utamaduni ambao huwezi ubadili kwa usiku mmoja. unazungumzia huduma ambazo unazipata ukiwa NewYork, London,Paris ama Tokyo kisha unataka kufanannisha na DSM! maajabu haya. hizi ni nchi tofauti kabisa kimaendeleo nyingine zina miaka zaidi ya 200 baada ya uhuru wakati wewe ya kwako ina miaka 50 ya kusinziasinzia. naungana na mlalamikaji juu ya huduma mbovu alizopata ila sikubaliani na jinsi alivyokashifu kazi za bank, ni matusi makubwa, mtu anayefanyakazi Benki huwezi mfananisha na mtu anayenawisha wazee Newyork, kupiga deki vyoo london au kuchuma nyanya Netherlands. kweli huduma mbovu na zinaudhi ila tafadhali siku nyingine tumia lugha nzuri kutoa kero yako vinginevyo unatuchefua tu.
ReplyDeleteWewe unatafuta audience. Matatizo iyosema ni common kwa poor countries, si tanzania tu! Nilikwenda cuba kuna frustration nyingi kama mtalii labda kuliko tanzania. Kenya watakuhudumia vizuri lakini hawana UTU, watakuuwa na kuiba fedha zako zote - tanzania hatuuwi. Kama uko marekani nasikitika kusema uwelewa wako wa dunia na realities mbali mbali bado ni finyu sana. Labda nisisitize tena point yangu - TANZANIA INAONGOZA KWA UTU SI CLIENT SERVICE NA KUABUDU HELA.
ReplyDeleteKaka Mtoa mada uko sahihi kabisa, wabongo ni wajuaji hawataki kukosolewa ndo maana hatuelendei na utajiri wa rasilimali tulizonazo tunajua sana kutetea maovu kuliko kukubali nakujirekebisha, tunapenda kula bila kutoa jasho mwisho wa siku itatutokea puan, wewe umekuja mara moja ukayaona hayo sisi tunaeishi huku yanatukera sana inafikia hatua UKIPEWA HUDUMA NZURI UNASHANGAA WAKATI NI WAJIBU WAKO
ReplyDeleteMdau hao waliokuponda baada ya kusema ukweli ni kuwa uligusa maeneo yao but ki-ukweli Customer Care TZ iko mahututio.Niko Moshi jana nilikwenda kununua chips pub ili nipeleke home na kulikuwa na mvua inanyesha,nilipofika nilikuta kuna watu wawili wamesimama pia bila kujua kama ni wateja au la..Nikamuuluza mchoma chips kuwa itachukua muda mrefu kupata chips?Jibu alilooa ndo liliniacha hoi kabisaa coz alisema ''Hatuuzi chips kwa watu wenye haraka'' the answer iliyokuwa irrelevant completely nikammwagia mitusi yangu hapo nikichanganya na frustration za ukta new year hii.
ReplyDeleteKAKA MAMBO YOTE ULIYOYAONGLEA NI UKWELI MTUPU. 80% YA WATANZANIA HAWAJUI CUSTOMER SERVICE NI NINI, SO THEY WOULDN'T EXPECT IT FROM ANYONE. ONE NEEDS TO TRAVEL AND SEE HOW PEOPLE LIVE IN OTHER COUNTRIES TO KNOW WHAT YOU ARE TALKING ABOUT. BILA HIVYO, HAKUNA KITAKACHOSAIDIA. EVEN IF YOU TRY TO BE CONSTRUCTIVE, THEY JUST BRING YOU DOWN WITH THEIR NAIVETY. BUT SLOWLY PEOPLE ARE WAKING UP. IT'S GONNA TAKE TIME THOUGH! MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteThis guy is back again, as I said the other day he is a a braggart, a sook and - after all he lives in NY. For gawd's sake he should grow up and man up, He knows he did tough without his make-up kit and foot massager. He is the most metrosexual Tanzanian ever exported to the to USA. Thanks God for that!!!!! I bet he does not know even to change a car tyre,
ReplyDeleteKwanza kaka hongera kwa kusema kweli. Anaebisha ni mzushi tu na hana lolote, tena inawezekana ndo walewale wanaopenda mambo ya shortcut na kupenda maisha rahisi bila kuwajibika! huduma kwenye bank zetu ni mbovu hakuna haja ya kubisha labda uwe una ugonjwa wa kubisha tu, uwanja wa ndege kweli kabisa wahudumu huwa hawakagui mizigo ya wazungu mara nyingi! hata kwenye baadhi ya hoteli ukienda mbongo umevaa kandambili unaweza kuzuiwa ila mzungu akaingia! huduma mbovu sehemu kibao tu hasa taasisi za serikali, watu wanatengeneza mazingira ya rushwa tu! KAKA ACHANA NA WAPUUZI WASIOKUBALI UKWELI! UJUMBE UMEFIKA NA WANAJIFANYA KUBISHA KWA SABABU NI WATU WA AINA HIYO!
ReplyDeletenafurahia jinsi watz tulivyo na hasira naupumbavu! hizo ndo hatua za kuelekea kwny maendeleo..tukaze buti. Tutafika.
ReplyDeleteWafanyakazi wa JKN Airport lazima wawe wezi, mishahara yao midogo sana kwa kweli, huku management wakijilipa mishahara mikubwa wao na watu wao wa karibu. Watu badala ya kusema yanayowasibu wanakaa kumbishia huyu baba wa watu. Jamani hapo JKN kuna matatizo makubwa sana na wizi lazima uwepo kwa sababu hao wafanyakazi hawana mikataba ya kudumu, hawana uhakika na ajira yao kama kesho watakuwepo au la, na huto tumshahara twa kima cha chini kinachotosha nauli tu na lunch.
ReplyDeleteKingine cha aibu kubwa hapo JKN ni wizi ndani ya ndege za watu, ndege zikitua tu mteja kama kasahau kitu ujue kimeondoka. Huko kwenye mizigo ya watu inayosafirishwa nje ndio usiseme watu wanaiba mpaka njegere na mboga mboga nyingine yaani nourmerr acheni tuweke wazi hapa kwenye HALL OF SHAME! MICHUZI HEBU ANZISHA HICHO KIPENGELE CHA HALL OF SHAME au mikingamo watu tuwe tunamwaga data humu, yaani ni aibu tupu JKN airport. Hilo la kuomba pesa ndio usiseme yaani kama wale chokoraa za Kisutu na Indira Gandhi, naomba, naomba! Halafu watu wanakuja kulia lia hapa eti wamedharau, you need to earn that respect kama unafanya madudu lazima udharauliwe eti, na mtadharauliwa sana kwa kuomba omba watu pesa na kutotimiza wajibu wenu!!Shame on you!!
Hapo JKN inabidi huyo TEMU aondolewe maana keshaatamia mayai yake hapo ana miradi kibao sijui mataxi sijui nini badala ya kuendesha uwanja, piga chini weka benchi weka mtu mwingine mpaka akija kutaga na kuatamia siku zimeshaenda, kama TRA vile vile unapiga chini management kila mkataba unapoisha watu waajiriwe kwa contract na itaendelea kwa kutegemea performance zao kama kuna public outcry unapiga chini weka wengine! Vijana wengi wako nje wamesoma wakiitwa kuja kufanya kazi watarudi sio hao wajima kila mtu wanamuona bepari!!
Naku support mpaka kule mdau wa ughaibuni, hata mie huwa nashangaa mno na u "customer services" wa bongo. Niko UK sasa kwa miaka 15. Kila mwaka naendas mara 2 au 3. Na kasheshe unazozipata ni sawasawa ninazokumbana nazo. Kuanza ardhi kulipia viwanja, utasikia mie sipokei hela, nafanya tathmini tu?! Huyo anayekuambia ana kila kitu pale, PC, vitabu vya risiti na kila kitu, tun a ukiritimba wa ajabu! Ukienda benki, labda kuchukuwa hela, ku "activate" au chochote kile, unaweza hata kuumwa, wale staff wa mabenki, wanajifanya wako busy for nothing, mpaka najiuliza sasa waliomba kazi ya nini kama hawawezi kuhudumia wateja?! Hapo bado hujaenda TANESCO, kama ni kuomba uletewe umeme, sahau, DAWASCI nao pia wanatisha, kwanza ukiingia tu, utaona mabomba yamekatika kwa nje, maji yanatiririka bila ya wahusika kujali hili wala lile, ukipeleka maombi mapya, nakwambia unaweza kukaa miaka 10 bila kuletewa hayo maji, kwa kisingizio eti bomba la nchi ngapi sijui halipita kwako?! Bado Posta, iwe kuchukua mzigo au kulipia sanduku la posta, yaani ma staff wanaandika pole pole kama wanayo siku nzima ya kukuhudimia wewe tu, hapo bado hawajaitwa kama wana smu, wageni au kwenda kupiga domo tu?! kwenye restaurants labda ndio utategemea kuna ahueni, kwanza ukiingia labda pale tuseme hotel ya jangwani sea breeze, utawaona ma staff wamesimama tu, OK, utatafuta kiti chenye meza ukae, kazi ni pale wanapotakiwa kuja kukuhudumia, kwanza watajifanya hawakuoni, ila utashangaa mzungu akiingia wanamkimbilia kama mungu! Labda watadai hawawahudumii wausi sababu hatutoi "TIP", lakini TIP si discretion ya mteja?! Ukienda baa zetu za kawaida labda kupata nyama choma na bolingo ya hapa na pale, ndio utalia, ukienda kama mdau mmoja alivyosema na mwanamke, ndio huduma hupati ng'o! Ukienda peke yako, utashangaa wakina dada au wakina kaka wamekaa nao vitini, wanakunywa maji au soda huku wakipiga zogo na kucheka kwa nguvu bila woga wa kufukuzwa kazi! Labda umeagiza chakula, kwanza kitachelewa ile mbaya, na kikija, wakati wa kulipa bill balaa, bonge moja la kubambika! Labda wahudumu wameongezea cha juu ili wamalize matatizo yao yote kwako! Kila kitu balaa, barabarani giza tororo, hakuna cha taa wala nini, ukifanya mchezo utaingia kwenye mitaro ya taka na eti maji isiofunikwa! Ukisema utembee kuwa na tahadhari, barabara nyingi hazina kinga, ile ya kufanya gari zisikugonge, kama za Salander, Morocco, Morogoro Rd au Sam Nujoma, ukiwa kwenye hizi barabara utashangaa daladala au taxi imekupitia na kukugonga kule! Na ikaendelea na safari bila kujali! Kila sekta inanuka rushwa, kila taasisi watu wako wako tu, njiani watu wako pole pole tu, zogo kwa sana chini ya miti, zaidi kusifia watu wanaofanya kazi na kuiba kwa sana TRA, TANESCO, WIZARA YA NISHATI, NGO's, na vitengo vyote nyeti! Hawa vijiweni mara nyingi utawasikia wakiwasifia pia ma traffic na majambazi wanaotumia silaha za moto! Hawa wavijiweni wanaamini kushinda maisha yao ni lazima uibe tu au upokee rushwa kwa sana! Nchi yetu ya ajabu sana, yaani........nimechoka...
ReplyDeleteWE MTU WA NY, ATI UMESHUPALIWA UFUNGUE BEGI AIRPORT WAZUNGU WAMEACHWA!!! ACHA USHAMBA WEWE TATIZO NDEGE UMEPANDA ULIPONDOKA HIYO MIAK 25 NA ULIPOKUJA JUZI HUTEMBEI DUNIANI KUJA YANAYOENDELEA. KITENDO ULICHOFANYIWA NI MOJA YA UKAGUZI KAKA KITAALAMU WANAITA RANDOM SEARCH,, INAFANYIKA KILA BAADA YA IDADI FULANI YA WATU KUPITA NA HII NI ALL AIRPORTS WOLD WIDE KAKA. TEMBEA SIO NY NA DAR TU.... UFANHAMU MDOGO ALAFU ATI WAJIDAI KULAUMU... TAMDUNI KAKA UNAVYONEKANA WEWE UNATAMANI UWE MWEUPE, LOL KAKAAAAA!! TEH,TEH KWIKWIIII KALAGABAHOOOO!!!!!!.
ReplyDeleteMDAU UNAJIKANYAGA SAAANA....NA KUMBUKA ELIMU SIO USTAARABU. KUNA WATU WENYE PhD'S LAKINI HAWANA USTAARABU, PIA KUNA WALE WA UPE NA WAMESTAARABIKA.
ReplyDeleteMIMI NIKO CANADA KWA ZAIDI YA MIAKA KUMI NA TANO. NIMESOMA, NNA KAZI YANGU WA MAANA NA NATUMA DOLA MBILI TATU KWA FAMILIA KILA MARA.
TATIZO LENU WABONGO MNAOISHI NJE, MNASAHAU BONGO MLIOIACHA, MNATAKA MKIRUDI BONGO MAMBO YAWE KAMA HUKO MLIKO. KUMBUKENI NI RAHISI KWA MTU MMOJA KUBADILIKA NA INACHUKUA MIONGO KADHAA KWA NCHI KUBADILIKA.
CUSTOMER SERVICE YA TANZANIA HAIJAWAHI KUBADILIKA...IMEKUWA JINSI ILIVYO MIAKA NENDA RUDI...AMBAO TUMETOKA NJE TUME-EXPERIENCE BETTER CUSTOMER SERVICE, THIS DOESN'T MEAN WE SHOULD EXPECT THE SAME IN TANZANIA. WATANZANIA WENGI HAWAJUI "BETTER CUSTOMER SERVICE" NA WAMERIDHIKA NA WALICHONACHO...ITS PART OF THE TRADITION. NA HII NI UKWELI KWENYE MAMBO MENGI SANA, UENDESHAJI, MAOFISINI, HUDUMA ZA AFYA, POLISI, RUSHWA, PORTS...TO LIST A FEW.
MIMI NIKIRUDI NYUMBANI HUWA SINA EXPECTATION YEYOTE ISYOKUWA REALISTIC. NIMEKULIA BONGO NA NIKITUA TU PALE AIRPORT, UTANZANIA WANGU UNARUDI.
NILIPOKUWA AZANIA, NILIKULA CHIPS DUME NA JUISI ZA KUPIMA NA SIKUWAHI KUUMWA, DANDIA SANA DALADALA. KILA NIKIRUDI TANZANIA NAKULA KWA MAMA NTILIE, AMERIKAN CHIPS, NAENDESHA KAMA WABONGO, NAPNGA FOLENI MASAA KUNUNUA LUKU NA KULIPA MAJI, NAPATA ATTITUDE KUTOKA KWA BANK TELLERS, NATOKA TIP (RUSHWA) ILI NIPATE SERVICE, JUST LIKE EVERY OTHER TANZANIAN. I DON'T EXPECT NY IN DAR. DAR WILL ALWAYS BE DAR...NA ACHENI UBISHOLOLO WA KULALAMIKA LALAMIKA. MMEKULIA MPIGI MAGOHE HUKO...SASA HIVI MNAJIFANYA CUSTOMER SERVICES. AIRPORT WANAIBA...ACHA WAENDELEE WATAKULA WAPI...MIMI NIMESHAIBIWA MARA MBILI PALE AIRPORT...SIKUKASIRIKA KWA SABABU NI KAMA SADAKA...HUYU JAMAA ALIYEIBA, AKIUZA LABDA MTOTO WAKE ATAPATA VIATU VYA SHULE AU ATAKULA NYAMA. THIS IS ECOLOGY.
ACHENI KUNUNANUNA KIPUMBAVU - KUWENI WASTAARABU NA VIELIMU VYENU
nawewe mtema ngeli umenichekesha kwelikweli. you are a caracature yourself.
ReplyDeleteWatanzania kweli mnatia huruma, ofisi zaserikali kumeoza, customer care ni O na mkitaka kujua either utoke ila ukiwa huko akili inakuwa GIZAAAAAAAAA. Pole mdau mi niko nje ya nchi nilituma gari nikaweka mabegi na vyombo vya jikoni ndani yake, believe me tulipfika Tanzania ilibidi niifanyie familia yangu shopping ya nguo kwani walikuwa hawana, na si kwamba pale bandarini waliiba mabeg No walifungua/kuchana wakajishindia. Shame on u Tanzanian una dini kweli unae mpa mtoto wako vitu haramu? Ndo maana mnapatwa na mikosi ya kufa ghafla
ReplyDeleteNaona watoa maoni negative wengi humu ni wafanyakazi wa sekta alizotaja huyu mdau. Mbona yote aliyoyasema humu ni ya ukweli? We need a change in TZ for real, yaani tunaridhika na ujinga na ndiyo maana viongozi wanatuibia sie tunaona ni sawa tu. Watu inabidi waandamane kumpinga kikwete kwani ni sie wenyewe ndio tuliompa kazi sasa kwa nini hatimizi ama hazingatii malalamiko yetu? We are tired and we need a change.
ReplyDeleteMi sijasoma kama we mdau nakula boksi na hla yake inalipa ile mbaya. Naishi vizuri nakula vizuri lakini sichanganyi kiswanglish kama wewe. Customer service mbovu kila kona. Kuishi juu haina maana nd`o kuna serevice nzuri. Bongo unaweza kwenda hospitali ukatibiwa uk kumwona gp unaumwa kichwa mpaka upange ahadi. Hiyo ndo customer service gani. Kusoma si big deal na kudharau waso soma. Kama wote tukiwa na elimu ya juu, nani atafagia barabara? Kama kuishi kwako nje kumekufanya udharau watu basi hujasoma wewe.
ReplyDeleteUlaya kila kazi ina thamani hata ukifagia choo unaheshimika. Hakuna discrimination au racism. Wapo mablack wabaguzi kwa taarifa yako.
Mi nawachukia sana waswanglish na ntawalaaani waingie motoni. We umesoma usimdharau asosoma. Mnasoma mnasoma kitu gani.
Huyo mwingine naye eti oooh nina mtasha na hatubebi box? Aaaaargh...so wut? Kwani mtasha nd`o nini? Nguruwe wa kigogo na nguruwe wa Essex au Chester, Texas, huston ninguruwe tu. Wa kigogo atakula uchafu kama wa ulaya so big deal ipo wapi.
Ohh wahudumiaji kunduchi beach safi sana. Sasa nd`o tujue umefikia kunduchi beach na siyo uwanja wa fisi tandale, manzese (kunradhi ashakum si matusi wa tandale)
Kwa taarifa yako na wenye kujifanya; elimu ulaya ni we mwenyewe ukitaka unasoma hakuna vikwazo vya umri au pesa.
Kama umekomaa unaweza kuomba access to high education mwaka mmojaa unabundi ukimaliza upo uni. Hawataki kujua umefikaa kidato cha ngapi au ngwe ngapi msingi.
Msikondeshe watu. Eti watu wanavaa boogaloo style.maan, watu wamevaa kila style na nguzo zinauzwa kila style. Za kubana (slim fit) bwanga (loose) baggy ni style hizo nd`o zinazoendesha uchumi wa china leooooo.
Bado ntakuamkia kesho kwenye laptop hapa nakushushia kwenye tab.
Mi sijasoma kama we mdau nakula boksi na hla yake inalipa ile mbaya. Naishi vizuri nakula vizuri lakini sichanganyi kiswanglish kama wewe. Customer service mbovu kila kona. Kuishi juu haina maana nd`o kuna serevice nzuri. Bongo unaweza kwenda hospitali ukatibiwa uk kumwona gp unaumwa kichwa mpaka upange ahadi. Hiyo ndo customer service gani. Kusoma si big deal na kudharau waso soma. Kama wote tukiwa na elimu ya juu, nani atafagia barabara? Kama kuishi kwako nje kumekufanya udharau watu basi hujasoma wewe.
ReplyDeleteUlaya kila kazi ina thamani hata ukifagia choo unaheshimika. Hakuna discrimination au racism. Wapo mablack wabaguzi kwa taarifa yako.
Mi nawachukia sana waswanglish na ntawalaaani waingie motoni. We umesoma usimdharau asosoma. Mnasoma mnasoma kitu gani.
Huyo mwingine naye eti oooh nina mtasha na hatubebi box? Aaaaargh...so wut? Kwani mtasha nd`o nini? Nguruwe wa kigogo na nguruwe wa Essex au Chester, Texas, huston ninguruwe tu. Wa kigogo atakula uchafu kama wa ulaya so big deal ipo wapi.
Ohh wahudumiaji kunduchi beach safi sana. Sasa nd`o tujue umefikia kunduchi beach na siyo uwanja wa fisi tandale, manzese (kunradhi ashakum si matusi wa tandale)
Kwa taarifa yako na wenye kujifanya; elimu ulaya ni we mwenyewe ukitaka unasoma hakuna vikwazo vya umri au pesa.
Kama umekomaa unaweza kuomba access to high education mwaka mmojaa unabundi ukimaliza upo uni. Hawataki kujua umefikaa kidato cha ngapi au ngwe ngapi msingi.
Msikondeshe watu. Eti watu wanavaa boogaloo style.maan, watu wamevaa kila style na nguzo zinauzwa kila style. Za kubana (slim fit) bwanga (loose) baggy ni style hizo nd`o zinazoendesha uchumi wa china leooooo.
Bado ntakuamkia kesho kwenye laptop hapa nakushushia kwenye tab.
Upuuzi mtupu huko kwetu. Nilikwenda nyumbani TZ mwaka 2010 na mwanangu akiwa 3yrs ambaye amezaliwa huku ughaibuni, cha kwanza nilichokishangaa ni pale mtaani kusikia mwanangu anazungumza kiswahili pure!! Eti eeh kumbe kanaongea kiswahili?? Tunampeleka day care wenyewe wanatusisitiza kuongea naye mother tongue na kutuambia hizo lugha nyingine zote atazijua tu!! Sasa anazungumza hiyo english yao lakini nyumbani kwangu ni kiswahili kwenda mbele!! Hata mwenyewe automatic anaswitch language pale akikutana na haya mazungu mtaani! AM PROUD!!
ReplyDeleteMdau wa New York, yeye tunamchukulia kama mwana ndugu kwetu ametusaidia sana na cha msingi ame tusasambulia UOZO WETU...Sasa basi KWA UPANDE WA WAGENI ALIOKUJA NAO ,NDIO TUMEKWISHA CHAFUKA SANA TU, NA TUMEAIBIKA VIBAYA! LAZIMA TUKUBALI,,,
ReplyDeleteMfano kwa mazingira yetu huku nyumbani Bongo, kwa mara ya kwanza uende safari ukweni kijijini halafu upate mapokezi yasiyo stahili utawachukuliaje ukweni?
(USTAARABU HAUNA MNADA)!
HAWA WENZETU WANA MENTALITY YA KUDHIHIRISHA MAMBO YALIVYO,,,NA NI KUWA MAJI YAMEKWISHA MWAGIKA TUJIPANGE TENA!
HUNA LOLOTE ANONY WA Sat Dec 31, 03:06:00 AM 2011,,,UTACHAKAA NA MABOX YAKO TU! UTAMWAMKIA,,,UTAMWAMKIA KWA AJILI YA NINI,,,ACHA UMBEA WA U-TURN NA MABLOG YA KIHUNIHUNI! HAPA TUNAJADILI MAMBO YA MSINGI YA KUIJENGANA NCHI YETU,,,WATU WENGINE MNAUDHI....
ReplyDeleteMdau Pole sana na hawa wenye longolongo achana nao.Mradi umewasilisha inatosha hamna nchi ya kipuuzi kama Tanzania.Customer Service ni ujinga mtupu,yaani nisianze hapa ila kikubwa ni utawala ujue wanaowahudumia sio wapuuzi.
ReplyDeleteMwaka mpya mwema
ukweli utabakia kuwa ukweli..huduma kwa wateja tz ni sifuri.
ReplyDelete