Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo (kushoto) akimkabidhi nyaraka za serikali maalum kwa kuapishiwa na Biblia, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ili kuanza kuapishwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Nyaraka za Serikali, Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Ombeni Yohana Sefue, mara baada ya kumuapisha rasmi, leo Ikulu Dar es Salaam.
Balozi Ombeni Yohana Sefue, akiwa ukumbini wakati akisubiri kuapishwa rasmi kushika madaraka ya Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa katibu Mkuu kiongozi Ikulu Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia katika ukumbi wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, aliyeapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue na Balozi Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
ni kabila gani huyo semfue ?
ReplyDeletehatma ya aliyepita vp, kimya?
ReplyDeleteMtangabara
ReplyDeleteKabila la sefue ni mtanzania
ReplyDeleteKabila lake ni Mtanzania! Alie pita ameshastaafu, unataka nini tena? Zaidi tunafikiria kumpa kitengo fulani au awe balozi katika nchi fulani! Una Swali jingine?
ReplyDeletekabila ni mtanzania,huna haja ya kujua ethinic group zingine.acha ukabila
ReplyDeletendio maana akasubiriwa astaafu,hak una kitu tena ndio kaondoka.
ReplyDeletevipi Jairo kuundwa tume na kupoteza hela za wavujajasho kumbe changa la macho jamani?
Big up kwa balozi Ombeni. Binafsi nimefurahishwa sana na Uteuzi huu. Ninasikia amani ya ajabu moyoni. Sijui ni kwa nini
ReplyDeleteEmmanuel
mzee wa masifa sifa sana huyo, sizana kama ataweza
ReplyDeleteOmbeni Sefue kwa kabila ni mpare
ReplyDeleteHapo bwana mkubwa Sefuwe tunaomba kaka Ankali naomba irushe hii hewani.
ReplyDeleteChonde chonde fanya uwezalo kabla ya kustaafu kwako in three years time urudishe nidhamu na hadhi ya utumishi wa umma. Utumishi wa umma uko kwenye veryu bad shape sihitaji kukueleza hili. Najua ulikuwa kwenye ile timu ya Mh. Mkapa na unajua mambo mengi mliyooanzisha yalijifia yenyewe. Sasa kazi moja urekebishe mambo hapo ndani ya miaka mitatu.
Asante sana
Whats the secret behind tie zao.
ReplyDeleteLook as the PHOTOS VERY WELL.
That is what called "JAIROOOOOOOOO," and that is why I like CCM. They know how to play the game which is named POLITICS,"Kudadadeki." Let's wait the new Luhanjo's position after his retirement.
ReplyDeleteHongera sana Balozi wetu. Tunakutakia kila la heri kwenye kazi yako mpya. Tutakumiss wana jumia NY.
ReplyDeleteKwa kweli "nnji hii" kwa kuua soo nimewakubali,,,haki ya nani kwa utawala wa aina hii hatufiki popote! You guys are extra clever,,,lol!
ReplyDeletekwa hiyo anmuachia uklaji mtu mwingine,sio utumishi kwa umma
ReplyDeleteKaribu nyumbani tule nchi, New York ilikuwa mbali mno. Hakuna baya na ulaji, hiyo ndiyo hali halisi ya watumishi. Free housing,medicalcare, transport and Ths 20 million kwa mwezi. Mfanyakazi analipwa Th 125,000 kwa mwezi, mimi kwa kweli nashindwa kuelewa wanaishije, I don't get it at all.
ReplyDeletemheshimiwa nafasi za kina mama bado unafinya sana huko nyumbani ina maana hakuna wanawake wa kutosha kushika uongozi ama hii imekaaje ? something needs to be done to encourage more women into leadership positions ........
ReplyDeleteWho is reading this in 2020?
ReplyDelete